Eti kati ya wanaume na wanawake akina nani wanateseka zaidi?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti kati ya wanaume na wanawake akina nani wanateseka zaidi??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Kichwani, Jan 31, 2010.

 1. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ................
  Yule mama: wanafundisha hivyo kwa sababu ndivyo ilivyo…….tena wanaume mna nafuu, mnateseka kipindi kifupi tu wakati wa kutafuta, lakini mkipata mnarelax kufurahia mapenzi……… lakni wanawake wakishakmkubali mwanaume, inageka zamu yao ya kuteseka, yaani wanateseka hadi kifo ndio kinawaokoa………. Hivyo utaona wanawake wanateseka muda mrefu zaidi!
  ..............

  haya endelea kisha toa maoni yako, ukitaka kuenjoy zaidi anzia chini kabisa kuja juu............, J2 njema

  Haya mazungumzo nilifanya na mama mmoja mtu mzima mwaka 2002 nilipoanza tu kazi baada ya kumaliza chuo, enjoy and finally discuss openly;

  Yule mama: hongera mwanang kwa kupata kazi nzuri, sasa bila kupoteza muda anza kujiandaa kimaisha na ni vizuri ukaanza kuafuta na mchmba, uoe utulie

  Mimi: Asante mama, lakini hayo ya kutafuta wachumba kwa sasa nataka nipumzike kwanza

  Yule mama: hapana mwanangu, ujana una vishawishi vingi, fikiria kuoa mapema utulie, usiwe kama vijana wenzako

  Mimi: hata mimi napenda kuoa lakini wasichana wanawatesa sana wavulana hasa wasio na pesa, ndio maana sitaki kuteseka tena kwa sasa. Bado namkumbuka yule msambaa…, yule mchaga, yule mkurya, yule mhaya, yule mhehe…… aaah mama, walinitesa sana na baadaye wakanikataa, wakachagua wengine. nataka nitulie angalau kwa miaka mitano kwanza labda nitawaamini tena wasichana

  Yule mama: hahaha……. usinichekeshe, hakuna mateso pale ndiyo maisha yenyewe mwanangu, unapaswa kuvumilia hadi umpate wako halafu hutateseka tena hadi kifo kinawatenganishe, believe me my son …………………

  Mimi: siku zote tunaambiwa hivo, hata kanisani mchungaji anatufundisha hivyo………

  Yule mama: wanafundisha hivyo kwa sababu ndivyo ilivyo…….tena wanaume mna nafuu, mnateseka kipindi kifupi tu wakati wa kutafuta, lakini mkipata mnarelax kufurahia mapenzi……… lakni wanawake wakishakmkubali mwanaume, inageka zamu yao ya kuteseka, yaani wanateseka hadi kifo ndio kinawaokoa………. Hivyo utaona wanawake wanateseka muda mrefu zaidi!

  Mimi: siamini mama, mbona tunaona wanawake wakifurahia sana maisha baada ya kupata wapenzi, wanaendesa magari amzuri ya waume zao, wanasaidiwa matatizo yao yote, wanaongezewa heshima hata kama mlikua rika moja anpata heshima kubwa kukuzidi………mbona sioni mateso pale?

  Yule mama: hahahah……. yapo mwanangu, tena makubwa tu…… na wengi huwa hawapati uisingizi… wanalia na kuomba usiku kucha, ……….wengi wana hofu siku zote za maisha yao…. Wengine wanalazimishwa kusamehe hata kwa makosa ya wazi ya waume zao….. wengine wanaachiwa kulea watoto peke yao mume anahangaika na wanawake wengine ……………. Mwanagu ukioa tafadhari usimtese mkeo hivyo………..Mungu alipanga ndoa ziwe mahali pazuri pa wote kufurahia

  Mimi: sawa mama, nashukuru sana, nakuahidi nikioa sitafanya hayo wanyofanya wanaume wengine…... usiache kuniombea kwa Mungu…………. Samahani, hivi na wewe baba anakutesa?

  Yule mama: hahahah………..mwanag umenikumbusha mbali sana…….siku hizi amepunguza, lakini tulipokuwa vijana alinitesa sana.

  Mimi: au ulikuwa na wivu sana na siku hizi umepunguza?...... nasikia umri ukiwa mkubwa wivu unapungua! Ni kweli?

  Yule mama: heheheeee, hilo swali nitakujibu siku nitakapowakaribisha nyumbani kwangu wewe na mchumba wako, na siku hiyo atakuwepo pia mume wangu naye anisaidie kujibu swali hili………………….
  Bottom-line
  This thread is dedicated to my love hapa JF: anajijua
  My take kwa mpenzi wangu
  tafadhari nijibu mapema tupange safari ya kumtembelea huyu mama, Mungu kawajaalia yeye na mumewe maisha marefu kwa ajili ya kutuombea sisi, wanatusubiri tangu mwaka 2002…… please my dear, mi ni kijana nitavumilia mateso ya kusubiri, naomba basi mhurumie hata huyu mama, yeye ni mzee na bado anavumilia, anavumilia mateso yake na mumewe na haya ya kutusubiri sisi watujibu swali lile!! tumpunguzie basi mama yetu japo haya mateso ya kutusubiri!!!!!!!!!
  My take kwa wana JF
  Tafadhari tujadili hili suala la mateso, ni kweli yapo mengi na ya muda mrefu zaidi kwa mwanamke kuliko mwanume?

