Ethiopia: Waasi wa Tigray wakubali kusitisha mapigano kwa masharti

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Chama cha ukombozi wa Tigray TPLF kimeitaka serikali kuu ya Ethiopia iwaondoe wanajeshi kutoka kwenye jimbo la Amhara pamoja na wanajeshi wa nchi jirani ya Eritrea ikiwa ni masharti kabla ya wao kushiriki kwenye mazungumzo yoyote na serikali kuu kuhusu kusitisha mapigano.

Chama cha (TPLF) kilichokuwa kinaongoza katika jimbo la Tigray ambacho kiliondolewa mamlakani mwaka jana na vikosi vya serikali kuu ya Ethiopia kimetoa tamko hilo Jumapili katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle.

Taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa TPLF Getachew Reda imesema, chama hicho kitakubali kusitisha vita iwapo watahakikishiwa kwamba hakutakuwa na uvamizi dhidi yao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo TPLF inataka malalamiko yao mengine yatazingatiea na kutatuliwa kabla kufikiwa makubaliano yoyote kati ya pande mbili hizo.

Mara tu baada ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, kutangaza hatua ya kusimamisha mapigano, msemaji huyo wa TPLF Getachew Reda aliikosoa hatua hiyo na kuiita kuwa ni "mzaha".

Hata hivyo upande wa serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed haujatoa tamko lolote kuhusiana na kauli ya chama cha TPLF.

Chanzo: DW
 
Back
Top Bottom