Eti kutoka 80% hadi kuzomewa inakuwaje?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,898
USEMI wa Rais Jakaya Kikwete, alipochukua uongozi wananchi, kwamba anakusudia kuendesha uongozi wake
akijenga katika yale yaliyofanywa na mtangulizi wake, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, unaweza kuwa na tafsiri nyingi sana. Wakati alipotoa msemo huo, (utabakia kuwa msemo mpaka utekelezaji wa yaliyoahidiwa utakapoanza kuonekana), wengi waliufasiri chini ya matumaini yao juu yake na kuuona kama sehemu ya ahadi ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

Wakati huo watu tayari walikuwa wameshayapima kwa undani yale yaliyofanywa na mtangulizi wake. Hivyo
matumaini ya watu wengi yalikwenda kwenye muendelezo wa hayo na ndiyo maana watu walimuamini sana Kikwete alipoahidi kuwaletea kila mmoja wao maisha bora.

Na watu walifahamu nini kuhusu mtangulizi wa Kikwete? Walikuwa wakimfahamu Mkapa kama mtu ambaye alitumia muda wake wa uongozi kujenga uchumi wa Tanzania. Walimfahamu hivyo kutokana na yale yaliyofanyika ambayo yalikuwa yanaonekana dhahiri. Haikuhitajika kuwa na darubini au hadubini kuyajua hayo.

Katika kipindi cha miaka kumi ya kuwepo kwake madarakani, jambo kubwa na la msingi ambalo Mkapa
alilifanya ni kufanikiwa kuutengamanisha uchumi mkuu (macro-economy) .

Huu ulikuwa ni msingi ambao ulimjengea sifa ndani na nje ya nchi. Hapa nchini, hivi sasa, sifa hii ya
Mkapa, pamoja na nyingine nyingi, zimeanza kupata tafsiri nyingine baada ya upande wa pili wa shilingi
ya mambo aliyoyafanya Mkapa akiwa madarakani, kuanza kuwekwa wazi.

Tumesikia upande mmoja tu unaotoa tuhuma hizo, hatujasikia Mkapa mwenyewe anasema nini. Na haiyumkini
kuwa tutamsikia akisema. Lakini hata kama tunapaswa kufanya uamuzi kuhusu tulichokisikia na ushahidi wake, na kuamua kuwa Mkapa aliyafanya yote anayotuhumiwa kuyafanya, haitafuta sifa zake, ikiwamo hii ya
kuujenga uchumi mkuu.

Pamoja na mabaya yake yote (na kwa hakika anayo mabaya kwa sababu yeye ni binadamu tu), sifa hiyo itaendelea kuwepo na kudumu, hata kama baadhi ya watu hawatakubaliana na hilo.

Nalichukulia hili la kujenga uchumi mkuu kama msingi wa yote aliyoyafanya Mkapa, kwa sababu hilo ndilo
jambo ambalo lilikuwa na mwelekeo wa kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Na kwa watu wa kawaida, iwapo watapata mahitaji yao muhimu, mambo mengine wala hayatawasumbua sana.

Iwapo mtu ana uhakika wa mlo kila siku, anapata uwezo wa kulipia ada watoto wake, anaweza kuipatia familia
mahitaji yake yote muhimu na mwisho wa siku kuweza kuweka akiba, hata kama Mkapa aliiba mamilioni
mangapi, hayatamuathiri sana kisaikolojia.

Ila itamuuma sana iwapo maisha yake yatakuwa ya shaka. Kila mara, anapokuwa na uhitaji wa kitu fulani alafu
akakosa uwezo wa kukipata, mawazo yake yatamfanya aamini kuwa wizi uliofanywa na Mkapa ndio
unaomsababishia leo hii akikose kitu hicho.

