Ethiopia: Waziri Mkuu asema lazima Serikali isimamishe msaada wa chakula ili kuepuka shinikizo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Waziri Mkuu wa Ethiopia amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kimataifa juu ya vita kaskazini mwa nchi hiyoImage caption: Waziri mkuu wa Ethiopia amekuwa akikabiliwa na shinikizo za kimataifa juu ya vita kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anasema nchi hiyo inahitaji kukoma kupokea msaada wa chakula ili kuepuka shinikizo za kigeni dhidi ya serikali, Kituo cha televisheni cha kinachomilikiwa na serikali ETV) kimeripoti.

"Tukihakikisha vitu hivi vinavyoitwa ngano [msaada wa chakula] haviingii Ethiopia, asilimia 70 ya matatizo ya Ethiopia yatasuluhishwa.

"Tatizo la Ethiopia ni msaasa wa ngano. Kutokana na msaaada wa ngano kunakuja magonjwa. Kutokana na masaada wa ngano kunakuja mambo mengi, athari nyingi. Tukisimamisha, baadhi ya matatizo yatasuluhishwa ," Bwana Abiy alisema.

Waziri Mkuu alisema hayo alipozuru mashamba ya ngano katika eneo la Oromia.

Ethiopia, ambayo ni miongoni mwa nchi ambazo zinapokea misaada ya kigeni, inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa nchi kadhaa za magharibi kutokana mzozo wa Tigray kaskazini mwa nchi, ambako ambapo mamilioni wako katika hatari ya njaa.
 
Back
Top Bottom