Eti idadi ya vishangazi kwenye ngozi ndo idadi ya watoto utakao zaa?

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Habari yenu w.akuu,

Kuna Watu nasikia wanasema eti vile vishangazi kwenye ngozi(vialama fulani rangi nyeusi wengine wanaita watoto) ndo idadi ya watoto utakao zaa?

Eti mtu ambaye hazai hawezi kuwa na alama hizo. Hizi stori nazisikia kitambo, je kuna ukweli wowote? Je ushawahi sikia hizi mambo?

Kuna alama nyeusi zipo kama dot hivi kwenye mwili, inaweza kuwa mkononi , mgongoni, kwenye paja. Nimeona kwenye picha ya beyonce anayo shangazia karibu na jicho, pembeni kidogo na wanja ulipoishia na nyingine anayo kifuani karibu na mkono.
Hii imekaaje?

BeyoncéKnowlesAAFeb09.jpg
 
Mimi kwa experience yangu naweza kuvihusianisha hivyo vishangazi na fertility......ila ni kwa case study moja ambayo ni mimi...naweza kuwa wrong....
 
Kama ingekuwa kweli kuna watu wangekuwa na kijiji maana siku hizi naona haka kamekuwa kama ni kaugonjwa fulan unakuta mtu uso mzima vimemjaa na hata kuna Mbunge mmoja(Mzito Kabwela) hadi vimemwaribu sura...Sasa ikija kuwa ndiyo idadi ya watoto wake ajiandae kujenga shule yake mwenyewe..
 
Habari yenu w.akuu,

Kuna Watu nasikia wanasema eti vile vishangazi kwenye ngozi(vialama fulani rangi nyeusi wengine wanaita watoto) ndo idadi ya watoto utakao zaa?

Eti mtu ambaye hazai hawezi kuwa na alama hizo. Hizi stori nazisikia kitambo, je kuna ukweli wowote? Je ushawahi sikia hizi mambo?

Kuna alama nyeusi zipo kama dot hivi kwenye mwili, inaweza kuwa mkononi , mgongoni, kwenye paja. Nimeona kwenye picha ya beyonce anayo shangazia karibu na jicho, pembeni kidogo na wanja ulipoishia na nyingine anayo kifuani karibu na mkono.
Hii imekaaje?

View attachment 345972
Kwa hiyo mtu akiwa na "vimjomba" inakuaje? Fanya utafiti kisha utuletee mrejesho.
 
Jamaa yangu mmoja aliniambia Ukiona mtu ana kishangazi kwenye lip ya juu basi naturally ni mpenda ngono.. Halafu kama unavyo kifuani jua una nguvu tele
 
Imani za kale, zilikuwa na maana yake! Kwetu tuliamini ni alama ya kuzaliwa na kila mtu lazima awe nayo!

Baada ya kwenda shule kidogo, nikagundua ni seli flani hivi zinajitengeneza, na zikiwa nyingi kwenye mwili wa mwadamu ni hatari sana kwa afya yake!
 
mim ntakua na machester united mbili kama hvyo vina potray idadi ya watoto
 
Back
Top Bottom