Eti Kisukuma kina wazungumzaji wengi kuliko Kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Kisukuma kina wazungumzaji wengi kuliko Kiswahili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MpigaFilimbi, Feb 22, 2009.

 1. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Utafiti unasema kuwa lugha ya kisukuma ndio inazungumzwa na watu wengi kuliko kiswahili.

  Na Abeid Poyo

  MRADI wa Lugha za Tanzania (LoT) umezindua atlasi ya lugha na kuitaja lugha ya Kisukuma kuwa na wazungumzaji wengi nchini.

  Katika uzinduzi huo uliofanyika jana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, lugha ya Kisukuma ilitangazwa kuwa na wazungumzaji wapatao 5, 195, 504 ikifutiwa kwa mbali na lugha ya Kiswahili yenye wazungumzaji 2,379,294

  Akizungumza katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa lugha kutoka ndani na nje ya nchi, Mratibu wa mradi huo, Prof Josephat Rugemalira alisema atlasi hiyo ya aina yake inatoa picha halisi ya idadi ya lugha zilizopo nchini, wazungumzaji, maandiko, usambaaji wake na maelewano ya karibu ya lugha.

  “Atlasi ya lugha za Tanzania ni kiungo muhimu katika mkakati wa wa kuzitambua na kuzitathmini rasilimali zetu za utamaduni”, alisema Prof Rugemalira na kuongeza kuwa, uzinduzi wa atlasi hiyo unatoa picha halisi ya maendeleo ya sekta ya lugha nchini.

  Kwa mujibu wa Rugemalira, atlasi hiyo ni matokeo ya utafiti wa miaka kadhaa wa mradi huo ulio chini ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  Alibainisha kuwa utafiti huo pia ulibaini kuwepo kwa lugha 150 hapa nchini huku baadhi yake, kama vile lugha za Wanda, Kiga, Kikuyu na Bwali zikiwa hatarini kufa kwa kukosa matumizi.

  Alifahamisha kuwa lugha hizo zimekumbwa na hali hiyo kutukana na mambo mbambali ikiwemo lugha hizo kumezwa na lugha kuu.

  Katika hafla hiyo, machapisho 20 zikiwemo kamusi 18 za lugha za asili zilizinduliwa na Balozi wa Sweden nchini Staffan Herrstrom aliyekuwa mgeni. Hafla hiyo ilikwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Lugha Mama duniani.


  Source: Gazeti la Mwananchi

  Wazo langu:
  Utafiti huu bila shaka haukuangalia overlap ya hizi lugha, kama kuna watu wanaozungumza kiswahili na lugha zingine ikiwemo kisukuma chenyewe au ulilenga kwa wale wanaozungumza kiswahili tu bila lugha nyingine, na kisukuma tu bila kiswahili? Ina maana wasukuma wengi hawajui kiswahili?
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Huyo aliyefanya Utafiti ana wazimu unless wana maana lugha ya kwanza kwa uzawa!..
  1. Asilimia kubwa ya hao hao wasukuma wanazungumza kiswahili!
  2 Kama Tanzania ina population ya millioni 40 ni zaidi ya asilimia 90 (kwa makisio yangu) wanazungumza kiswahili acha mbali kuwa lugha yao ya kwanza. Bado hujagusa huko Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Kongo..
  Karibu kila taifa kubwa siku hizi kuna shule zinafundisha lugha ya kiswahili ikiwa ni pamoja na Marekani, Ujarumani, Canada, Sweden yaani hata sielewi wanaposema Kiswahili kina WAZUNGUMZAJI 2,379,294 wana maana gani... Hakuna takwimu zozote duniani zinazoweza kuonyesha Kiingereza au Kifaransa kina Wazungumzaji wangapi! sembuse kiswahili!..utaanzia wapi kwanza ikiwa hata population ya wasukuma wenyewe ipo ktk makisio!
  Tumekosa kazi, badala ya kutafuta mbimu za kuondoa Ujinga na Umaskini tunaaza na tafiti za kina Alibaba na Alinacha!
   
