Eti Kulala Pamoja si Afya! kwa wana NDOA

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,955
22,128
Eti Kulala Pamoja si Afya!

Tafiti za karibuni zinaonesha kwamba wanandoa kulala kitanda kimoja si afya kama kila mwanandoa yaani mke na mume kulala kila mmoja kitandani chake mwenyewe.

Kitendo cha wanandoa kulala kitanda kimoja kilianza wakati wa mapinduzi ya viwanda (industrial revolution) kitu kilichosababisha watu kuhamia katika miji na kujikuta wanakosa accommodation na kulazimika mke na mume kulala kitanda kimoja.

hali hiyo imeendelea hadi leo na kuwa kama mfumo ambao watu wakioana tu huamua kulala kitanda kimoja.

Pia bado baadhi ya jamii zinazoishi vijijini mke na mume huendelea kulala kila mmoja kitanda chake hadi leo.

Kwa wastani wanandoa wanaolala pamoja huweza kusumbua mwenzake (disturb) nusu ya usingizi anaotakiwa kulala kama kila mmoja angelala kitanda chake.

Wanandoa kulala pamoja huweza kusababisha kusumbuana na hatimaye kusababisha magonjwa kama vile kuchoka, magonjwa ya moyo. Depression, stroke. Matatizo ya kupumua nk.

Pia historia inaonesha kwamba kitandani hakukuwa mahali pa kulala wanandoa bali ilikuwa sehemu muhimu (maalumu) ya wanandoa kukutana pamoja kwa ajili ya kuwa mwili mmoja (tendo la ndoa) na si wanandoa kulala pamoja.

Daktari wa sociology kutoka chuo kikuu cha Surrrey Dr. Robert Meadows anasema kwamba watu hujisikia vizuri wakilala kitanda kimoja na wapenzi wao hata hivyo ushahidi ni kwamba kulala kitandani kimoja si afya.

Je, unaonaje suala Hili la kulala kila mwanandoa kitanda chake mwenyewe?
 
Kama ukiwa na mpenzi anayekoroma au anageuka geuka sana usingizini lazima utakuwa unakosa usingizi, mwisho wa siku utakuwa mchovu.

Kuna jamaa nafanya naye kazi yuko kwenye ndoa mwaka wa 13 huu lakini yeye na mkewe hawalali chumba kimoja kwa sababu jamaa anakoroma sana.
 
haya ni makubaliano at the end of the day, lakini pia mi naona ingekuwa poa tu maana navyopenda usingizi wangu usiwe disturbed, na pia space ni muhimu sana kwangu linapokuja swala la kulala.
 
haya ni makubaliano at the end of the day, lakini pia mi naona ingekuwa poa tu maana navyopenda usingizi wangu usiwe disturbed, na pia space ni muhimu sana kwangu linapokuja swala la kulala.

HILI SWALA HAMNA ANAEBISHA!hahahahaha
 
you got it mpwa, by the way jana hujaonekana, vp?
jana nilikuwa tait kiduchu!leo pia lakini nitajaribu kuibia ka muda kidogo!kuna mtu nasikia alinitukana sana.sasa tangu jana usiku naitafuta hiyo post siioni!unaweza ukawa unaikumbuka?
 
Kulala pamoja watu wawili wa jinsia tofauti ni raha jamani khaaa!!Hizi tafiti nazo zinataka kutibua tu.
 
Kulala pamoja watu wawili wa jinsia tofauti ni raha jamani khaaa!!Hizi tafiti nazo zinataka kutibua tu.
kuna kipindi mwanamke anataka sex,HALAFU MWANAUME HANA MOOD!hapo ndipo utaona uchungu wa kulala wawili
 
kuna kipindi mwanamke anataka sex,HALAFU MWANAUME HANA MOOD!hapo ndipo utaona uchungu wa kulala wawili

Mwanamke lazima awe anajua namna ya kukuweka kwenye mood mara anapotaka sex! Huyo anayekurupuka tu inamaana hajafundwa? Ndiyo kati ya mambo ambayo Jando na Unyago enzi zile vijana walikuwa wakifundwa. Siku hizi mmekutana kwenye daladala,disco,sherehe za harusi, mara house party tayari tunabebana , Demu/Jamaa anakupa mambo safi unapagawa, miezi miwili tu NDOA, Hapo fikiria mwenyewe kitakachotokea................
 
kuna kipindi mwanamke anataka sex,HALAFU MWANAUME HANA MOOD!hapo ndipo utaona uchungu wa kulala wawili

huyo mwanaume atakuwa mzembe tu, mwanamke atake halafu yeye hana mood. Na wakati wanaume wanatafuta bahati za kuwa na mwanamke anayeanzisha kutaka mchezo.
 
kulala pamoja watu wawili wa jinsia tofauti ni raha jamani khaaa!!hizi tafiti nazo zinataka kutibua tu.
na kweli..
Ile kugusana na kijimwili laini...
Hakika kunaleta burudani, labda huyo mwenzi wako uwe humpendi ndio utaona karaha ya kulala pamoja
 
huyo mwanaume atakuwa mzembe tu, mwanamke atake halafu yeye hana mood. Na wakati wanaume wanatafuta bahati za kuwa na mwanamke anayeanzisha kutaka mchezo.

umeolewa dada angu?
 
hii nimebali......kisaikolojia unaweza kuona raha kulala na mwenzio.....lakini ki afya ni mbaya, mwanamme pengine heshi kugeuka na kukoroma! dada wa wat hujazowea kupumuliwa na pumzi ......
 
hii nimebali......kisaikolojia unaweza kuona raha kulala na mwenzio.....lakini ki afya ni mbaya, mwanamme pengine heshi kugeuka na kukoroma! dada wa wat hujazowea kupumuliwa na pumzi ......

Hivi wanawake huwa hawakoromagi? Ish!
 
Back
Top Bottom