Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Nimekuwa nikifikiria hii dhana ambayo nimegundua ipo sana na kwa watu wengi kuwa inapotokea mwanamke au msichana akawa anamegwa sana mtaani kwao au maeneo anayoishi huonekana ni malaya, kicheche na majina kibao hupachikwa. Lakini inapotokea eneo hilo hilo kuna mwanaume au mvulana hodari wa kulamba mademu basi kwake ni tofauti huonekana kama ndio kidume cha mbegu na haonekani kama malaya kwa mitazamo ya watu. Hili limenikuta juzi tu nilikuwa safarini mkoani Iringa na pale nilipofikia mtaani kwetu nilikutana na kabinti kako vizuri sana kwa mtazamo wa nje na sikupoteza muda nikaanza operation mara moja lakini jamaa mmoja akaniambia mzee wewe hukai hapa sana huyo binti ni kicheche mbaya achana nae. Hali huwa tofauti kwa mwanaume akiwa mpenda mademu na hata mwanamke akijua jamaa anayemtokea ana sifa ya kumega sana mademu wengi nimegundua hujipeleka kiurahisi sana ingawa atakuwa akisononeka kuwa jamaa ana sifa ya ukoboaji sana.