 3. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280

  du hii nayo kali.
  Ukichukuwa jumla ya wanafunzi wa shule ya msingi wanao hitimu darasa la saba tu idadi yake ni sawa ama zaidi ya hiyo na bado naamini wanafunzi hawa 99.9999999999999999999999999999999999999999% wanaongea kiswaz.

  sasa huyu aliyofanya hii research du labda alikuwa UHOLANZI
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  kisukuma kiwe lugha ya taifa!
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  I second your statement.

  Of all the tribes in Tz, Sukuma ndio kabila kubwa so to say and obviously kisukuma ndio kina wazungumzaji wengi.

  Lakini majority ya wasukuma hawa wanazungumza Kiswahili pia, kama ilivyo kwa other tribes. Hivyo ni rahisi kusema kuwa Kiswahili kina wazungumzaji wengi kuliko lugha za makabila.
   
 6. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Halafu eti hawa watafiti bogus ndiyo inapangwa watengewe 1% ya bugdet (Tsh 40 Bill) ....
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Bull Shyt
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh huu ni uongo mchana kweupeee.
  Utafiti huu ni wa kizushi.
  kiswahili ni lugha inayozungumzwa na karibu kila mtanzana.Population ya watu wa Dar es salaam pekee ni zaidi ya watu milioni 4 ambao ni wazungumzaji wazuri wa kiswahili bado hatujaenda katika miji mingine mikubwa kama Arusha,Mwanza,Mbeya,Iringa,Tanga,Morogoro,Kilimanjaro,Kagera na Dodoma mtafiti anataka kutundanganya watu wanaozungumza kiswahili Tanzania ni watu 2,379,294.Sijui hizi data zimetoka wapi au ndiyo zile tafiti ambazo watafiti wanakaa maofisi bila kwenda kwenye field.Kwa hakika watafiti wameshindwa kuelewa kwamba wazungumzaji wakisukuma karibu wote pia ni wazungumzaji wa kiswahili.Prof Josephat Rugemalira nadhani amepitiwa kidogo tumsamee.
   
 9. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mimi nina 99.9% ya uhakika kwamba tatizo ni mwandishi kilaza wa Mwanachi.

  Kama hii ni ripoti ya "matokeo ya utafiti wa miaka kadhaa," hakika humo ndani wameainisha ni nani "muongeaji," na ili uhesabiwe "muongeaji" inabidi uwe anajua hiyo lugha kiasi gani, na wamepima kwa njia zipi za utafiti.

  Inawezekana kabisa kabisa kwamba ripoti ya utafiti imemaanisha "muongeaji" ni muongeaji mzawa , kwa maneno mengine, muongea Kiswahili unatakiwa lugha ya Mama yako iwe Kiswahili, lugha ya kwanza kabisa ambayo uliongea wakati unaomba maziwa.

  Yani huu mradi inawezekana ulikuwa unatafiti ni lugha gani ina waongeaji wazawa wengi kupita wote Tanzania. Ikaonekana ni Kisukuma.

  Tusubiri labda kuna mwandishi mwingine atasoma hiyo ripoti vizuri atuwekee kilichosemwa humo. Sitegemei.
   
  Last edited: Feb 22, 2009
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kuhani,
  Mkuu utafiti wa namna hii hauwezekani kabisa hata iwe ni lugha mama..kwani sio kila Msukuma anazungumza kisukuma, wapo wengi sana hawajui na nawafahamu.. ukubwa wa kabila haina maana wote wanazungumza kisukuma, pia wapo watu wewngi wasiko kuwa wasukuma kwa kabila lakini lugha yao ya kwanza ani kisukuma vile vile!..
  Utafiti wa namna hii ni ujinga mtupu kwani utaanzia wapi? sii lazima uongee nao kujua kama wanazungumza kisukuma kisha hao wenyewe wasukuma kwa kabila wamezagaa nchi nzima..
   
 11. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kuhani hata mimi nakubaliana na wewe kuwa inawezekana mwandishi ndiye kilaza,, hakujua namna ya kuripoti na implication ya reporting yake!

  kama watu waliofanya huo utafiti wako hapa watuwekee andiko zima tujue mbivu na mbichi, lakini ukweli mwingine ni bayana mno jamani! mweh
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Kimakonde kiwe lugha ya Taifa, kigogo, kimwela, kinyakyusa.......
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Si kweli kwamba Kisukuma ndio lugha yenye waongeaji wazawa wengi nchini. Ingawa hawajaweka assumption za utafiti wao na njia walizotumia kuwaainisha hao wazungumzaji wa lugha mbalimbali, bado matokeo ya utafiti huu hayana ukweli na hayalingani na hali halisi.

