Eti Kisukuma kina wazungumzaji wengi kuliko Kiswahili

hahahahaaaaa! le profeseri! huyu profesa anataka kutuambia jiju la dsm kuna watu wengi wasiojua kiswahili???? chukua idadi ya watu wanaokaa mijini tu ambao wote wanajua kiswahili wanazidi milioni kumi. hata hao wasukuma mfano chenge anajua kiswahili. Hatariiiii, prof.
 
Utafiti unasema kuwa lugha ya kisukuma ndio inazungumzwa na watu wengi kuliko kiswahili.

Na Abeid Poyo

MRADI wa Lugha za Tanzania (LoT) umezindua atlasi ya lugha na kuitaja lugha ya Kisukuma kuwa na wazungumzaji wengi nchini.

Katika uzinduzi huo uliofanyika jana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lugha ya Kisukuma ilitangazwa kuwa na wazungumzaji wapatao 5, 195, 504 ikifutiwa kwa mbali na lugha ya Kiswahili yenye wazungumzaji 2,379,294

Akizungumza katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa lugha kutoka ndani na nje ya nchi, Mratibu wa mradi huo, Prof Josephat Rugemalira alisema atlasi hiyo ya aina yake inatoa picha halisi ya idadi ya lugha zilizopo nchini, wazungumzaji, maandiko, usambaaji wake na maelewano ya karibu ya lugha.

“Atlasi ya lugha za Tanzania ni kiungo muhimu katika mkakati wa wa kuzitambua na kuzitathmini rasilimali zetu za utamaduni”, alisema Prof Rugemalira na kuongeza kuwa, uzinduzi wa atlasi hiyo unatoa picha halisi ya maendeleo ya sekta ya lugha nchini.

Kwa mujibu wa Rugemalira, atlasi hiyo ni matokeo ya utafiti wa miaka kadhaa wa mradi huo ulio chini ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alibainisha kuwa utafiti huo pia ulibaini kuwepo kwa lugha 150 hapa nchini huku baadhi yake, kama vile lugha za Wanda, Kiga, Kikuyu na Bwali zikiwa hatarini kufa kwa kukosa matumizi.

Alifahamisha kuwa lugha hizo zimekumbwa na hali hiyo kutukana na mambo mbambali ikiwemo lugha hizo kumezwa na lugha kuu.

Katika hafla hiyo, machapisho 20 zikiwemo kamusi 18 za lugha za asili zilizinduliwa na Balozi wa Sweden nchini Staffan Herrstrom aliyekuwa mgeni. Hafla hiyo ilikwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Lugha Mama duniani.


Source: Gazeti la Mwananchi

Wazo langu:
Utafiti huu bila shaka haukuangalia overlap ya hizi lugha, kama kuna watu wanaozungumza kiswahili na lugha zingine ikiwemo kisukuma chenyewe au ulilenga kwa wale wanaozungumza kiswahili tu bila lugha nyingine, na kisukuma tu bila kiswahili? Ina maana wasukuma wengi hawajui kiswahili?

Hizi tafiti sijui wana cook data chumbani!!! Aibu hata kusoma matokeo yake. Yaani Kiswahili kiwe na wazungumzaji milioni 2 na Kisukuma milion 5? Duh...Yaani hata Dar es Salaam yenye zaidi ya watu milion 4, ina maana wazungumzaji wa Kiswahili hawafiki nusu yake. Uongo huu...
 
Huu ni upotoshaji mkubwa,ni utafiti wa kijinga na prof. Rugemalira huenda si jagina na abtali mbobezi wa lugha hii adhimu. Kiswahili ni lugha ya Taifa na lugha rasmi Tanzania. Sababu ya kuteuliwa kwake ni kuenea na kuwa na wazungumzaji lukuki. Kiswahili ni Lugha ya inayofndshwa tangu elimu ya chekechea hadi Vyuo Vikuu. Aidha ni lugha inayofundishia masomo yote ya elimu ya msingi na Vyuo vya Ualimu astashahada isipokuwa somo la Kiingereza ukiachia mbali vyuo vya ufundi. Je,ni wahitimu wangapi wanahitimu kila mwaka? Kuna mhitimu anayehitimu bila kujua Kiswahili? Kiswahili ni lugha mama. Watu wanakimudu kwa kurithi bila kufundshwa. Kiswahili ndio lugha kuu Tanzania inayowaunganisha watanzania wote bila kujali lugha Zao. Kinawaunganisha watanzania katika shughuli za maendeleo,mf. Biashara,utamaduni,uchumi,kilimo,elimu,mawasiliano(usafiri na vyombo vya habari),siasa n.k. Hii ni sawa na kusema kuwa Kiswahili kimemeza lugha zote za kibantu. Hitimisho,utafiti uliofanywa kuwa Kisukuma kina wazungumzaji wengi ni utafiti butu na si utafiti wa kisomi labda kwa maslahi fulani
 
