Eti Azam ni waleta mapinduzi ya soka hapa nchini,NAKATAA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Azam ni waleta mapinduzi ya soka hapa nchini,NAKATAA

Discussion in 'Sports' started by Anselm, Jul 25, 2012.

 1. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wengi wamekuwa wakiamini uwekezaji ulio' na unaoendelea kufanywa na mmiliki wa Club ya mpira wa miguu ya Azam ni njia mojawapo itakayoligeuza soka la Tanzania kutoka kwenye u'kichwa cha mwendawazimu kwenda kwenye level nyingine, kitendo chao cha kumchapa Mnyama jana goli 3-1 kinaonekana kukoleza dhana hiyo na kuamini kuwa enzi za Tanzania kuchukulia mpira ni Simba na Yanga ndo zinaishilia taratibu kama siyo zimemalizika kabisa.
  Ni kweli wamiliki wake wamewekeza sana katika team hiyo,wamesajili vizuri,wana walimu wazuri,madaktari wazuri,uwanja mzuri,Hostel nzuri vifaa vya team (mabasi na vifaa vingine vya mechi na mazoezi) vizuri tuseme almost wana kila kitu kizuri, lkn je uwepo wa team hii yenye kila kitu kizuri katika ardhi ya Tanzania kunaweza kuwa na mchango wowote chanya kwenye maendeleo ya hili soka la nchi yetu?
  Hapa nitaongelea jambo 1 tu...
  Issue ya Mrisho Khalfani Ngassa, habari nilizozipata kutoka kwenye chanzo changu cha kuaminika kabisa ni kuwa Mchezaji huyu sasa hivi yuko kwenye mgomo usio rasmi unaotaka kufanana na ule wa madaktari wa hii Republic yetu, akishinikiza aruhusiwe kurejea kwenye Chama lake lililomuweka katika ramani ya juu katika usakataji wa kabumbu hapa nchini,lakini Viongozi wa Club hiyo wamemgomea na wamesema watamshikilia mpaka atakapomaliza mkataba wake.Licha ya team ya Yanga kujaribu mara kadhaa kuongea na viongozi wa Azam kuhusu kumnunua mchezaji huyo kwa njia tofautitofauti kama Cash kwa dau watakalolitaja Azam wenyewe au Cash plus mchezaji bado Viongozi wa team hii wamezikataa offer hizo pamoja na kujaza wachezaji wengi wa ndani na nje ya nchi wenye uwezo kama au pengine zaidi ya Ngassa....je kitendo hiki cha hawa Viongozi wa Azam ambacho dhahiri kinataka kufanana na cha wale viongozi wa team Swahiba wao (cha kukomoana) hakirudishi nyuma maendeleo ya soka la nchi hii kweli?,leo hii Ngassa mchezaji anayeweza kuwa na mchango mkubwa tu kwa team yake ya Taifa anashindwa kutumika vizuri kwasababu ndogondogo ambazo zingeweza kufanyiwa kazi na kumfanya aifanye kazi yake(ambayo ni kucheza mpira) kwa ufanisi wa hali ya juu kwa maendelo yake binafsi,Club yake na team yake ya Taifa.
  Nilistaajabu sana kuona Ngassa akipewa dk 13 tu katika mechi kati ya team yake ya Azam na Tusker huku jana nikimshuhudia akisugua benchi kwa dakika zote 90+5...sikubaliani na hili kabisa,hawa Mabwanyenye waache kuua kipaji cha Mshikaji wamuache aje apige soka Jangwani, Taifa bado linamuhitaji akina Msuva,Atupele na Christopher Edward kule Ngorongoro Herois bado wanahitaji kujifunza vitu kutoka kwake.
   