  Ukichukulia kwamba mtafiti alilenga wazungumzaji wazawa. Haiwezekani kabisa kuwa katika Tanzania watu milioni 2 na ushee wakawa ndio wazungumzaji wazawa wa kiswahili. Maeneo ya mijini tu ya baadhi miji ya Tanzania kwa ujumla (Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Unguja, Pemba, Arusha, Moshi, Dodoma, Iringa, Mbeya, Kigoma, Mwanza), unapata wazungumzaji wazawa wa Kiswahili ambao ukiwajumlisha wanazidi milioni 10, ambayo ni zaidi ya wazungumzaji kiswahili waliotajwa na ripoti kuwa milioni 2.

  Hata hivyo idadi ya Wasukuma Tanzania iko kati ya milioni 3 -4. Sasa hii idadi ya milioni 5 ya wazungumzaji Kisukuma inatoka wapi?
   
  Last edited: Feb 22, 2009
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkandara,

  Hatuongelei Msukuma ni nani, anaongea lugha gani, na "ukubwa wa kabila" na lile na hili. Msukuma asiyeongea Kisukuma huyo hatuhusu hapa, mtoe, utajichanganya.

  Ninachosema mimi ni kitu kidogo, rahisi mno: kwamba utafiti huu inawezekana ulikuwa utatafuta muongeaji mzawa wa lugha fulani. Hivyo tu.

  Kwamba mzawa wa Kiswahili ni yule ambae lugha aliyosemeshwa na Mama yake wakati anaitwa kunyweshwa maziwa ni Kiswahili. Bila kujali huyu Mama yeye lugha yake ni nini. Ni hivyo tu. Hivyo tu.

  Ikaonekana kwamba Kisukuma ndio zaidi.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kuhani,
  Mkuu nakubaliana na wewe ktk hoja lakini ni kitu ambacho hakiwezekani...utaweza vipi kutambua lugha ya mtu aliyosemeshwa akinyeshwa maziwa!.. mkuu hata mimi sielewi ni lugha gani kati ya Kiswahili na Kikerewe nilisemeshwa wakati huo..na ukija kwangu nitajibu lolote litakalo nipendeza iwe ni kukutoa baada ya kuona una wazimu au nitazua moja..ndugu wawili wanaweza kuwa tofauti, mmoja fluent kwa kiswahili na mwingine kikerewe na sote tusijue ni lugha gani tuliyonyonyeshwa nayo!..kibaya zaidi limetumika neno Atlas!..meaning eneo limetumika na sio population au uzawa ndilo limetoa conclusion wakifanya mahesabu ya Alinacha!
  Mkuu ebu nambie wewe unafikiria wamefanya utafiti vipi kufikia hesabu ya millioni 2.. maanake hata sielewi..wameenda kila nyumba au?
   
 16. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hili ni bonge moja la assumption ambalo hujui kama ni kweli!

  Ni hivi, Mama.

  Ukichukua waongea Kiswahili wote wazawa kutoka Tanzania, Burundi, Kenya, Mozambique, Somali, Uganda, the Congo, Rwanda, Comoro, woooote hao, waongeaji wazawa ni milioni 5 mpaka 10! (
  "Swahili", Encyclopedia of Language and Linguistics, 2nd ed., 2006, Elsevier; Lutz Marten )

  Sasa hao millioni kumi wa Mbea na Kigoma na Iringa na Moshi umeitoa wapi hao kama Afrika nzima wazawa wa Kiswahili hawazidi milioni 10? Umetoa wapi hiyo milioni kumi Mama?

  Ndio maana hawa watafiti wetu wakasema kwamba waongeaji Kiswahili Tanzania ni milioni mbili tu!

  Naomba kusisitiza: Maana ya "muongeaji" wa Kiswahili katika hii ripoti inawezekana ni yule tu ambae lugha ya kwanza kabisa kusemeshwa na Mama yake ni Kiswahili.
   
