Eti Mbunge wa Kilwa nae ameunga mkono budget: Angalia shule za kwao za enzi za mawe

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Duniani kuna mambo, eti nae huo kaunga mkono budget
 

Attachments

  • Kilwa PICTURE.jpg
    Kilwa PICTURE.jpg
    422.3 KB · Views: 1,037
ajabu kaunga kwa 600% huku hakuna hata senti iliyotengwa kwa ajili ya shule hii.

Nakumbuka JJ alisema Dar kuna tatizo la maji ila kusini (Lindi na Mtwara) limezidi mno
 
Ninukuu maneno ya mwanamziki moja wa hip hop hapa tanzania aliimba hivi kwenye moja ya nyimbo zake '"...MACHOZI YALINITOKA SEGELA WATOTO HAWAPATI HAKI, WENGI WAMEKIMBIA SHULE, BASI ILI NKAUZE VISHETI WANAOSOMESHWA KWA MTAJI WA CHAPATI NA UVUVI WA SAMAKI,
WABUNGE WAO WAMEKAA NA WANAJIITA WANAHARAKATI????
RUDI KWENU UKAHAMASISHE NDUGUZO HAWANA TAARUMA,
WAZARAMO WAMEGOMA SOMA, STILL MWALI WANAMCHEZA NGOMA, WANALIA KILWA KIVINJE, HUKU WANAOCHEKA NI WABUNGE WALIONUNUA KURA YA BIBI KWA KUMUHONGA0 DOTI YA KITENGE.." mwisho wa nukuu.. Kwahiyo naona mheshimiwa wao anatimiza maandiko.
 
Ulitaka waunge mkono bajeti yenye mapato "0"? kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Maajabu ya nchi yetu. Ukiwasikiliza wabunge toka majimbo chokambaya huwezi amini kama wanao ongea ni wabunge wao.. Mimi nadhani nikuwarekodi ili siku vijana wao wakikata tamaa,wakataka kujitoa mhanga tuwaonyesha maneno ya wawakilishi wao.
 
Hawa wabunge nafikiri urimbukeni unawasumbua, halafu mbunge mwenyewe ni kijana kabisa!!! nilitegemea angekuwa msitari wa mbele kutetea masilahi ya vijana wenzake kule Kilwa ili wapate mahali pazuri pa kusomea lakini Zerooooooooooooooo!!. Hivi katika hali ya kawaida mtoto anayesomea shule kama hiyo unategemea kabisa ataelewa anachofundishwa??.

Lakini pia watu wa pwani tuache kujidekeza, hivi shule kama hiyo kujenga iwe nzuri kwa matofali ya kuchoma inahitaji pesa za kigeni?? Mbona wenzenu bara nenda mikoa ya kusini Iringa, mbeya na pia nenda kasikazini Moshi wananchi wamejitolea kwa nguvu zao na kujenga shule na nyumba za walimu bila kutegemea serikali. Hivi Pwani mnaogonjwa gani usiopona?????
 
ugonjwa wa akili ni mbaya, maana hupotezi hamu ya kula ila unakuwa hupendi kuoga.

Na unavaa magwanda ya khaki ya wawindaji wa kizungu na huku hupendi kuoga, hilo kwapa linakuwaje? hesabu zako bajeti mapato ni "0", eti sababu ni "taipu" kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Jadili Hoja iliyopo.Swala hapa sio Gwanda au Gamba. Muhimu ni Bajeti na Mustakabali wa TAIFA
 
Unajua hii ndiyo mitaji yetu sisi wana-CCM jamani tena hii shule ni nzuri sana ilitakiwa iwe imelala upande kama inataka kudondoka ili 2015 nikija na kanguzo kamoja naweka kuzuia isianguke nikigawa na t-shirt na vitambaa vya chama kwa walimu napita bila kupingwa kwahiyo bajeti iwe nzuri iwe mbaya naunga mkono kwa mia%. Kwanza kule bungeni sijuagi hata kinachoendelea
 
Back
Top Bottom