 2. m

  mbeshere Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hicho ndio Azam wanataka kukomesha ulimbukeni wa usimba na uyanga ambao pia wewe unaonekana ni mnazi ,
  Kwani Ngasa haujui mkataba wake na na Azam ukoje ? sasa anapoleta mapenzi kwenye kazi hayo ndio madhara yake kwanini aliamua kusaini azam kwa mbwebwe na fedha nyingi halafu leo anataka kurudi yanga....hawa wachezaji wetu hovyo kabisa acha mpira wake uishe na akae benchi watatokea wengine wenye akili kupitia ujinga na dhabu yake...
   
 3. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,731
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Azam nao ni walewale yuko upande wa msimbazi kuikomoa yanga
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu hii ni kali nilitaka kushangaa anselm asihusishe na mambo ya yanga hapa hamna kitu kabisa...
   
 5. K

  Konya JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  nahisi kama issue ya msingi kwako ilikuwa ni mgogoro wa ngasa na azam yake(kama upo) coz nilimsikia kally akihojiwa baada ya mechi ilikuwa kipindi cha michezo capital redio amedai kwamba ngasa ni majeruhi(mgonjwa) na yeye alikuwa anajiumauma wakati akijibu hilo swali, mwisho wa siku ngasa ana mkataba na azam na nilazima aheshimu mkataba wake na kama ni uhamisho kuna taratibu za kufuata, kugoma,kuzira sijui haitamsaidia na kama ni kuuzwa au vipi ni suala lililopo mikononi mwa viongozi wake as far as his contract concern... but all in all azam wanaleta/wataleta changamoto kwenye haka ka ligi ketu kalikokuwa ka timu mbili tu
   
 6. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa waliifunga Yanga 3-0?
   
 7. Tisha-TOTO

  Tisha-TOTO JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 1,173
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  No. Ni kwa kuwa waliiwekea kauzibe Simba na kuiwezesha Yanga Afrika kuwa bingwa wa TZ 2010-2011 na pia kuifanya mwaka huu Yanga Afrika kucheza fainali ya Kagame na Vita SC badala ya Simba kama ilivyokuwa mwaka jana!!
   
 8. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Bro naona bado unaweweweseka na ile 3-1,
  Nataka nikuambie mchezaji kutaka kurudi kule alipotoka siyo dhambi ya kumfanya sijui aadhibiwe au vp,yeye ni mchezaji na mpira ndo kazi yake,Azam walipanda dau aka'sign sasa ameona hawana jipya anataka kurudi nyumbani ni kwanini wambanie wakati hawaihitaji service yake,waliondoka Nasri na Febregus wakati Wenger akiwahitaji kwanini ishindikane kwa Ngassa ambaye hahitajiki?
  Hivi vitabia vya Viongozi wa type hii ndo vinavyodumaza mpira wetu,kwanini tusiige wenzetu wanaendeshaje michakato ya aina hii?
   
 9. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kiongozi Kally ni muongo ndo maana alikuwa anajiumauma na ukitaka kujua Ngassa ni mzima si unaona alicheza dakika 13 mechi na Tusker,kilichopo ni kuwa baada ya Ngassa kuwaomba kama vp wamuuze back Yanga wakakataa automatically morale yake ikashuka na kusababisha performance yake ishuke pia anzia mazoezini mpaka kwenye mechi ,sasa wao Viongozi wa Azam wanaamini mshikaji yuko kwenye mgomo baridi ili aachwe,na Viongozi na wenyewe wamejiapiza (kama alivyojiapiza "naniliu" kwenye issue ya Yondani) kuwa hawatamwachia....sawa all in all ana mkataba kwani mkataba hauvunjwi? mwenyewe anataka kuondoka kama anavyotaka kuondoka RVP kwanini iwe issue...viapizo viingi,hivi viapizo vitatufikisha wapi?
   
 10. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Sawa lkn mnaua mpira wa Dogo,kwanini msimuachie aje ang'arishe nyota yake Jangwani mna wachezaji kibao wazuri wa namba yake,yuko Kipre Tchetche sijui Kipre Bolou,Khamis Mcha na wengineo kibao....yaani Viongozi wa hiyo team yenu na ile team mliyoi'ulimboka jana dugu moja
   
 11. M

  Masuke JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Acheni malumbano jiandaeni na mechi za kesho, sisi kazi yetu sasa ni kushangilia wageni tu hasa AS VITA.
   