Na ukiangalia alipofikia Mkapa katika kuujenga uchumi, aliwafikisha Watanzania mahali pa kuleta matumaini. Na
ninarudia kusema kuwa ndiyo maana Kikwete alipoahidi kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania akijenga katika
yale aliyoyakuta, watu walimuamini sana. Walimuamini kwa sababu waliyaona hayo ambayo yamejengwa na Kikwete kuyakuta. Waliona kuwa ilibakia kazi ndogo tu ya kuufanya uchumi mkubwa uujenge uchumi mdogo
(micro-economy) , ambao kimsingi ndio unaomjaza mtu mafedha mfukoni.

Na kwa jinsi ilivyokuwa, uwezo wa uchumi mkuu wakati Mkapa anaondoka madarakani, ulionyesha dhahiri kuwa
kazi ya kuujenga uchumi mdogo ni rahisi kwa kiasi fulani kwa sababu misingi ilikuwa imeshajengwa.

Mfumuko wa bei ulikuwa umeshuka kutoka tarakimu mbili na ulikuwa ukizidi kushuka. Hii ilimaanisha kuwa uwezo
wa mtu kununua (purchasing power) ulikuwa ukiongezeka.

Akiba ya fedha za kigeni nchini ilikuwa ya kuridhisha, iliyotoa uhakika wa uchumi wa nchi kuhimili misukosuko
ya muda mfupi na wa kati iwapo itabidi.

Makusanyo ya kodi yalikuwa yakiongezeka kila mwezi na kwa hakika kila mwisho wa mwaka, Mamlaka ya Mapato
nchini (TRA) ilikuwa ikitangaza kuvuka malengo iliyojiwekea.

Hii inamaanisha kuwa nchi ilikuwa na uwezo wa kulipia zaidi ya sehemu ya bajeti ambayo ilijipangia kulipia
na mapato ya ndani, ndiyo maana kila mwaka asilimia ya utegemezi katika bajeti ilikuwa ikipungua.

Thamani ya sarafu yetu ilikuwa inajizatiti. Ni kweli kuwa ilikuwa ikishuka, lakini si kwa kasi ambacho
tunaishuhudia hivi sasa. Hii ilionyesha kuwa mambo hayakuwa mabaya sana.

Lakini leo hii, takriban miaka miwili baada ya Kikwete kuingia madarakani tupo wapi? Mfumko wa bei unaelekea
kwenye tarakimu mbili, kule ambako Mkapa alitutoa. Hapa mtu unaweza kujiuliza ni jinsi gani Kikwete
anajenga uongozi wake katika yale aliyoyafanya Mkapa.

Ushahidi kwamba mfumko wa bei unapanda, unatolewa na Benki Kuu kila mwezi. Lakini hata katika maisha ya
kawaida, hili linaonekana. Bei za bidhaa zimepaa kiasi kwamba watu wameanza kujiuliza maswali mengi
yanayokosa majibu.

Mtafaruku kuhusu bei ya saruji wala bado haujatulia. Bei za vyakula zinabadilika kwa kasi kuliko kinyonga
anavyoweza kubadili rangi zake. Kibaya zaidi ni kuwa mabadiliko hayo yanahusisha si tu kupanda, bali
kupanda kwa tofauti kubwa mno. Leo si ajabu ukakuta bidhaa ikiwa imepanda bei mara mbili ya uliyoiona
jana.

Lakini serikali imekuwa haiishiwi na visingizio na kutoa matumaini kwa kutumia takwimu. Tulitarajia kuwa
hali ingekuwa mbaya mwaka jana baada ya msukosuko uliotokana na kukosekana kwa umeme. Lakini wakati wa
tatizo hilo, serikali yenyewe iliwatoa Watanzania wasiwasi na kuwaeleza kuwa kila kitu kilikuwa
kimedhibitiwa ipasavyo.

Na kama kawadia yao wakatumia takwimu, zilizoonyesha kupanda kwa makusanyo ya kodi ya kila mwezi
kuhalalisha kauli yao kuwa kila kitu kipo sawa. Hamkujua kuwa kutoyumba kwa uchumi wa nchi kulitokana
na misingi ya kuweka akiba ya kutosha fedha za kigeni kulikofanywa na Mkapa.

