Eti hawa ndio tegemeo(Majembe) wa Ccm ktk Siasa za MAJI TAKA!!

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Tokea kuisha kwa uchaguzi mkuu wa 2010 na Chama cha Mapinduzi kikiwa ndicho kilichopata ridhaa ya Watanzania kuunda serikali kwa miaka mitano,huku Chama Kikuu cha Upinzani CHADEMA kikipata nafasi ya kuunda Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni,kumekua na Vuta nikuvute Ndani na nje ya bunge kati ya aidha Viongozi waandamizi wa vyama husika au Wabunge wake!

Tangia kuanzishwa kwa Mfumo wa vyama vingi hapa Tz 1992 Kumekuepo na Ushindani au Upinzani kati ya vyama vya upinzani [NCCR-Mageuzi 1995-2000.... TLP 2000-2005..... CUF 2005-2010] na CCM kuanzia 1995-2010. lakini kuanzia uchaguzi mkuu 2010 Upinzani mkubwa na ambao unatishia Uhai wa Chama hiki Kikongwe CCM,ni kutoka kwa CHADEMA.

CDM ndicho chama pekee kinachoonekana kuwa ni hatari kwa utawala wa CCM kwani kina nia ya dhati ya kumkomboa mtanzania kwenye Umasikini wa Mali na Fikra baada ya Kulagaiwa na Ccm kwa zaidi ya miaka 50 huku baadhi ya Watanzania maisha yao yakiwa sawa na mtu anaeishi PEPONI,huku wengine maisha yakiwa ya shida kama JEHANAMU.

Kwa sababu ya Ccm na Watawala kupeana Madaraka kifamilia na Kiundugu,kumekua na wasiwasi kwamba siku CDM watakapo chukua Serikali basi itakua ni hatari kwa watawala na familia zao kwa kuwa iwe isiwe Chini ya serikali ya Rais Dk Slaa,hakutakuepo na Huruma kwa wote walioiba na kujilimbikizia mali ya UMMA!

Kwa sababu hiyo basi baada ya Ccm kuona Watanzania hususan vijana wanaiunga mkono CHADEMA ndipo wakaja na wazo la kuhakikisha kuwa wanawatumia vijana viongozi ndani ya CCM na baadhi ya Wazee WASIOJIHESHIMU kukichafua CDM na kuwapaka baadhi ya viongozi wake Matope kama njia ya Kupunguza kasi!

CCM CHAMA CHA ZAMANI Kilichokosa "DIRA" na MWELEKEO....(kama ambavyo aliwahi kusema Marehemu HORANCE KOLIMBA,katibu mkuu wa zamani wa CCM,kabla ya kukumbwa na Mauti),kimekua kikijitapa kwamba wana watu [MAJEMBE] ambao wanatosha kupambana na Viongozi wa machachari wa CDM,iwe Bungeni au nje ya BUNGE.

Majembe hayo ya CCM ni NAPE NNAUYE..MWIGULU MCHEMBA..,LIVINGSTON LUSINDE...,WILLIAM LUKUVI...,STEVEN WASSIRA...,ANNA MAKINDA..,SILVESTER MABUMBA..,PETER SERUKAMBA..,JUMA NKAMIA..,EMMANUEL NCHIMBI..,JOB NDUGAI na JOHN KOMBA!
Hawa ndio wanaoitwa Majembe ya CCM ktk kuhakikisha kuwa wanawazibiti Cdm bungeni na nje ya Bunge.!
 
Hao wote walitoroka Milembe hospital, utadhibitisha hilo kwa maneno yao. Mi nilimheshimu sana Juma nkamia kabla hajawa mbunge but kumbe ni hovyo kuliko harufu ya mzoga.
 
ahsante mkuu kwa kutuwekea bayana hayo majembe. hakika yanafanya kazi nzuri na chadema wanashindwa kupumua
 
Hao wote walitoroka Milembe hospital, utadhibitisha hilo kwa maneno yao. Mi nilimheshimu sana Juma nkamia kabla hajawa mbunge but kumbe ni hovyo kuliko harufu ya mzoga.

mkuu, waliotoroka mirembe wako chadema. kuanzia na kubwa lao TUNDU LISU. HATA DR HAMISI KIGWANGALA ANALIJUA HILO
 
Ingekuwa mpira ivi sasa ingekuwa dakika ya 88,CCM imeshapigwa bao 4 kwa Mshangao.
 
ahsante mkuu kwa kutuwekea bayana hayo majembe. hakika yanafanya kazi nzuri na chadema wanashindwa kupumua

Mwana ndugu acha kukomaa hapo ktk Screen, Umeshajihakikishia ushindi kwa kuhifadhi ya wadanganyika kadi zao?, Mshiko umetembea wa kutosha? Je umejihakikishia sio Kula kwako Kura CDM?. Mi nakukumbusha sitaki lawama na ugovi wa kutaka kupindia matokeo kesho kutwa. Shauri lako kama husikii.
 
Back
Top Bottom