  Last edited: Feb 22, 2009
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Feb 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Bing'we...mbona mna hate hivyo mother tongue yetu na ng'wanangwa Masanilo na Kalunde na Kabula wake...Sukuma ndio kabila kubwa Tanzania na ndio lenye wazungumzaji wengi. Kama kuna kabila ambalo linaitwa "Waswahili" then hapo ndio ningeelewa....Basukuma oyeeeeee...Basukuma massive stand up
   
 18. M

  Mama JF-Expert Member

  #18
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Asante sana Kuhani kwa rejea hiyo. Hapo hawajaongelea wazawa kama ambavyo wewe unaaza. Hivyo let it out of the window.

  Hata hivyo zaidi ya asilimia 60 ya hao waongea Kiswahili barani Afrika wako Tz. Hivyo, basi ukweli unabaki kuwa zaidi ya Watanzania milioni 5 wanaongea Kiswahili.

  Kwa mfano, kwa hesabu za haraka haraka ukichukua watu milioni 2 wanaotoka Unguja, Pemba na Dar es Salaam, wawe ni waongeaji wazawa na Kiswahili. Ukiongeza Tanga, Morogoro, Lindi, Mtwara, Arusha na Mwanza, unapata wazungumzaji Kiswahili wazawa wanaozidi milioni 3 na ushee. Hivyo basi watu wanaoongea Kiswahili Tanzania wanazidi milioni 3.


  Okay, okay, hebu tuangalie wazungumzaji wazawa wa Kisukuma ili tuweze kuhusisha na hiyo idadi ya waongea Kiswahili nchini.

  Tanzania kuna Wasukuma kati ya milioni 3-4, iweje leo mtafiti au hata kama ni mwandishi atueleze kuwa wanaoongea Kisukuma ni milioni 5? Wamepika taarifa, au takwimu zao ni za uongo. Kifupi ni kwamba wameudanganya umma kwa kusema kuwa kuna idadi waongea Kisukuma ni kubwa kuliko idadi halisi ya Wasukuma wenyewe! Au kuna Wasukuma hewa?
   
  Last edited: Feb 22, 2009
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Feb 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hakuna population growth Usukumani? Na hiyo idadi ya kati ya milioni 3-4 takwimu za lini? Na ziko static wakati wote...haziongezeki wala kupungua? Na kutoka milioni 3-4 kwenda 5 sio leap kubwa hivyo with the passage of time....Kwa hiyo uwezekano wa Basukuma kuwa milioni 5 si kitu hewa....it's a real possibility

  Basukuma massive stand up....
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Mkuu bado nashindwa kabisa kujuwa kama makosa ni ya mwandishi ama ni ya utafiti wenyewe...Maoni yangu binafsi nafikiri ni BOTH....Kwasababu heading inasema kisukuma kina wazungumzaji wengi zaidi ya kiswahili na utafiti wenyewe wametoa namba ambazo zinaelekea kuwa si kweli kwani idadi ya wasukuma haifikii idadi ya wazungumzaji wa kisukuma. Hata hivyo bado wametaja lugha ya kikuyu kuwa imo hatarini kufa kwasababu ya kumezwa na lugha kuu...Sasa lugha kuu ni kisukuma ama kiswahili?(hawakutaja)
  Haingii akilini kuwa wazungumzaji wa kisukuma ni wengi zaidi ya wazungumzaji wa kiswahili na wakati kwenye kila kabila kuna wazungumzaji wa kiswahili.
  Hata wasukuma wenyewe uki minus wale wenye kuzungumza kiswahili halafu hao wenye kuzungumza kiswahili ukawajumlisha na wengine wenye kuzungumza kiswahili kutoka makabila mengine basi logically namba ya wenye kuzungumza kiswahili itakuwa kubwa zaidi...Sasa utafiti huo unasema hapa nchini, haukumention EA,na wakati huo huo wametaja lugha ya kikuyu kwenye utafiti wao huo.

  Bado sijaelewa labda nisubiri wachangiaji wengine ama mawazo ya tofauti...Other than that ni ngumu ku elewa makosa yako upande upi hadi usawa huu.
   
Loading...