Leo hii uchumi wa nchi upo matatizoni. Hakuna kiongozi wa serikali au chama anayetaka kukiri hili hadharani.
Wengi wanauchukulia uchumi kama sehemu ya siasa wanazopiga majukwaani. Na ndiyo maana tunaumia na
tutaendelea kuumia iwapo viongozi wetu wataacha kuuona uchumi kama siasa.

Ndio wanauona uchumi kama siasa. Hii inatokana na jinsi wanavyotukoga. Haiwezekani mtu apange safari,
akiwa ametinga magwanda ya kijani kibichi na nyeusi, akitumia gari la serikali, alafu anasema kuwa
anaelezea uzuri wa bajeti huku hotuba yake ikianza na salamu za kidumu chama.

Uchumi haujui chama, unajua mipangilio na mambo kimahesabu. Ni utaalamu wa kimahesabu, si ujuzi wa
kupiga domo jukwaani. Wanaweza kuwa mabingwa wa kuelezea uzuri wa bajeti kwa lugha tamu,
zinazonakshiwa na vikorombwezo na vichekesho, lakini kama hesabu za kiuchumi hazijakaa sawa, kesho yake
itajionyesha wazi kwa mfumko wa bei kupanda.

Hayo maneno matamu hayawezi kuifanya thamani ya shilingi isishuke. Thamani ya shilingi itaendelea
kushuka na tofauti kati ya riba ya kuweka na kukopa kupanuka iwapo tutaishia kutoa maneno matamu jukwaani
bila kuchukua hatua za kuidhibiti hali hiyo.

Iwapo watafanya mambo yanayotakiwa kudhibiti viashiria vya uchumi, wala hawatahitaji wajuzi wa kutunga
mashairi ili kuwashawishi watu. Kila kitu kitaonekana dhahiri; hali ya mambo itabadilika, maisha yatazidi
kuwa bora na hapo hata wasipowaambia Watanzania lolote, watafahamu kwa kweli serikali yao ipo kazini.

Miaka miwili iliyopita, asilimia 80 ya Watanzania waliichagua serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
iliyopo madarakani. Huu ni ushindi ambao hadi hii leo bado umewalevya baadhi ya watu ndani ya CCM, kiasi
kwamba hawaachi kuutajataja kana kwamba shida za Watanzania zitamalizwa na asilimia 80.

Hivi hawa viongozi wameshawahi kujiuliza kwa nini hao asilimia 80 waliowachagua juzi tu, leo wanaanza
kuwazomea majukwaani? Yanatokea haya mara nyingi sana, na yanapaswa kuwa somo kwa viongozi wetu.

Lakini wao inaelekea wameamua wasiyaone. Inatisha sana kuwa wanaozomewa ni wao, lakini wakitoka hapo
wanakanusha kuwa hawakuzomewa! Hivi ni kuwa wamelewa sana madaraka kiasi kwamba kelele za kuzomewa wao wanaziona kama za kushangiliwa? Siamini.

Kuzomea huku ni aina fulani ya wananchi kutoa hasira zao. Na namna yao ya kueleza manunguniko yao. Lengo
lao ni kutaka kilio chao kisikiwe na viongozi. Lakini viongozi wasiposikia kuzomea huko, na hata kufikia
hatua ya kukanusha kuwa hawakuzomewa, wananchi watajua kuwa salamu zao hazijafika.

Watatafuta njia na mbinu nyingine ya kufikisha kilio chao. Na huu ndio utabiri ambao CCM siku zote imekuwa
wakiambiwa lakini hawataki kuamini. Kwamba ipo siku, wananchi ambao wanajihisi kudharauliwa kwa kiasi cha
juu na viongozi wao, ambao wakiwafikishia ujumbe na kilio chao hawakisikii, wataamua kutafuta njia na
mbinu nyingine ya kufikisha kilio chao. Watafanya nini? Ni vigumu kujua sasa.

