Eti makundi ndo yanaitafuna CCM na kuipa ushindi CDM: Hiyo ni sahihi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti makundi ndo yanaitafuna CCM na kuipa ushindi CDM: Hiyo ni sahihi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vijijini Lawama, Apr 12, 2012.

 1. Vijijini Lawama

  Vijijini Lawama JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashindwa kuelewa nikisikia viongozi na wanachama wa CCM wakisema kuwa kinachowapa ushindi CDM ni makundi ndani ya Chama hicho.CCm ni chama kilichojaa wasomi wenye mashahada ya ajabu sana. Hivi unahitaji kumulikiwa na tochi kujua kwamba CCM wameshindwa kuongoza nchi na kuwaletea wananchi ustawi wa kijamii na kiuchumi na hiyo ndo chuki kubwa ambayo inawafanya washindwe katika chaguzi za hivi karibuni? Wasomi wa magamba wako wapi? Na magamba hawana tena uwezo wa kubadili hali hii kwa sababu tayari nchi inatembelea mguu mmoja kiuchumi wemekwiba vya kutosha na hawawezi tena kujenga viwanda na makampuni yaliyoachwa na wakoloni kwa muda mfupi ili kuishawishi jamii kuwaamini tena. Huduma za kijamii zimezorota na hata maisha yamekuwa aghali na jibu lao kubwa ni kuanguka kwa uchumi wa dunia, je uchumi wa dumia umeanguka Tanzania tu ambako mfumuko wa bei mkubwa kuliko.
  :A S-fire1:
   
Loading...