Eti China kusaidia Tanzania Kujenga Viwanda!

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Nasikia eti china itaisadia Tanzania kujenga viwanda ????? Jambo tunalotakiwa kufanya kwa wakati huu kama tunataka kujenga uchumi wetu tusikubali mataifa makubwa eti kutusaidia kujenga uchumi wetu.

uchumi wa dunia ni wa kunyanganyana, biashara ni ileile na waliozishikilia biashara hizo ndio wana uchumi mzuri na ndio matajiri na wazembe wanaosubiri kusaidiwa ndio hubaki masikini. ili masikini aweze kuinuka inabidi na yeye kuingia katika biashara na kuzichukua baadhi ya biashara na hiyo ina maana ya matajiri hao watapoteza baadhi ya biashara. yaani masikini anapanda juu na tajiri anashuka chini.

matajiri hawa ni wajanja sana kwa kuangalia upepo unavyovuma kwa masikini na kutafuta mbinu za kubaki juu.

hawa wameona kile ambacho nchi yetu imekingamua kuwa hatuwezi kuagiza hata vitu vidogo vidogo kwao na wametafuta solution tayari ya kuja kuzalishia huku kwetu na katika misaada hiyo tutajikuta tunabaki kuwategemea kwa kila kitu mpaka nafasi za ajira kwenye viwanda hivi tunagawana.

kama tunataka kuendelea China ni mfano tunaotakiwa kuiga kwa kuwatumia watu wetu kuiga wanayoyafanya kule kwao tuyafanye hapahapa na yale tu tusiyoyaweza sisi ndio tuwaite wageni.

watanzania wengi wanauwezo wa kutengeneza baadhi ya bidhaa za nje kwa kuziiga na tumekuwa tukiziita bidhaa feki bila kutambua hivyo ni vipaji ambavyo tumeshindwa kuendeleza na tunahangaika kuwakamata badala na kuanza kuwasajili ili wazalishe kihalali na kuwapa mbinu za kutotumia majina ya nje kama nembo ya bidhaa zao bali watumie nembo zao na tulinde soko lao.

wachina hawa wamekuwa wakilalamikiwa na marekani kuwa wanaiba technolojia zake na sisi tunatakiwa kuwaiga katika sekita ya uzalishaji.

lazima tutambue kuwa kujenga viwanda wanasema ni mpango wao wa maendeleo wa miaka 5 hivyo tayari wameandaa katika njia ambayo position yao ya sasa na ya kwetu itabaki palepale.

haya si mambo pia ya kwenda kwenye majukwaa na kusema hatuwataki wachina watuzalishie kwani tunahitaji transition period ambayo urali wa biashara utaenda unabadilika taratibu. hivyo tukae chini tuandae mpango ambao tukiutekeleza utabadili urali wa bishara taratibu sisi wenyewe kwa kujua ni kitu gani tuzalishe sisi wenyewe na kwa wakati gani na kile tunachoagiza tuagize kwa kiasi gani.
 
Kama wanataka kujenga viwanda na wajenge tuu sababu hawa wachina wamegeuza nchi yetu wateja wa bidhaa zao kwa jina LA uwekezaji.

Wanaleta vitu vyao ready made from China wanakuja kuuza hapa kwetu eti wawekezaji..kama wanataka kutengeneza viatu ni bora wajenge viwanda hapa kwetu wanunue ngozi kutoka kwa wamasai na wasukuma na waajiri watu wetu..sio watengeneze viatu China waje wawekeze maduka yao hapa hiyo ni big noo waende zao
 
Sijaona shida ya Wachina kujenga viwanda hapa kwetu mkuu au kama labda sijakuelewa vizuri. Duniani kote na tangia enzi za adam wafanyabiashara wanataka kupata faida kubwa jinsi inavyowezekana.

Ukiangalia vizuri utagundua kuwa Marekani na matajiri wengine walihamishia viwanda vyao china Vietnam Indonesia ufilipino na kwingineko kwa sababu ya gharama mishahara kodi maji umeme nk- kuwa rahisi sana ukilinganisha na kwao.

Baada ya miongo kadhaa china na Vietnam na wengine wameendelea na gharama za biashara si rahisi tena kama zamani.

Kwahiyo kwa sasa wanatafuta sehemu ambazo gharama hizi ni rahisi ambako ni huku kwetu na ukiangalia wameingia sana Ethiopia na nchi nyingine za kiafrika.