Lakini ni dhahiri kuwa chaguo la watakachokifanya litakuwa si kuwakumbatia viongozi wasiowasikia.
 
Hii asilimia 80 ndio inawapa watu wengine kiburi cha ajabu bila kukumbuka kuwa Mwinyi alipata kura zaidi ya hapo!
 
...Lakini si Mwinyi alikuwa mgombea pekee.....

Yes Ngabu ni kweli Mwinyi alikuwa peke yake lakini "akapata kura zaidi ya asilimia 80". Kitu kinachomaanisha kuwa Mwinyi "alipigiwa" kura na percentage kubwa ya wapiga kura zaidi ya percentage ya "waliompigia" kura Kikwete.

Emphasis kwenye quotation marks! Hii inaonyesha kuwa Mwinyi "alipendwa" na wapiga kura kwa percentage kubwa kuliko ya Kikwete!
 
Lunyungu,
Nashkuru kwa Ushairi wako mzuri, lakini kuna mengi ya kujiuliza.

Uchumi (macro economy) umesema wakati wa BWM ulikua mzuri,
1. Tanzania kupitia Bureau of statistic ambayo ndio inakusanya data kama sio zote basi 80% for micro and Macro econmic projection hawa relaible sources of data. Nenda leo NBS waombe data price trends ya consumer goods, agricultural, industrial n.k uone kama wanazo hata BoT wenyewe hawana, Swali ni kwamba wanafanyaje calculation of Inflation, Economic Growth?

Kama kigezo cha kukua kwa uchumi ni kungezeka kwa mapato, Je mashirika ya serikali yaliuzwa na PSRC yaliingizia fedha nyingi sana serikali which may be sources of increase in revenue collection. Kukua kwa uchumi(economic Growth) is a necessary but not sufficient condition for Economic development maana kuna Suala la Income distribution, naamini utakubaliana na mimi hiki ndio kipindi income gap imekuwa kubwa zaidi, Can you call it maendeleo?

Kumekuwa na uuuzaji mkubwa wa migodi ya madini ambayo hata wewe umekuwa ukipiga kelele kila kukicha, hivi vyote vimeongeza pato la taifa kwa wakati huo sasa hivi Kikwete hana vya kuuza ndio maana nasikia kauza Serengeti walau aanzee na yeye kufidia hilo gap. Kama export ziliongezeka wakati wa mkapa y not this Time?

BWM hakutunga macroeconomic policies, wala Kikwete hajatunga macroenomic policies ni wachumi hao hao wa mkapa ambao bado wapo kwenye wizara na institution husika wakiendelea na sera hizo husika. naomba niishie hapa kwa sasa

Hoja hujibiwa kwa hoja
 
sasa hapa cha ajabu ni nini haswa ? mshasema 80% mbona hamfikirii hiyo 10% ?? hao ten pasenti ndio waliokuwa wakifanya huo upuuzi ! na sio wale wa 80% !!
 
Bowbow,
Bado kuna watu wanasherekea ushindi wa 80% mpaka leo, na kujiamini kuwa wanakubalika, kwa hiyo sishangai sana ukimuuliza mtu kuwa 'Mbona mambo hayaendi kama tulivyoahidiwa'?. Atakujibu, ina maana wewe humuamini muungwana? Ina maana huna uhakika kuwa tulishinda kwa tsunami?
Lakini ukiuliza 'tangible results' za ushindi huo utapata majibu ya kushangaza sana.
Wanaozomea sasa ndio wale walioahidiwa kile kisichoonekana. Ikumbukwe kuwa wazomeaji hawali takwimu. Kwam,ba uchumi unakua inatakiwa ionekane katika mfumo wa maisha ya mtu wa kawaida kabisa, sio katika vitabu. Sasa mtu kama hana uhakika wa milo mitatu kwa siku, atajisifuje kuwa uchumi wa nchi yake unakua? Tanzania yenye neema si ya miaka kumi ya awamu hii, ni awamu kadhaa zijazo baada ya hii.
Jaribu kuchokoza maswali hayo kwa badhi ya wana JF hapa.
 
