Eti Meli za mizigo 65 zilipotea bandarini na Serikali kukosa mapato yake,Du inauma sana

IT PROFESSIONAL

JF-Expert Member
Mar 17, 2016
228
95
Jamaa tujadili kidogo ,Nimemsikia Mheshimiwa Rais akisema eti kuna Mali 65 za mizigo ziliwahi kuyeyuka(kupotea) bandarini Dar ,na serikali imekosa mapato ,hizi inakuaje meli yenye mita zaidi ya 100 zipotee kirahisi ,why?
 
si hata contena lililojaa noti za 10000 limewahi kupotea na kutoweka kabisa pale airport!!?
 
si hata contena lililojaa noti za 10000 limewahi kupotea na kutoweka kabisa pale airport!!?

Hiyo "kupotea" labda ina maana tofauti hapa. Mzigo wa fedha lazima utakuwa umeagizwa na BOT na kushushwa kwa ulinzi mkubwa. Bila shaka gavana wa BOT anajua kontena la fedha lilikwenda wapi.

Nchi imeatawaliwa na wezi na wanyanganyi kwa miaka mingi. Nchi ambayo kontena zima la fedha linaweza kuingizwa nchini na kupotea ni nchi inayotawaliwa na kizazi cha nyoka. Binafsi naamini JPM sio sehemu ya kizazi cha nyoka lakini ameridhi watekelezaji wengi sana ambao ni kizazi cha nyoka. Mtukufu Rais, safisha BOT.
 
Hivi kontena linawezaje kupotea kama inavyopotea sindano ya mkono?

Only in Tanzania. Labda kulikuwa na mkanganyiko TRA kwenye kuliandikia ushuru. Aina ya mzigo - fedha. Hiyo haipo kwenye vitabu vyao labda. Ila ni kwa nini tubuni wakati waandishi wanaweza kumwuliza Ndulu? Au waandishi wetu wamekuwa mafarisayo wote?
 
Sasa ikitokea Rais ana komesha ushenzi huu
Wanatokea wapuuzi Fulani eti hatendi haki

Rais fumba macho ziba masikio kwa usalama wa Tanzania
TUMBUA MPAKA KIELEWEKE
 
How dare kitu kama meli kupotea bandarini? Huo ni mchezo ulichezwa watu wakapiga chao haiingii akilini kitu kama hicho kwa serikali ambayo iko makini katika utekelezaji na usimamizi wa shughuli zake za kila siku otherwise kama sio mchezo umechezwa tungeskia watu wamewajibishwa
 
Hazikupotea ndio maaana ikajulikana namba 65
Hili suala kama hupo mtu anaejua shughuli hizi za bandari na meli zinavoinhia na kuondoka labda atujuze kama inawezekana hili jambo
Atujuze
Meli ikiingia kuna taratibu gani kuanzia polisi wa bandari , namna inavopewa sehemu ya kushusha mzigo
Malipo yake yanafanywa vipo kwa cash au transfer au cheque
Namna Tiscan wanavo iingiza katiaka recodi zao
Malipo ya Pilot tug
Hapa tunahitaji mjuzi tupate ukweli
Isije ikawa meli zimeondoka kwa sababu ya urasimu na kwenda kushusha mombasa..
 
Back
Top Bottom