Cha kufanya hapa ni kujipanga kama nchi tuwalazimishe waingie ubia na makampuni ya hapa isipokuwa tu pale ambapo makampuni yetu hayana utaalam katika uzalishaji wa hizo bidhaa mathalani vifaa vya elektroniki
 
Sijaona shida ya Wachina kujenga viwanda hapa kwetu mkuu au kama labda sijakuelewa vizuri. Duniani kote na tangia enzi za adam wafanyabiashara wanataka kupata faida kubwa jinsi inavyowezekana. Ukiangalia vizuri utagundua kuwa Marekani na matajiri wengine walihamishia viwanda vyao china Vietnam Indonesia ufilipino na kwingineko kwa sababu ya gharama mishahara kodi maji umeme nk- kuwa rahisi sana ukilinganisha na kwao. Baada ya miongo kadhaa china na Vietnam na wengine wameendelea na gharama za biashara si rahisi tena kama zamani. Kwahiyo kwa sasa wanatafuta sehemu ambazo gharama hizi ni rahisi ambako ni huku kwetu na ukiangalia wameingia sana Ethiopia na nchi nyingine za kiafrika. Cha kufanya hapa ni kujipanga kama nchi tuwalazimishe waingie ubia na makampuni ya hapa isipokuwa tu pale ambapo makampuni yetu hayana utaalam katika uzalishaji wa hizo bidhaa mathalani vifaa vya elektroniki

sisi tuna tatizo la watanzania kutokuangalia biashara ya dunia kabla na kuandaa sera na miongozo inayowafanya wanufaike na biashara.

tunachokitaka ni kitu chochote ambacho mtanzania anaweza kuzalisha hapa serikali iwezeshe watanzania kuzalisha. tunataka malighafi zinazopatikana hapa zipewe kipaumbele na baada ya kukosa malighafi ndani basi ndio ziada iagizwe nje.

sisi tulikuwa usingizini, tumestuka ghafla tunaanza kudai kwa nini njiti za meno zitoke china. wao wameona hilo na bado wanataka kulinda soko lao hivyo wanafanya mikakati ya wao kujenga kiwanda cha njiti za meno kwetu.

kama tunawaza vizuri sidhani kama tunahitaji mchina kuja kuzalisha njiti za meno hapa kwetu bali tunataka watanzania kuzalisha njiti hizi. kuna soko kubwa la pikipiki hapa kwetu hivyo wachina tunaweza kuwaita watengeneze pikipiki.

hizo ndio njia za kuondoa umasikini kwa watanzania kwa kuangalia kile wanachoweza kufanya wenyewe ni serikali kuwawekea mazingira ya kisoko, ki mitaji na ki nyenzo ili wazalishe wenyewe.
 
mkuu nakubaliana nawe kwa upande flan lakini kwa upande mwingine bado nasimamia point yangu ya awali. tukianza na sisi watanzania ni ukweli usiopingika kuwa wengi wa fanyabiashara wakubwa kariakoo wanafanya biashara ya uchuuzi (kwenda kuchukua mzigo china thailand india na uturuki na kuja kusambaza tanzania na nchi za maziwa makuu).

Lakini pia hawa hawa wafanyabiashara wakubwa wana mitaji ya kutosha sana kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama ulivyosema mathalani toothpicks, toileries, viwanda vya kusindika mafuta ya kula na juisi, vya kutengeneza vyakula vya mifugo viwanda vya fanicha etc (unaweza kuingia alibaba.com ya china uangalie bei za hizi mashine ziko hewani tu).

Mpaka sasa kuna wafanyabiashara wachache sana wachuuzi wakiwemo wakina saba general (nimeona wanatengeneza toilet papers) wameweza kupata akili ya kubranch into manufacturing wengine wanaendelea na uchuuzi.

kwa hiyo shida hapa sio serikali imewakataza ama hawana mitaji.shida ni tofauti kabisa.

Sasa kama sie bado tunaona dili kwenda kuchukua waipaza, riflektaz etc china wakati uwezo wa kimtaji tunao wa kuvitengeneza hapa kwann tuwazuie wachina wasijenge hivyo viwanda?
 
mkuu nakubaliana nawe kwa upande flan lakini kwa upande mwingine bado nasimamia point yangu ya awali. tukianza na sisi watanzania ni ukweli usiopingika kuwa wengi wa fanyabiashara wakubwa kariakoo wanafanya biashara ya uchuuzi (kwenda kuchukua mzigo china thailand india na uturuki na kuja kusambaza tanzania na nchi za maziwa makuu). Lakini pia hawa hawa wafanyabiashara wakubwa wana mitaji ya kutosha sana kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama ulivyosema mathalani toothpicks, toileries, viwanda vya kusindika mafuta ya kula na juisi, vya kutengeneza vyakula vya mifugo viwanda vya fanicha etc (unaweza kuingia alibaba.com ya china uangalie bei za hizi mashine ziko hewani tu). Mpaka sasa kuna wafanyabiashara wachache sana wachuuzi wakiwemo wakina saba general (nimeona wanatengeneza toilet papers) wameweza kupata akili ya kubranch into manufacturing wengine wanaendelea na uchuuzi. kwa hiyo shida hapa sio serikali imewakataza ama hawana mitaji.shida ni tofauti kabisa.sasa kama sie bado tunaona dili kwenda kuchukua waipaza, riflektaz etc china wakati uwezo wa kimtaji tunao wa kuvitengeneza hapa kwann tuwazuie wachina wasijenge hivyo viwanda?