Yes Ngabu ni kweli Mwinyi alikuwa peke yake lakini "akapata kura zaidi ya asilimia 80". Kitu kinachomaanisha kuwa Mwinyi "alipigiwa" kura na percentage kubwa ya wapiga kura zaidi ya percentage ya "waliompigia" kura Kikwete.

Emphasis kwenye quotation marks! Hii inaonyesha kuwa Mwinyi "alipendwa" na wapiga kura kwa percentage kubwa kuliko ya Kikwete!

Mwinyi ata kama angejipigia kura mwenyewe nyingine zote zingeharibika bado angeshinda kwa ushindi mkubwa(funny stuff isn't it?)
 
BWM hakutunga macroeconomic policies, wala Kikwete hajatunga macroenomic policies ni wachumi hao hao wa mkapa ambao bado wapo kwenye wizara na institution husika wakiendelea na sera hizo husika. naomba niishie hapa kwa sasa

Heshima kwako mkuu BOWBOW
Ukumbuke kuwa magari yote yametengenezwa kwa kutimia principle sawa, lakini tofauti ya madereva ndiyo inafanya mengine yanende kwa kasi mengine yasiende kwa kasi, mengine yaanguke na mengine yasianguke, mengine yadumu na mengine yasidumu. Sera karibu zote za Uchumi ziko kwenye biblia ya uchumi aliyoiandika Smith (Material wealth), kikwete hajatunga hata moja na wala BWM hakutunga hata moja, isipokuwa alichagua zinazofaa mazingira ya Tanzania nakuweza kuzitekeleza. Lazima tukubaliane kuwa BWM aliunda timu nzuri ya wasomi, watekelezaji na wasimiamiaji wa sera za uchumi, ndio maana Tanzania iliondoka kutoka kwenye uchumi wa ovyo na kuwa na uchumi walau unaoneleweka. Nilimsikia siku moja kwenye hotuba yake akisema anapenda kuona mfumuko wa bei Tanzania unakuwa kwenye asilimia 4, na alijitahidi kufanya hivyo. Wakati wa kipindi chake hakukuwa na mfumuko wa bei wa kutisha.
Lakini angalia timu aliyounda JK sasa hivi, wamo wale waliokuwa wabovu wakati wa Ben, na aeongeza kina Karamagi, na kuwapa Wizara nyeti watu kama kina Meghji, unaweza kushangaa ni kwanini amefanya hivyo, lakini huwezi kushangaa kuona mambo yanaenda ovyo kwa sababu make up ya cabinet inaonesha kuwa hayo niya kutegemea kabisa.
 
