Eti alikuwa bungeni na alikuwa waziri kwa miaka yote hii

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,634
Hiyo ni moja ya vijihoja vinavyozungumzwa sana na watu 'wenye akili' [naona ukiwa anti-Magufuli humu basi eti wewe una akili ] kuhusu hizi jitihada za rais hususan kuhusu mikataba ya madini.

Okay, sawa. Yeye alikuwa mbunge kwa miongo miwili na amekuwa naibu waziri na waziri kwa karibu muda huo huo.

Sasa, hata kama alikuwa hivyo vyote, so what?

Ndo asifanye haya anayoyafanya sasa?

Mnataka afanye nini sasa?

Akifanya mnalia hivi....asipofanya napo mtalia vile tu. Si ajabu naye mtaanza kumwita dhaifu.

Watu hamna jema kabisa nyie.

Ni rahisi sana kujikalia huko mlipo na kusubiri wengine wafanye ili tu mpate fursa ya kukosoa.

Eti ooh alikuwa mbunge....alikuwa waziri....so freakin' what?

Asifanye chochote kısa tu alikuwa mbunge na waziri?

Mnataka aache mambo yaendelee kuwa kama yalivyokuwa au?

Wahshi kabisa nyie.

Watu mmekalia kupinga tu. Saa ingine hata mnachopinga hakieleweki.

Hicho kihoja chenu ni dhaifu mno. Kwa sababu tu yeye ni CCM haina maana ya kwamba ndo asifanye chochote kile kısa tu CCM ndo iliyotufikisha hapa tulipo.

Asipofanya yeye mnataka nani sasa afanye? Babu Lowassa?

GTFOH
 
Nyani siku hizi umeshuka viwango! nahisi wewe ni NYANI RAPPER Sio yule wa zamani tunayemjua! kiongozi anatakiwa ajulikane misimamo yake juu ya maswala mbalimbali.sio leo unapenda yanga kesho simba.leo wapinzani marufuku.kesho umechagua.unajua huko USA kila kiongozi wanamtathimini kutokana na mitizamo yake aliyowahi kutoa katika maisha yake ya siasa?
 
Kamati 1&2.....Wezi..wezi..wezi..wezi....tunapendekeza hawa wezi wachukuliwe hatua za kisheria.

Rais......Wezi..wezi..wezi..wezi nakubaliana na mapendekezo yote ya kamati na nayachukua kama yalivyo bila mabadiliko yoyote.

Hitimisho (rais)...Nendeni mkakae mjadiliane na wezi ni jinsi gani watalipa walichotuibia.

Wezi....sisi hatukubaliani Kabisa na kilichopo kwenye report ya kamati ya 1 na ya 2.

Najiuliza tu haya maelekezo yaliyotolewa ya kwenda kwenye majadiliano na wezi ambao kimsingi hawajakubali kuwa ni wezi..majadiliano hayo yatafanyikaje. Na endapo yatalazimishwa na wezi kushikilia msimamo wao kuwa wao sio wezi itakuweje?? Unajadiliana na wezi??only in Tanzania.
 
Nyani siku hizi umeshuka viwango! nahisi wewe ni NYANI RAPPER Sio yule wa zamani tunayemjua! kiongozi anatakiwa ajulikane misimamo yake juu ya maswala mbalimbali.sio leo unapenda yanga kesho simba.leo wapinzani marufuku.kesho umechagua.unajua huko USA kila kiongozi wanamtathimini kutokana na mitizamo yake aliyowahi kutoa katika maisha yake ya siasa?
Wewe siasa za USA unazijua au unazisikia tu?

Yule kibibi gagula wenu Hilary mpaka leo bado analaumu wengine huku yeye mwenyewe akijiacha....
 
37 Reactions
Reply
Back
Top Bottom