 12. Aleyn

  Aleyn JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 10,228
  Likes Received: 13,671
  Trophy Points: 280
  Kwani Mkataba wake unaisha muda gani? Kiukweli Azam mimi binafsi nawachukia sana japokuwa wameifunga Simba ila sijafurahi kiviiile. Kwa sasa Azam wasilete uwendawazimu wamruhusu tu Ngassa arudi nyumbani sisi bado tunampenda sana
   
 13. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nikutafute kesho Kaka twende ground?,lkn tutakaa jukwaa la Yanga ili ushangilie vizuri hao Wageni wako
   
 14. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkataba wake unaisha mwakani,ndo maana kuna watu wamemshauri kama vipi atulie mwakani arudi bure,tutamkatia fuba lake binafsi wakati Azam watatoka mikono mitupu ingawa wao hili hawalioni kama litawaathiri,wanachoangalia wao ni kuikomoa Yanga.
   
 15. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ngasa hana tena kiwango kama zamani. Hata akirudi Yanga hatapeleka changes zozote.
   
 16. daniel don

  daniel don Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu, haiwezekani mchezaji kama ngassa hii leo akasugua benchi wakati hakuna mtu asiyemjua Ngassa anavyocheza. Huo ndo mwanzo wa kuua kipaji cha dogo, kama ni kweli kuna ka mgomo baridi kwa Ngassa ni bora awe wazi watu wote wajue kama ngassa anaiota Jangwani kuliko kupotelea benchi ama kuua kabisa kipaji..Rudi Yanga urudishe uwezo kama Chuji.
   
 17. Zeddicus Zu'l Zorander

  Zeddicus Zu'l Zorander JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 571
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 60
  Nadhani umefika wakati wachezaji inabidi waeshimu mikataba yao,Azam walimsajili Ngassa ili acheze mpira,Nawaunga mkono Azam, kama bado wanamuhitaji waeendelee kuwa nae,
  Kwani Modric ameomba kuondka mara ngapi Tott, lakini as long as walikuwa wanamhitaji walisema no, na yeye aliendelea kujituma msimu wote uliopita.
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Soka la bongo bwana, hivi kuzifunga Simba au Yanga ndo kuleta mapinduzi katika soka la Bongo? Kuna nini kipya? Ndo kuipandisha Tz katika Fifa ranking? ndo kutengeneza football academies? ndo kuongoza soka kwa kufuata taratibu? Ndo kuwa na viwanja stahiki? Sidhani kama ni mapinduzi kwa soka la Bongo, labda mapinduzi kwa SOKO la bongo!!!!
   
 19. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Zeddicus huwezi kulinganisha issue ya Modric na Tott yake na Ngassa na Azam yake,wakati Modric anapoomba kuondoka Tott wanamkatalia ksbb wanamuhitaji ni kweli wanamuhitaji kiwanjani siyo kwenye daftari la usajili kama ilivyo kwa Ngassa Azam,Modric anahitajika sana Tott na anatumika sana uwanjani sote ni mashahidi lkn inakuwaje Ngassa ahitajike sana Azam na kutumika sana pale benchi?
   
 20. k

  kicha JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 519
  Trophy Points: 180
  porojo lote ilo kama skosei point kuu ni kwa nini ngasa hachezeshwi kwa kua wewe unampenda, mpira una taratibu zake kaka na mwalimu ndio muamuzi wa kila kitu, ikiwa sababu ni kiwango, sijui haitaki azam nk hilo atajua yeye mwenyewe ila kama mwalimu ndie mwenye maamuzi, basi huangalia maslahi ya timu kwanza halafu nyie wapenzi wa ngasa sijui wa yanga mtabaki kupiga domo ambalo sidhani kama lina tija kwa azam.
   
Loading...