Eti elimu bure wakati wazazi wanawalipa walimu wa kujitolea mshahara

Oct 30, 2017
78
90
Serikali ya awamu ya tano imekuja na sera ya elimu bure, lakini Hali imekuwa tofauti kabisa.

Katika tarafa ya lupembe Kijiji cha Wanginyi wananchi wanachangia fedha ya kuwalipa walimu wa kujitolea kutokana na uhaba wa waalimu ktk Shule ya Msingi Wanginyi.

Wananchi wanafuatwa na migambo ili waweze kutoa fedha za kuwalipa waalimu wa kujitolea. Hapo dhana ya elimu bure iko wapi?

Naomba Rais Magufuli angalia jambo hili.
 
Hata sisi wilaya ya Morogoro Mjini kuna shule inaitwa KAUZENI, tunachangishwa pesa ili tuwalipe walimu wa kujitolea, na pesa ya walinzi, vyoo - vyote ni mshikemshike, kweli bure ni ghali.
 
Ushambiwa kama unaona elimu garama jaribu ujinga, yani unatoa pesa analipwa mwalimu anayemfundisha mwanao na unaona kabisa mwanao kweli anafundishwa unakuja hapa kupiga kelele kwanza shukuru hata hao walimu wakujitolea wapo wenzako uko wanatafuta hata hao wakujitolea hawawaoni.

Pambana na elimu ya mwanao kama mnaitwa mnashirikishwa kwa mwaka.ukitoa elfu hamsini ajili ya elimu ya mwanao kuna tatizo gani acha siasa ifanye kazi yake wewe pambana na maendeleo ya mwanao.
 
Bure haijawahi kuwa haulipi. Ukitaka kuamini hilo angalia vifurushi vya mtandao ya simu.
 
Wewe kama mwanajamii ulichukuliaje hili swala? Je ni kwa maslahi ya nani? Ukisubiri vitu vya bure ndugu hakika huwezi kupata ubora ndani yake, Ni kweli Elimu ni bure ila ikiwa jamii imekubaliana kuchanga fedha kuboresha elimu zaidi Nafikiri ni swala ambalo hata Magufuli analiunga mkono.

Wale walimu hawako kwenye payroll ya Serikali hivyo ni kama motisha kwao na hata jamii zilizoendelea kielimu hili kwao sio swala gumu.
 
makoga pangatulale,
Enyi ndugu zangu mara mia muendelee kuwachangia hao walimu ili wawafundishie watoto wenu.Mkimuamini huyo anayesema elimu bure itakula kwenu.Nazifahamu shule nyingi za Lupembe sidhani kama Kuna shule ina walimu wa Kutosha.Kadili miaka inavyoenda elimu inazidi kudidimia Lupembe tukimsubiri huyo aliyesema elimu bure tuhesabie tumeumia.Wazazi waliobahatika vihela huko Lupembe wanawakimbizia Private schools sisi tusio na hela tupambane na hali zetu kwa kujichanga
 
Kuna Jambo wanasiasa wanawaficha wananchi hasa wa mikoa ya pembezoni na hii imekuwa Siri kubwa sana! Watoto wenu wananyimwa fursa ya elimu makusudi kabisa kwa lengo la kuwaandaa wapigakura watiifu kwa ccm! Mifano ni Mungu na maendeleo ya elimu hata miundombinu yake inajieleza bayana!

Na msipokuwa na mkakati wa kuusimamia elimu ya watoto wenu basi mtakuwa mnaunga mkono ccm ili iendelee kuwatumia kubaki madarakani! Changieni elimu achaneni na hii dhana inayodumaza elimu!
 
Ndugu yangu wewe inaonekana hujaelewa namaanisha Nini,
Sio kwamba nakataa kuchangia suala la elimu ila is ni kwamba serikali inasema elimu bure sasa hiyo bure inatoka wapi wakati wazazi wanachangishwa fedha kwa ajili ya kuwalipa waalimu?
REJESHO HURU,
 
Mi sikatai kuchangia Ila nataka ufafanuzi wa elimu bure,
Maana yake waende darasani wakakae na kurudi bila kufundisha au inaendana pamoja na waalimu, vifaa vya kufundishia,majengo na miundombonu mingine
Wewe kama mwanajamii ulichukuliaje hili swala? Je ni kwa maslahi ya nani? Ukisubiri vitu vya bure ndugu hakika huwezi kupata ubora ndani yake, Ni kweli Elimu ni bure ila ikiwa jamii imekubaliana kuchanga fedha kuboresha elimu zaidi Nafikiri ni swala ambalo hata Magufuli analiunga mkono.

Wale walimu hawako kwenye payroll ya Serikali hivyo ni kama motisha kwao na hata jamii zilizoendelea kielimu hili kwao sio swala gumu.
 
Yaani wewe ni mtu wa ajabu sana. Kuna tatizo kubwa la walimu wa hesabati na physics sasa kama hamtaki hao walimu wakujitolea watoto wenu watashindwa kusoma masomo hayo hivyo msahau kuwa na Engineer, pilot au daktari hapo kijini kwenu.

Nadhani hata wewe mleta uzi unaupungufu wa elimu. Mimi mwenyewe niko mbioni kujitolea endapo wazazi watanichangia huwa napata uchungu kuona shule za kata zimenizunguka hapa na cha ajabu hawana walimu wa physics wala hesabu na mimi nipo tu japo professional yangu siyo ya uwalimu ila hayo masomo nayamudu sana.
 
Mkuu, hakuna cha Elimu bure hiyo ni geresha tu! Hayo Mambo yameshamiri kila Mahala hapa Nchini, hata Mbeya ni Vivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom