Eti, “Huyo sio wa kuoa, ni wa kuchezea tu!”

Tegelezeni

JF-Expert Member
Dec 31, 2009
268
124
Bila shaka wewe msomaji unayesoma hapa utakubaliana na mimi kuwa umeshawahi kuzisikia kauli hizi kutoka kwa wanaume pale anapozungumziwa mwanamke mzuri kwa sura na umbo.

Kwa kawaida vipimo vya uzuri wa mwanamke kwa wanaume vimegawanyika. Wanaume wengi hupima uzuri wa mwanamke kwa sura au umbo, lakini linapokuja swala la kuoa, suala la tabia na mwenendo hupewa nafasi kubwa.

Na ndio maana wakati mwingine unaweza kushangaa kukuta mwanaume ambaye ni hodari wa kuchagua wanawake wazuri, lakini ukija kumuona mke aliyemuoa, utakuta ni mbaya kwa sura na umbo, lakini kwa upande mwingine utakuta mke huyo ni mzuri katika maeneo mengine kama vile, tabia nzuri,upendo, wema, na anayemudu malezi ya watoto katika familia.

Sifa nyingine ni zile za kumkubali mwingine kirahisi, kuwa tayari kusaidia yanapojitokeza matatizo katika familia, mpenda amani na kumfanya mume wake aone kuwa hakukosea kumchagua yeye kuwa mke wake. Kwa kifupi wanawake wa aina hii hata kama wangekuwa ni wabaya kwa sura na umbo bado wako kwenye nafasi ya kuonekana kuwa ni wazuri, na huolewa kirahisi zaidi.

Wanawake wazuri kwa sura na umbo ambao tabia na mienendo yao hairidhishi wako kwenye nafasi kubwa ya kuishi bila kuolewa, na kwa bahati mbaya zaidi wanawake wengi wanaohesabika kuwa ni wazuri, tabia na mienendo yao ni ya kutilia mashaka. Wanaume wengi huvutiwa na wanawake hao kujenga uhusiano nao hasa wa kimwili tu na si vinginevyo, na ndio maana wanawake wazuri kwa sura na umbo wanalo soko kubwa sana kwa wanaume, lakini huishia kuchezewa zaidi kuliko kuolewa.

Wanaume nao kwa upande wao wamejenga dhana kwamba wanawake wazuri sana sio wa kuoa na hivyo kuwaogopa. Wanaamini kwamba wanawake wazuri sana ni wasumbufu, kitu ambacho kina ukweli kwa kiasi fulani. Wanaume wanaamini kwamba wanawake wazuri sana kwa sura na umbo huwasababishia waume zao maradhi ya moyo,shinikizo la damu na wakati mwingine hata kuwafanya kupata matatizo fulani ya kiakili, na hiyo inatokana na waume hao kuwa katika mashaka ya wake zao kuchukuliwa na wanaume wengine wakati wowote kutokana na uzuri wao. Hata hivyo wanawake wazuri nao huwaendesha waume zao wakijua kuwa ni wazuri na soko lao liko juu na waume zao nao huwanyenyekea wakihofia kuachwa.

Na ndio maana usishangae kuona kuwa wale wanawake ambao watu wamekuwa wakiamini kuwa ndio wabaya kwa sura au umbo lakini tabia na mienendo yao ni mizuri ndio wanaoolewa na hata ndoa zao zinadumu, tofauti na za wale wanaoonekana kuwa ni wazuri sana kwa sura na umbo na ambao tabia na mienendo yao si mizuri, ndoa zao hazina umri mrefu.

Kwa kukanusha
Unasema hakuna mwanamke
Mzuri wa umbo, sura na tabia...

Lazima kuwe na makundi mawili
au matatu.

Au nimekosea m..

Kwa kukanusha

Unasema hakuna mwanamke

Mzuri wa umbo, sura na tabia...

Lazima kuwe na makundi mawili

au matatu.

Au nimekosea m..

hujakosea AD, hawa wako makundi matatu, wazuri, wazuri wa kati, alaf wale...sitapenda kumalizia.
Wazuri wa kati ndio kundi kubwa la wanawake wanaolewa kwa haraka, na hata wanaume wengi wanaoa wanaonekana kuwa na furaha ndani ya ndoa zao kuliko hao 'wazuri'

na wanaume je!!

wanawake utasikia huyu ni wa kuchuna yule ni wa kunioa, na ndo maana mademu hata kwenye suala la mawasiliano utakuta kuna wengine anawabeep tu na kuwaomba salio lakini mwingine atapigiwa aongee anavyotaka na salio akitaka ataongezewa!

