Kama umeoa au umeolewa kuna ulazima wowote

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Kuna ulazima wa mke au mwanaume kumtaarifu mume au mke wake anapotaka kuwatumia pesa wazazi wake?
 
Hakuna, ila kutokana na ugumu wa maisha na kuwa na rasilimali chache za fedha ndani ya nyumba;inabidi kutaarifiana utumapo fedha,ili mkija kufirisika mjue mlishirikishana katika matumizi ya fedha.
 
Hakuna, ila kutokana na ugumu wa maisha na kuwa na rasilimali chache za fedha ndani ya nyumba;inabidi kutaarifiana utumapo fedha,ili mkija kufirisika mjue mlishirikishana katika matumizi ya fedha.
Kweli kabisa! Mambo ni mengi,yanaenda kwa kasi,ila muda ni mchache.
 
Hakuna, ila kutokana na ugumu wa maisha na kuwa na rasilimali chache za fedha ndani ya nyumba;inabidi kutaarifiana utumapo fedha,ili mkija kufirisika mjue mlishirikishana katika matumizi ya fedha.
Kama unaona kuna ulazima kujiambia wewe mwenyewe, basi ni lazima. Ila ukiona siyo basi hata na wewe usijiambie. Nini maana ya ndoa basi?
 
Usipofanya hivyo hawa wenzetu Akili zao wanazijua wenyewe,Utashangaa wife Ana Gorofa kwao wewe huku ndio unamalizia msingi...Siwaamini hata kidogo kutokana na uzoefu wangu.
 
Hii mara nyingi inalalia sana upande mmoja. Wanawake mara nyingi ulazimisha kujua waume zao wanatumiaje fedha zao ikiwa ni pamoja na wanatuma kiasi gani kwa wazazi wao au wanatoa msaada gani kwa ndugu zao. Lakini wao wakituma upande wao wala hawaoni umuhimu sana wa kumjulisha mme hivyo ufanya hivyo kwa siri. Slogan ni ile ile ya kuwa fedha za mwanamme ni za mwanamke na za mwanamke ni za kwake binafsi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom