Eti Arusha ni jiji la "chapombe?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti Arusha ni jiji la "chapombe?"

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kyachakiche, Aug 28, 2009.

 1. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Katika Gazeti la Business Times( Aug 28-Spt 3, 2009), kuna habari kwamba pamoja na Jiji la Arusha kuitwa Geneva ya Afrika, yawezekana huko tuendako likabadilika na kuitwa jiji la wanywa bia(chapombe)!

  Inaelezwa kwamba, kiasi cha hela za Kitanzania millioni 288.6 hutumika kwa ajili ya kununulia bia pekee tena zinazotengenezwa na TBL tu bila ya kuhusisha zile zinazotengenezwa na makampuni mengine au aina nyingine za vilevi ikichukuliwa wastani wa Tshs 1,300 kwa chupa. Na hii ni sawa na lita 111,000 za bia kwa siku.

  Kwa mujibu wa bwana Fimbo Butallah ambaye ni Brand Manager wa bia aina ya Safari tawi la Arusha, kiasi cha lita million 70 sawa na bia 140million ambazo huzalishwa kwa mwaka, asilimia 57 hunywewa na wakazi wa Arusha pekee. Kiasi kinachobaki hutumiwa na mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Singida.

  Wakuu, hebu tujadili, hii inamaanisha nini? Kazi hufanywa saa ngapi na akina nani? Nawasilisha!
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Safari ni moja kati ya brand nyingi za bia zinazotengenezwa na TBL kwa hiyo kwa kuwa safari ina wanywaji 57% hatuwezi chukulia kwamba zote zitakuwa the same au zaidi. Hicho siyo kithibitisho kwamba Arusha ndo inaongoza
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwani kazi wewe una-define vipi?
   
 4. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona mnakanganya??? Mlishasema tutumie bidhaa zetu za ndani. Zamani ilikuwa tunakunywa bia za Kenya kwa sasa twtumia vyetu shida. Hapo inakuwajee?

  Kusema kazi zitafanywa saa ngapi nakushauri jambo moja tuu! nenda fanya utafiti wako kwa hawa watu wa Arusha pia waulize kazi waifanya saa ngapi. Ina maana hawa watu wanapiga kazi sana na saa ya bia hakuna mtu anaomba bali ni zungusha nami ni zungushe hakuna kudandiana hapo.

  Alafu inaelekea unawanafkia wanaArusha acha chuki watu wanafanya kazi sana kipimo ni kuwa ujambazi umedhibitiwa umehamia Dar kwa sasa. Unaweza kunijibu hilo?

  Mkoa hata president anaufagilia au unasemaje?.
   
 5. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Habari hii inavested interest kwa wadau. TBL na customers. Inamaana wewe unataka nini hasa ktk hilo? Nani aliekosa kwenda kazini sababu ya kunywa bia Arusha? Fanya utafiti wa mkoa gani wanaenda kazini zaidi kuliko mingine then uje na utueleze sababu ni zipi? Infact this thing has some business implications to the TBL, managerial implications to the lacal authorities, and financial and moral consequences to households. Weekend njema. Karibu sana Sakina.
   
 6. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  hii inaonesha sisi wakazi wa arusha ni wazalendo tunatafuta mahela na kuyatumia kwa kununua bidhaa za ndani kwa wingiiiiii, m288.6 sio mchezo ati,natoa wito kwa mikoa mingine waige mfano huu.
   
 7. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu nimekupata, ingawa hivyo, hii niliyoiweka ni sehemu tu ya taarifa ya hilo gazeti na kwamba jumla ya kiasi cha uzalishaji wa bidhaa nyingine za TBL tawi la Arusha pia imefafanuliwa. Kimsingi, kufuatia takwimu alizotoa huyu manager, safari ndiyo inayoongoza kwa uzalishwaji na hivyo kufanywa kuwa moja ya kigezo.
   
 8. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Unaweza kuanza mada pia ya kutaka kujua watu wana-define vipi kazi!
   
 9. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu mbona unakuwa mkali, mimi nimebandika kama nilivyoipata kwenye source ili tujadili kwa pamoja. Ukiniuliza nina chuki na watu wa Arusha utakuwa hunitendei haki, after all mimi niko Arusha pia!
   