Hapa nadhani kuna kitu muhimu sana kilikosekana, nacho ni kile kisemacho idadi ya watu wanaozungumza Kisukuma kama lugha ya kwanza. WaTz wengi wanaongea lugha zaidi ya moja, na ukiwauliza lugha ya kwanza ni ipi atakutajia ile ya kabila lake, halafu akaja Kiswahili halafu English akajifunzia shuleni. Sasa, ni watu kiasi gn wanazungumza Kiswahili kama lugha ya kwanza (mother tongue) na kiasi gani wanazungumza Kisukuma kama lugha ya kwanza aliyoanza kuongea alipokuwa mtoto, hapo ndipo Kisukuma kinamtoa Kiswahili. Haihitaji jazba kung'amua mambo kama hayo.

Mwisho kbs mwa habari hiyo wamesema "Hafla hiyo ilikwenda
sambamba na maadhimisho ya Siku ya Lugha Mama duniani"

Kama hukusoma Lugha huenda usielewe, sasa usitumie jazba, soma kwanza kuhusu First language (mother tongue) na second language (L2). Halafu ujiulize ww na wenzio kwenye family yenu, lugha yenu ya kwanza ni ipi!
 
Ni kwamba kisukuma kinaongoza kwa kwa kuwa na waongeaji wanaokitumia kama lugha yao ya kwanza tofauti na kiswahili kina waongeaji wengi lkn sio lugha yao ya kwanza …[mother tongue]

wengi wetu hujifunza kiswahili lkn kisukuma hawajifunzi ila wanakua nacho ndo maana kinaongoza kuwa na `native speakers wengi ` kuliko kiswahili
 
Ndugu,
HEBU ACHA JAZBA
Ni kwamba kisukuma kinaongoza kwa kwa kuwa na waongeaji wanaokitumia kama lugha yao ya kwanza tofauti na kiswahili kina waongeaji wengi lkn sio lugha yao ya kwanza …[mother tongue]

wengi wetu hujifunza kiswahili lkn kisukuma hawajifunzi ila wanakua nacho ndo maana kinaongoza kuwa na `native speakers wengi ` kuliko kiswahili
 
Ndugu,
HEBU ACHA JAZBA
Ni kwamba kisukuma kinaongoza kwa kwa kuwa na waongeaji wanaokitumia kama lugha yao ya kwanza tofauti na kiswahili kina waongeaji wengi lkn sio lugha yao ya kwanza …[mother tongue]

wengi wetu hujifunza kiswahili lkn kisukuma hawajifunzi ila wanakua nacho ndo maana kinaongoza kuwa na `native speakers wengi ` kuliko kiswahili

Kuwa mpole tu kaka, watu hawaelewi na hawataki kuelewa maana ya lugha mama (mother tongue) na lugha ya pili (second language). Hata huyo anayebisha ukimuuliza lugha ya kwanza aliyoanza kuongea alipokuwa mtoto atakutajia ya kabila lao na sio Kiswahili lkn hapa atabisha tu maana haelewi.
 
Kuwa mpole tu kaka, watu hawaelewi na hawataki kuelewa maana ya lugha mama (mother tongue) na lugha ya pili (second language). Hata huyo anayebisha ukimuuliza lugha ya kwanza aliyoanza kuongea alipokuwa mtoto atakutajia ya kabila lao na sio Kiswahili lkn hapa atabisha tu maana haelewi.
Ilonga,
Hata kama unazungumzia ''mother tongue'' bado tu kiswahili kina waongeaji wengi. Una habari sehemu nyingi za vijijini kama Kilimanjaro kiswahili ndio kimekuwa ''mother tongue'' na kichaga ndio lugha ya pili? Siku hizi watoto wengi wanatumia kiswahili zaidi ya kichaga. Sasa ukichanganya na sehemu karibu zote za miji ya Tanzania ambazo watoto wanatumia kiswahili zaidi ya lugha za wazazi wao. Unataka kusema mtoto aliyezaliwa na wazazi wa kisukuma kwa mfano Dar atatumia lugha ipi zaidi kama si kiswahili (hata kama wazazi wake nyumbani watakuwa wanatumia kisukuma).
 
Nimeelewa alichokimaanisha Prof, lakini bado utafiti huu una walakini, unless huu utafiti uwe wa 1978, na sio 2009
 
Back
Top Bottom