FB (sorry sio face book lakini) umeongea la maana hapo
angetupa na other side of the story

hujakosea AD, hawa wako makundi matatu, wazuri, wazuri wa kati, alaf wale...sitapenda kumalizia.

Wazuri wa kati ndio kundi kubwa la wanawake wanaolewa kwa haraka, na hata wanaume wengi wanaoa wanaonekana kuwa na furaha ndani ya ndoa zao kuliko hao 'wazuri'

Na huu utafiti umefanywa kwa wanaume
wangapi na wa wapi???

Labda kuna ukweli. Kuna mmoja namjua mzuri sana sura na umbo (na tabia kidoogo) anakimbilia 40 hajaolewa na anasema kabisa hajapata wa kumuoa. Na naona sasa amekata na tamaa ameamua kubanana kwa waume za watu tu.

Tegelezeni na mchambuzi ni mtu mmoja?????????

No, sio mtu mmoja, bali mimi na Mtambuzi ambaye kiukweli tunafahamiana tulihudhuria shule moja inayohusiana na maswala ua Utambuzi.
Je kuna tatizo lolote kuandika Mada zinazoshabihiana hapa JF?

Uzuri wa mwanamke siyo ellimu, ni TABIA. sasa kama una tabia za kimbweha ujue imekula kwako hata kama ni mzuri na umeliza vyuo vyote

Labda kuna ukweli. Kuna mmoja namjua mzuri sana sura na umbo (na tabia kidoogo) anakimbilia 40 hajaolewa na anasema kabisa hajapata wa kumuoa. Na naona sasa amekata na tamaa ameamua kubanana kwa waume za watu tu.

nyumba kubwa - nyaruju!

natumaini huyo dada anayekimbilia 40 hajabanana na muzee?

Niko makini. Nakaba mpaka penati

Nakuaminia!

Back to the topic:

Wale wanaitwa ni "wa kuchezea" wanatengenezwa na jamii - na - hasa hasa wanaume!

Wanaume wengi huwa tunasahau kuwa - it is not always true that:- What You See Is What You Get!!!

Kuna dada mmoja alikuwa amepanga nyumba moja na mama_enock mitaa ya "Kijitonyama", kila siku niliyokuwa naenda kumtembelea mama_enock (wakati wa uchumba), nilikuwa nakuta yule dada yupo na mwanaume tofauti!!! Hadi nafunga ndoa na mama_enock (baada ya kuchumbiana for 6 years), sikuwahi kumuona "boy friend" wa yule dada!... Mpaka leo hajaolewa (20 years later)!!!!

Umeona eeh. Yani dada akiwa mzuri saana anahitaji nguvu za ziada ku prove jamii wrong maana jamii ina mentality ya kuwa hawa ni wa kutumia zaidi si wa kuoa. Wale wanaojitahidi ku kubehave kama vile kuwa expensive bila kuwa na kiburi na dharau wamefanikiwa kukwepa dhana hii potofu. Their behavior is socially constructed. Watu wanawasema vibaya na wao wanakubali kuwa wako hivyo. Wenye watoto wa kike kazi kwenu.

Namshukuru babangu hakunilea kama chombo cha kutumiwa na wanaume au kutumia wanaume ku make it in life. Solution kama una mtoto mzuri anza mapema kumjenga kuwa strong na kutobehave legelege atatumiwa kama toy

Nakuaminia!

Back to the topic:

Wale wanaitwa ni "wa kuchezea" wanatengenezwa na jamii - na - hasa hasa wanaume!

Wanaume wengi huwa tunasahau kuwa - it is not always true that:- What You See Is What You Get!!!

Kuna dada mmoja alikuwa amepanga nyumba moja na mama_enock mitaa ya "Kijitonyama", kila siku niliyokuwa naenda kumtembelea mama_enock (wakati wa uchumba), nilikuwa nakuta yule dada yupo na mwanaume tofauti!!! Hadi nafunga ndoa na mama_enock (baada ya kuchumbiana for 6 years), sikuwahi kumuona "boy friend" wa yule dada!... Mpaka leo hajaolewa (20 years later)!!!!

Afu shida ya wadada wazuri sasa nimeshaona hata kwenye colleges wanaume wanapanga foleni kwa SIRI. Hamna anayekuwa tayari ku declare interest openely kwa hofu ya kuchekwa. Inasikitisha. Tulikuwa tunasoma na mdada si mchezo. Lakini watu kibao wamepitia mpaka kuna siku alibakwa na several boys baada ya kuleweshwa lakini yuo can't imagine hakuwa na boyfriend. Alikuwa na wa one night stand tu. Utasikia fulani nae kapita pale, fulani nae kapita pale. Hakuna anayetaka kuweka makazi ya kudumu.

Back
Top Bottom