Eti mbunge mmoja wa CDM sawa na wabunge wote wa CUF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti mbunge mmoja wa CDM sawa na wabunge wote wa CUF

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Dec 5, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Kabla ya uchaguzi mkuu watu walikuwa wanafananisha wabunge 20 wa CCM sawa na mbunge mmoja wa CDM, sasa kuna maneno huku mitaani watu wanasema kuwa Mh. Tundu Lissu mbunge wa CDM ni sawa na wabunge 50 wa CCM, kwa hiyo Lissu anaweza kufananishwa kuwa sawa na wabunge wote wa CUF.
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Eti jumla ya kura zote za wabunge wa CUF hazifiki za jimbo la Ubungo, nasikia eti Pemba kila mtaa ni jimbo ya kweli hayo.
   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Kafu hawawafikii CDM katika idara zote kwenye idadi ya wapiga kura, idadi ya wabunge na vichwa vilivyotulia nitajie mpemba mmoja mbunge unayemtegemea.
   
 4. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  CDM huwawezi wewe kwa kujikwanza tungoje bunge lianze utaona utumbo wao
   
 5. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,052
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  WW MS fikiria mbuge ana represent watu 11,000
  halafu wa bara ana watu 192,000 say is like mmefanya mtihani mmoja wa marks 20% na wa 90% eti wanpewa zawadi sawa, where have you seen
  such a misconduct, ila kwa uelewa wako ni sawa naongea na Matonya ombaomba, somehow matonya is better of in thinking, na wana maneno hao, kila mtaa mbunge, tumewachoka, period
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahahahahah una maana ya Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden!
   
 7. D

  DENYO JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tusiandikie mate wino upo, huwezi kumlinganisha lissu na mch.rwakatare, kamata, ............................................................................................................................................................................wapo wengi tuu ni empty headed wapo kwa kazi moja kusema ndiyo na kupiga makofi
   
 8. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,052
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  ongezea na kulala na kupiga miayo (yawning) bungeni
   
 9. N

  Nonda JF-Expert Member

  #9
  Dec 5, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Wana JF

  Inaonekana kumbukumbu zetu ni fupi . Wenzetu wa Zanzibar wanapokuja na hoja za msingi huwa tunawaona wao ni « Mr. Bean »

  Walikuja na hoja ya 1+ 1 = 3. Baba wa taifa, Mwalimu alituhutubia, akasema wasikilizeni hawa wazanzibar ,wanasema « moja na moja ni tatu » huku anacheka na sisi ,tukampigia makofi.

  Unapolinganisha Zanzibar na jimbo la Ubungo, kimantiki umeanza na wrong/false premise na kwa hivyo conclusion yako pia itakuwa wrong.

  Tanganyika, ikiwa ni nchi iliungana na Zanzibar, ikiwa ni nchi.
  Jimbo la Ubungo halikuungana na Zanzibar. Ukisawazisha hapo na ukielewa kuwa huwezi kuitazama Zanzibar katika mtazamo unaolitazama jimbo la Ubungo , jimbo la Kawe au jimbo la Kiteto hutaweza kufanya dharau unayoifanya. Wala hutacheka, Utagundua kuwa « we have a wrong structure of the Union ».

  Kama tunashindwa kulifahamu hili kuwa Zanzibar ni Nchi kama ilivyo Tanganyika ndani ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania(Tanganyika na Zanzibar) basi itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gita.

  Sote tunaelewa kuwa kuna nchi ndogo zaidi ya Zanzibar duniani, kama Maldives, Mauritius, Sychelles lakini kwa utamu wa mada hii ni bora tuchukue East Timor na Indonesia, Tafiti mahusiano yao, au kwa mbali Hong Kong na China ( one country, two systems), pia tafiti mahusiano yao. Si vibaya pia kama utapitia historia ya UK (mahusiano yaliyopo baina ya Scotland, Northern Ireland, Wales na England)

  Ukishajifunza hayo ,utaona kuwa unayoongea na kushabikia ni vitu visivyopikika katika chungu kimoja, ni vitu visivyopimika katika mezania moja ya mantiki. Na kwa hivyo 20% to 90 % , theory , au ukubwa wa Jimbo la Ubungo na Zanzibar hapa itakuwa haifanyi kazi.

  Ukimaliza hayo, rudi katika mjadala wetu na tuendelee kijifurahisha.

  Jimbo la Ubungo kubwa kuliko Zanzibar ! Are we serious, guys?

  Mbunge wa Ubungo ana thamani zaidi, ni bora zaidi kuliko mbunge wa Mji Mkonge au Tumbatu. Mbunge mmoja wa CDM ni sawa na wabunge wote wa CUF !

  Ushabiki ni kitu maridadi kabisa.Ushabiki ni kileo. Ubaya wa ushabiki ni kuwa unampa mtu taabu ya kutenda haki na usawa, huwa analazimisha lazima mizani iinamie upande wake ! na atalazimisha hivyo, lazima i-tilt upande wake

  Waswahili wanasema , Mpenda chongo, huiita kengeza !

  Tutakaposhindwa kuona kuwa Mwalimu na ujanja wake wote kuwa alituuzia mbuzi ndani ya gunia, na tukashidwa kuchukuwa hatua ya kulisahihisha kosa hili, badala yake tukawa tunawatupia lawama na kuwalaani wazenj, tutakuwa hatuna tofauti na Mbuni.
  Mbuni anaficha kichwa chake ardhini wakati mwili wote unaonekana.

  Let us get serious, ladies and gentlemen !
  There is too much at stake, and there are serious issues to address.
   
 10. M

  Mwera JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sio kila mtaa nijimbo ni kila kaya nijimbo,pambaf kama kila mtaa nijimbo kungekua na wabunge lak2.
   
Loading...