  Magwiji wa mapenzi tupeni experience zenu …………..
   
 2. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  mmmhhhh

  mazungumzo ya kusisimua sana.

  bora umtaje huyo mpenzi wako kuna watu watakusaidia kumbembeleza mkajitambulishe kwenu,

  all the best
   
 3. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nzuri ila bandika bandua.
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  mkuu upo???

  nashukuru kwa maoni, lakini naomba tusaidie ufafanue kidogo hapo, nzuri kwa vipi na bandika bandua kwa vipi??

  thanks
   
 5. 2my

  2my JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 30, 2010
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anajijua huyo mupenzi cdhani km anahitaji kubembelezwa tena!!

  haya nendeni mkapewe somo!
   
 6. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  asante mkuu, we tupe tu ushauri wako, huko aliko atasoma na ataheshimu mawazo yako mheshimiwa.

  vipi, uliaga hapa kuwa unaenda jimboni, kampeni inaendeleaje? umesikia jinamizi la CCJ, we uko upande gani?

  all the best
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,930
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Dah kumbe jamvi lina utamu wake watu wanapata na wachumba humuhumu
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,946
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Ndiyo maana yake mkuu, mimi bado nipo mawindoni hapa ingawa kimya kimya.. Hehe!
   
 9. M

  Mende dume Member

  #9
  Feb 1, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama wanawake ndo wanateseka zaidi kuliko wanaume, why in the hell do men die earlier?

  it is mateso that kills thems! yes i have said it
   
 10. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ule ni mtazamo wa yule mama. we umekuja kivingine kabisa, can you explain briefly?

  unasema in the hell wanaume wanakufa mapema zaidi, can you prove it with reference? any source 4 this please?
   
 11. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,506
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145

  Kila mmoja anateseka kulingana na jinsi mlivyogawana mapenzi yenu. Ili wote mfurahie mapenzi, lazima iwepo kitu kinachoitwa "DOUBLE COINCIDENCE OF LOVE" yaani kila mmoja awe anampenda mwenzake sawasawa na jinsi naye anavyopendwa, vinginevyo mmoja atateseka na mapenzi hayo. Mara nyingi aliyependa zaidi ndiye anayeteseka, kwa kuwa mwenzake hatojali shida zake kwa wakati na kwa kiwango sahihi, lakini pia yeye anaweza kujikuta akisamehe makosa hata yaliyowazi kabisa, tena bila masharti wala kiwango. Hujikuta akikubaliana na mienendo ya mwenzake hata yale yasio na maslahi kwake yeye, au hata yenye kumdhalilisha na kumkandamiza yeye, na kuhatarisha maisha yake.

  Hivyo, cha msingi ni kwamba; OGOPA KUPENDA BILA KUPENDWA!
   
 12. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  mzee umedadavua vyema kabisa na umesomeka. thanks very much.

  hapo penye bold ndipo pagumu zaidi na panapouma zaidi japo ndilo tunalopaswa kufanya, lakini ngumu sana practically
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Konakali,

  Umemaliza kila kitu. Hakuna kipimio cha kuteseka au kutoteseka. Ni suala la nini kinaendelea katika kila uhusiano (independently of others). Hii iliyopo hapa inaweza kuonekana kuwa kweli endapo itachukuliwa kwa mtazamo wa ndoa za huko nyuma au baadhi ya maeneo ambapo mume ndiye chanzo cha maisha (may be na uhai) katika ndoa. Mwanamke anakuwa mtu wa kupokea tu na siyo mchangiaji wa kuendesha familia. Katika mazingira hayo, mwanamke atakuwa anateseka tu. Kwa hali ya sasa hivi ambapo tunaelekea kwenye 50% kwa 50% (hasa hasa mijini) hii kitu itazidi kuwa historia. Tutaendelea pia kupata hadithi za mateso ya upande wa pili (i.e wanaume wanaoonja joto la jiwe kama inavyoendelea katika nchi kama Denmark).
   
 14. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  mzee si denmark tu, mbona hata hapa tz ya leo tayari watu wnaonja joto ya jiwe kama kawaida????????///

  nafikiri ishu muhimu uliyogusia n relative position kati ya wanandoa na kiwango cha mapenzi baina yao. ikiwepo imbalance kidogo, upande mmoja unalizwa na mwingine unaingia katika mtego wa unfair relation kama sio adultery kwa kwenda mbele

  tutafika tu............
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...