Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,888
- 143,985
Ni kweli hivi vitu tunavihitaji lakini sidhani kama ni sahihi kuvifanya viwe ndio vipaumbele vyetu vikuu kwa sasa tena kwa kuvitekeleza vyote kwa pamoja na pengine kwa gharama ya kukwamisha mambo mengine.
Sidhani kama ni sahihi kuelekeza fedha nyingi katika haya maeneo huku maeneo mengine nyeti kama kilimo,elimu na uhamasishaji na uendelezaji wa viwanda yakionekana kudorora.
Tanzania tunahitaji kuwekeza zaidi katika kilimo kinachogusa watu wengi pamoja na kuendeleza na kufufua viwanda mbalimbali ambavyo vitatoa ajira kwa watu wengi na kuongeza pato la Taifa hasa tukiwa na viwanda vingi vitakavyotumia mazao ya kilimo kama malighafi sambamba na viwanda vingine vitakavyotumia malighafi tofauti na mazao ya kilimo.
Ndugu zangu,ndege,fly over,treni za kisasa,n.k bila ustawi wa viwanda, kilimo, elimu, n.k,vitu hivi haviwezi kuleta tija inayokusudiwa.Hivi vitu ili viwe na tija ni lazima viambatane na uwepo wa shughuli nyingi za kiuchumi tofauti na hapo watu wengi watatumia miundombinu hii kusafiri kwenda kusalimia ndugu na jamaa na zaidi kusafirishia wagonjwa.
Hivi vitu ni vichocheo tu vya uchumi lakini huwezi kuchochea moto pasipo kuwa na kuni na kuni zetu hapa ni viwanda pamoja na kilimo huku tukiwa na sera za kutoa ruzuku kwa wakulima na mambo mengine ya aina ikwamo kutoa mafunzo kwa maafisa kilimo na wakulima wenyewe pamoja na kuwa na mipango na sera zitazovutia watu kujenga viwanda hapa nchini.
Kwa mfano,treni zitasafirisha nini kama hakuna mazao au bidhaa za viwandani zinazohitaji kusafirishwa kwa wingi ili treni iwe na tija?
Tukiwa na viwanda vingi maeneo mbalimbali ndani ya nchi,hatuoni watu watalazimika kusafiri kwa wingi kwenda makazini na kuongeza abiria watakaotaka kupanda treni kuwahi makazini?
Tumetenga fedha kiasi gani kutangaza utalii ili hata hizo ndege ziweze kupata abirai wa kutosha ambao watakuwa ni watalii wanaokuja hapa nchini?Lakini pia tunazingatia ukweli kuwa biashara ya utalii ni biashara ya msimu?
Au tunasubiri ndege ziwasili ndio tuanze kutangaza utali kwa nguvu kubwa?
Labda tujiulize wenzetu Ethiopia wenye ndege, treni za umeme,fly over,n.k hali ya maisha ya wananchi wake ikoje?
Sio ndio hawa hawa kila siku wanakamatwa hapa nchini kama wahamiaji haramu wanaotaka kuvuka mipaka kutafuta maisha katika nchi nyingine?
Ni kweli tunahitaji ndege,fly-overs, treni za kisasa,n.k, lakini ni lazima pia tu-balance mambo ili hivi vitu viweze kutuletea tija tunayoitaka.
Badala ya kununua ndege sita kwa wakati mmoja,nunua ndege tatu kwanza(ATCL ilikufa taratibu,tuifufue taratibu)na hizo fedha zingine zielekezi kwenye kilimo,kufufua viwanda, kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji,n.k
Mfano mwingine ni Kujenga reli ya kisasa kutoka Dar kwenda Kigoma.Hili ni jambo jema na lenye logic kabisa, ingawa nalo lina madhara yake, lakini hili la kujenga SGR kutoka Dar mpaka Dodoma kwa sasa sidhani kama ni jambo la zima na kwa mtazamo wangu ni bora hizo fedha zikaelekezwa katika maeneo mengime muhimu kwa sasa ikiwemo sekta ya Afya,umeme vijijini,mikopo ya elimu ya juu,n.k.
Bwana mkubwa mmoja alishauriwa kuwa makini na sera zake za ubinafsishaji wa mashirika ya umma lakini hukusikiiza la mtu na kila aliempinga alionekana si mzalendo ila baadae ukweli ulikuja dhihirika hivyo na huyu wa sasa nae ni swala la muda tu kabla mambo hayajadhihirika.
Tunachokifanya kwa sasa ni sawa na mtoto anaejaribu kutembea kabla ya kutambaa.
Kupanga ni kuchagua.
Kwaherini.