Eti Kubaki vituoni kulinda kura ni ishara mbaya

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,986
1,190
Historia au kumbukumbu ni walimu wazuri,kwenye kura za maoni za majuzi tu ndani ya CCM tunaambiwa wanaccm walilinda kura zao usiku kucha.Swali liko hv kwa nn wanaccm hawa waliamua kulinda zao,jibu rahisi tu ni kwamba wanujua mchezo huu kwa undani zaidi kuwa ndio tabia iliyojengeka ndani ya ccm.Tume imeteuliwa na wana ccm.Swali la msingi unawezaje kumuaminisha asiye mwana CCM asilinde kura wakati wakati hata wanaccm wenyewe hawaaminiani hata kidogo hata kufikia hatua ya kukesha wakilinda kura zao kwenye uchaguzi wa ndani wa kuchagua wagombea watakao pambana oktoba mwezi huu.NB:kulinda kura ni lzm mita mia kadiri ya sheria.Tuheshimu sheria hii.
 
kama huyu mtu mzima amechona na anapingana na sheria bora tumpeleke jumba la makumbusho akapumzike. lazima tulinde kura. kama ma mcc yanaibiana yenyewe yatashindwa nini kuiba kura z edo?
 
Kama sheria inaruhusu sijui kigugumizi kinatoka wapi, kulinda kura ni wajibu wa mpiga kura
 
Kwa hiyo kauli za tume zinavunja sheria na ndio chanzo cha uvunjifu wa amani oktoba 25 NEC ijipime kwa mujibu wa sheria na ijue watanzania wanaheshimu sana sheria hiyo ya mita mia na wataendelea kuiheshimu hata ktk uchaguzi huu.
 
kati ya watanzania kumi ktk kundi fulani mmoja tu ndio mwanaccm,ndio maana ccm inahaha sijui kwa nn wakati wenye mamlaka wametamka wazi kuwa hawaitaki ccm iliyojaa watu wenye viburi vya kutisha.
 
Mimi nauliza kama wanataka watu waondoke vituoni sasa hizo kura na matokeo wanazosema watatangaza vituoni je wanataka wamtangazie nani kama wanataka watu waondoke vituwoni??
 
Zinalindwa mpaka kieleweke sisi tutakuwa tunazunguka kila kituo kuwahaamasisha wafate sheria ila wabaki eneo la tukio
 
Historia au kumbukumbu ni walimu wazuri,kwenye kura za maoni za majuzi tu ndani ya CCM tunaambiwa wanaccm walilinda kura zao usiku kucha.Swali liko hv kwa nn wanaccm hawa waliamua kulinda zao,jibu rahisi tu ni kwamba wanujua mchezo huu kwa undani zaidi kuwa ndio tabia iliyojengeka ndani ya ccm.Tume imeteuliwa na wana ccm.Swali la msingi unawezaje kumuaminisha asiye mwana CCM asilinde kura wakati wakati hata wanaccm wenyewe hawaaminiani hata kidogo hata kufikia hatua ya kukesha wakilinda kura zao kwenye uchaguzi wa ndani wa kuchagua wagombea watakao pambana oktoba mwezi huu.NB:kulinda kura ni lzm mita mia kadiri ya sheria.Tuheshimu sheria hii.

kulinda kurA NI LAZIMA LA UKAWA WANATAKA KUTEKA IKULU. HUWEZI KUAMINI KUNA USALAMA HALI UNAONA MTU KAKATWA MKONO HALAFU MTU HUYOHUYO ANAKUAMBIA USIWE NA WASIWASI HUKATWI MKONO . HUO NI UCHURO AKILI ZA KUAMBIA NA JAJI DAMIAN LUBUVA CHANGANYA NA KWAKO, QUOTES" JMK"- WAZEE WA DAR-ES-SALAAM MWAKA 2010
 
Back
Top Bottom