 10. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  hii ni matatizo bia 110,000 lita za bia kwa siku ni balaa,nimeona pahali leo hii hii stockholm kipindi cha summer juni to july kiasi cha lita 49,000 za pombe zimenywewa na wameona ni kiasi kikubwa sana mpaka kuanzisha counselling ya kushauri watu wapunguze alcohol,sasa hiyo 111,000 lita kwa mji wa arusha tena kwa siku hayo ni mauaji,na kweli hapo inaelekea watu wanafanya kazi na wanalamba bia wakati huo huo,hayo maendeleo sijui yatakuja lini.
   
 11. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kyachakiche kikacha nakwi lalu mangi? data zaonyesha mkoa wa Arusha watu zaidi ya asilimia 50 ni wahamiaji na ni wapangaji.

  Wenyeji wameona ili kujinasua kwenye umaskini nao wamejenga nyumba kwa ajili ya kuwapangishia wakuja. Industries za madini na utalii ndo zalipa au ndo uchumi wa mkoa achia mbali kilimo na mifugo. Kwa hiyo basi ni mkoa wa neema wenye kuwapa watu baraka za kunufaika.
   
 12. S

  Simoni Member

  #12
  Aug 28, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Arusha kwa maana ya mkoa? Au kwa maana ya Manispaa ya ARusha? Kama ni mkoa then it is not a big deal. Watu wana vijisenti na wanakuza uchumi wa nchi bwana.
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kwanza nianze kwa kusema kuwa umewakosea sana watu wa arush kwa jinsi ulivyoweka kichwa cha mada yako. Sidhani kama kwenye source uliyopata habari hii waliuliza swali kama hili. Pia sishawishiki kuamini kuwa huyo manager wa TBL wakati anatoa habari hii aliuliza swali kama hilo. Kwahiyo kwanza nakuomba uwaombe radhi wakzi na wenyeji wa Arusha kwa jinsi ulivyoweka mada yako.

  Pili nikuambie kuwa kuuliza kuwa watu wa Arusha wanafanya kazi saa ngapi ni kukosa uelewa wa mambo mengi san. Ni sawa na kuuliza hivi watu wenye post nyingi hapa JF wanafanya saa ngapi kazi zao. Mimi nafikiri kabla ya kuuliza au kuandika jambo ujiulize mwenyewe kama unachokiandika kina usahihi au unauliza tu.

  Mwisho nikufahamishe kuwa katika mikoa ambayo watu wanafanya kazi kwa kujituma kwenye sekta zote basi Arusha ni miongoni mwao. Tazama kuanzia kwenye sekta ya madini, utalii, biashara na nyingine nyingi.
   
 14. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sidhani hat kama mtoa mada anaijua Arusha vizuri na pilika pilika za watu wa pale. Kwahiyo hata swali ulilomuuliza atapata ugumu sana kulijibu na akilijibu nina uhakika utacheka tu
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu umeona jinsi alivyokujibu? Eti uanzishe mada kwa swali lako
  huyu muanzisha mada sijui ana maaan gani kwa sababu unapoanzisha mada pia ujitahidi kujibu na maswali ambayo wadau watakuuliza.
  Au wewe kazi kwako ni kulima?
   
 16. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Malyaaruwa! Kiche na aando koose nakamwii! Karibu niko Sanawari.
   
 17. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  This man doesn't know all these issues
   
 18. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Acha hizo wewee, mbona na wewe hukumjibu? Hii ni mada, yeyote anaweza kumjibu, kuchangia zaidi ama kukaa kimya!
   
 19. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Siamini kwamba kwa mtu "anayeonekana kuwa makini" kama wewe ungefikiri kwamba mtu mwingine makini angewaza kama hapo palikokolezwa!
   
 20. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuacha itakuwa ngumu hasa pale ambapo naamini kuwa naongea au kuandika ninachokijua. Kimsingi ulitakiwa ukae kimya basi pasipo kujibu au kwa kuwa muungwana zaidi hungesema tu kuwa hujui, tukueleweshe
   
Loading...