BRAZA LUNYUNGU,UR THREAD WAS FANTASTIC, AM A KEEN FOLLOWER WA MAMBO YANAYOENDELEA NCHINI KWETU EVEN THOUGH NIPO KAMPALA KIMASOMO.DESPITE THE FACT THAT WATU WANAMTUHUMU KWA UFISADI BEN LAKINI TO BE HONEST THE MAN STILL REMAIN NI MTU WA VITENDO NA SIO MANENO SANA, KAMA ULIVOKIRI YEYE KAMA BINADAM HAKOSI MAPUNGUFU TENA PENGINE NAFIKIRI KUWA WATU WANAYASEMA SANA AS FAR AS DURING HIS REGIME HAKUWA KTK GOOD TERMS NA WADAU WAKUU WA KUWAPASHA HABARI WANANCHI i.e WAANDISHI WA HABARI, HENCE THERE FORE NADHANI UTAJUA WHAT FOLLOWS MKUU AKITOKA MADARAKANI.
MKUU WETU WA KAYA IS TOO MUCH POLITICAL,NA SINS HAKIKA SANA NA HOW MUCH POTENTIAL IS HE!,LEAVE ALONE THAT,MISTAKE NAMBA TWO NI POTENTIAL YA WASAIDIZI WAKE, HOW MUCH ABLED THEY ARE?,MI NADHANI KUWA NA CABINET, NA WASHAURI WA SALIENT SECTORS BORA NI CATALYST NA KU ACHIEVE DVLPT, ASA KAMA UNAKUWA NA MSHAURI WA MAMBO YA KIUCHUMI AMBAYE HANA EXPERIENCE YA KAZI ATA ZAIDI YA MIAKA KUMI, WHAT DO YOU EXPECT KWA NCHI MASKINI KAMA TZ? UNATEGEMEA NINI KAMA MKUU WETU ANAHAMISHA FOREIGN KA ILIVO NA KUIWEKA STATE?DESPITE THE FACT ATA WAWE NA POTENTIAL KIASI GANI,USWAIBA KTK MATAZ OF STATE WAPI NA WAPI?
TO BE HONEST HALI NI MBAYA KAMA ULIVO BAINISHA NA MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA,U KANT IMAGINE WITHIN MIAKA MITATU PESA YETU VERSUS HELA YA UGANDA INAZIDI KUDROP TU.. FOR ALMOST 0.6,HUWAGA NAWAZA IVI AWA WAUNGWANA NA MATATATIZO YAO YOTEEEEEEEE, VITA, NJAA, UFISADI.NK INAKUAJE WANATUSHINDA SISI INHALI TUNA ALMOST KILA SEKTA TUMEWAZIDI, KUANZIA VIWANDA, MADINI,MBUGHA ZA WANYAMA,ETC?JIBU TNALO WENYEWE WA TZ..
THE WAY FORWARD;NICOLLO MACHIAVELLI ITALIAN PHILOSOPHER ALIOSEMA..... IS BETTER TO DEAL WITH THE DEVIL YOU KNOW THAN THE ANGEL YOU DONT KNOW.....WAUNGWANA NA WEB KA HIZI NI MHIMU SANA KTK KUISADIA NCHI YETU,IDARA NA TAASISI MBALIMBALI ZA KISERIKALI[INCL..NGOs] LAZIMA WA PLAY PART YAO FANTASTICALLY,AWA WAKUU WETU AMBAO WANACHOMA MAFUTA YA WANANCHI KWENYE MASHANGINGI KILA UCHWAO LAZIMA WASOME[REF;MAKALA YA ULIMWENGU],SIO KUISHIA KUSOMA IJUMAA WIKIENDA[KAMA LIPO BADO],KUKAA N AQULIFICATIONS BILA KUJISHUGHILISHA NI SAWA LA MVINYO WA ZAMANI KTK CHUPA MPYA, THTS WHY WAKISEMA HIVI WEWE TAWILE TUU AS FAR AS YOU ARE UNABLE TO IDENTIFY WHAT TO DO AND WHAT NOT TO DO...
THANX KAKA LUNYUNGU FOR YOUR BRILLIANT THREAD!..MWENYE MACHO.............
 
Miaka miwili iliyopita, asilimia 80 ya Watanzania
waliichagua serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

iliyopo madarakani. Huu ni ushindi ambao hadi hii leo
bado umewalevya baadhi ya watu ndani ya CCM, kiasi
kwamba hawaachi kuutajataja kana kwamba shida za
Watanzania zitamalizwa na asilimia 80.

Mkuu Lunyungu,
Hapo utakua umekosea sana mkuu! SI ASILIMIA 80 ya WATANZANIA! Ni ya wapiga kura mkuu,

JK mwenyewe inaezekana anajua ni asilimia 80 ya Watanzania.Ila hata yeye anajua amekamatika ndio maana hata akizomewa anajifanya hafeel kitu.Aliahidi mbingu na nchi kisa madaraka sasa watakoma ila wakubali lawama tu.

Ten years mtu akirudisha maendeleo nyuma? halafu ajitutumue kukwepa lawama?Haiwezekani labda abadilike haraka
 
Back
Top Bottom