wananchi kuzalisha sio swala la mwananchi yeye binafsi bali ni swala la serikali kutengeneza mazingira na hapa serikali inatumia taasisi kama SIDO, TIRDO na mengine kuwawezesha, inakuwa na mabenki ya kuwapa mitaji, inakuwa na mifumo ya kodi inayoendana, inakuwa na sera kwa ujumla za kuwalinda na kuwakuza wajasiriamali lakini kwetu viongozi wanapiga kelele tu lakini mfano nenda kanunue kitambaa ushone nguo alafu ukanunue nguo ilishonwa malasia utakuta ya malasia bei iko chini, hii inaonyesha mifumo yetu ya kodi ni kichaka kimojawapo cha bidhaa za nje kumiminika kwenye masoko yetu.
 
Nasikia eti china itaisadia Tanzania kujenga viwanda ????? Jambo tunalotakiwa kufanya kwa wakati huu kama tunataka kujenga uchumi wetu tusikubali mataifa makubwa eti kutusaidia kujenga uchumi wetu.

uchumi wa dunia ni wa kunyanganyana, biashara ni ileile na waliozishikilia biashara hizo ndio wana uchumi mzuri na ndio matajiri na wazembe wanaosubiri kusaidiwa ndio hubaki masikini. ili masikini aweze kuinuka inabidi na yeye kuingia katika biashara na kuzichukua baadhi ya biashara na hiyo ina maana ya matajiri hao watapoteza baadhi ya biashara. yaani masikini anapanda juu na tajiri anashuka chini.

matajiri hawa ni wajanja sana kwa kuangalia upepo unavyovuma kwa masikini na kutafuta mbinu za kubaki juu.

hawa wameona kile ambacho nchi yetu imekingamua kuwa hatuwezi kuagiza hata vitu vidogo vidogo kwao na wametafuta solution tayari ya kuja kuzalishia huku kwetu na katika misaada hiyo tutajikuta tunabaki kuwategemea kwa kila kitu mpaka nafasi za ajira kwenye viwanda hivi tunagawana.

kama tunataka kuendelea China ni mfano tunaotakiwa kuiga kwa kuwatumia watu wetu kuiga wanayoyafanya kule kwao tuyafanye hapahapa na yale tu tusiyoyaweza sisi ndio tuwaite wageni.

watanzania wengi wanauwezo wa kutengeneza baadhi ya bidhaa za nje kwa kuziiga na tumekuwa tukiziita bidhaa feki bila kutambua hivyo ni vipaji ambavyo tumeshindwa kuendeleza na tunahangaika kuwakamata badala na kuanza kuwasajili ili wazalishe kihalali na kuwapa mbinu za kutotumia majina ya nje kama nembo ya bidhaa zao bali watumie nembo zao na tulinde soko lao.

wachina hawa wamekuwa wakilalamikiwa na marekani kuwa wanaiba technolojia zake na sisi tunatakiwa kuwaiga katika sekita ya uzalishaji.

lazima tutambue kuwa kujenga viwanda wanasema ni mpango wao wa maendeleo wa miaka 5 hivyo tayari wameandaa katika njia ambayo position yao ya sasa na ya kwetu itabaki palepale.

haya si mambo pia ya kwenda kwenye majukwaa na kusema hatuwataki wachina watuzalishie kwani tunahitaji transition period ambayo urali wa biashara utaenda unabadilika taratibu. hivyo tukae chini tuandae mpango ambao tukiutekeleza utabadili urali wa bishara taratibu sisi wenyewe kwa kujua ni kitu gani tuzalishe sisi wenyewe na kwa wakati gani na kile tunachoagiza tuagize kwa kiasi gani.
Taaluma yako mkuu?
 
kwa upande wa mifumo ya kodi nakubaliana nawe mia kwa mia. Anyway mtizamo wangu mimi ni kuwa sisi (mwananchi mmoja mmoja na mamlaka pia) tuna sehemu kubwa kwenye hili tatizo lakini pia sioni kama ni sawa kuwazuia wachina wasiweke viwanda hapa (ili mradi isiwe janja ya kuimport finished goods ambazo wanazipaki vichochori kariakoo na kwengine)
 
Sidhani kama wanakuja "kutujengea" viwanda.They just can't do that,halafu na sisi hatuwezi kukubali.Nadhani wanakuja kuwekeza kwenye viwanda na hili ni zuri.Na kama hivyo ndivyo,sioni shida.You cannot do everything yourself.Tuwaruhusu wawekeze kwenye viwanda na hata maeneo mengine halafu tuwatoze kodi kisawa sawa.Then as our economy improves, na sisi kama serikali tu invest kwenye maeneo ambayo wakati huo tutaona yanalipa sambamba na Wachina na wawekezaji wa ndani.Ingawa binafsi sioni haja sana sana serikali kujiingiza kwenye biashara ambazo sio strategic.

Back
Top Bottom