Ethiopia: Updates on war against TPLF

Alice Gisa

Senior Member
Sep 6, 2014
172
417
Salaam,

Kwa mahaba yangu Nitakua naweka updates za mapigano yanayoendelea huko Ethiopia Kati ya Jeshi la Serikali na Waasi wa TPLF na Jeshi lao liitwalo TDF.

Kwanza Kuna vitu vya kuweka sawa

1. Vita siyo Kati ya Ethiopia na Jimbo la Tigray. Bali ni Vita ni Kati ya Ethiopia na Chama Cha TPLF. Chama hicho ndiyo kina Jeshi lake liloitwa TDF (Tigray Defence Force). Chama hiki wafuasi wake wengi ni watu wa Jimbo la Tigray ila siyo wote. Takwimu zinataja Chama kinaungwa mkono huko Tigray kwa wasitani wa asilimia 70. Hivyo kama 30 ya Watigray hawakikubali.

Chama hiki ndiyo kiliongoza mapigano ya kumpindua Waziri mkuu wa Zamani Mangisu Haille Mariam mwaka 1991. Baada ya kufanikiwa Mtigray wa kwanza akaongoza nchi hiyo Bw Meles Zenawi.

Melez ndiye alirudisha utawala wa majimbo uliokua umetokomezwa tangu 1975 baada ya mapinduzi ya mfalme Haile Selassie.

Aidha katika utawala wa Melez ndiyo Watigray walikamata fursa zote za taifa.

Baada ya kifo cha Melez na maandamano ya Waoromo na Wahmara ulifanyika uchaguzi mkuu akashinda Bw Ali Ahmed Ali mwaka 2018.

Bw Abiy kwa kabila ni Muoromo. Abiy akaanza mikakati ya kuweka usawa jeshini na kwenye taasisi nyingi nyeti za taifa. Jambo ambalo liliwaudhi Watigray.

Chuki hii ndo imefikisha taifa katika vita.

2. Napenda niweke sawa wiano wa watu Ethiopia. Nchi hiyo inamakabila mengi zaidi ya 20 ila Makabila makubwa ni matatu. La kwanza ni Oromo 34% la pili Ahmara 27%, na la tatu ni TIGRAY 06%.

3. Historia utawala wa Ethiopia ni Kati ya wa Ahmara na Tigray. Wa Oromo hawajajaliwa kutwaa kiti mara nyingi.

4. Wa Tigray na Ahmara ni Wahabeshi wakati Waoromo ni Wakush.

Mwisho wa UTANGULIZI.

Vita.
TPLF ni rafiki wa Magharib hasa US. Wakati Abiy ni rafiki wa nchi majirani hasa Eritria, Somali hadi UAE. Sababu ya hili ni moja, Watigray huwa ni vibaraka wa US, kusimamia maslahi ya US katika pembe ya AFRICA. Utakumbuka enzi za PM Melez Zenawi akiwa Waziri Mkuu wa Ethiopia. US walikua wanatumia Jeshi la Ethiopia kuwachapa Wasomali na Wa Eritria.

Sasa Waeritria hawataki Watigray watawale Ethiopia kwa hofu zama za Marekani kuwapiganisha zitarudi.
 
Nyongeza ya 1.

Baada ya Watigray kuanzisha vita Hadi nje ya Jimbo lao. Jeshi la Ethiopia lili pooza hasa kwa kua makamanda wengi walikua Watigray. Ndipo Abiy PM akaomba msaada wa Eritria kuaidia kuzuia Kasi ya Watigray. Ila Waeritria wana chuki sana na Watrigay kwa mauaji ya miaka mingi waliofanya enzi wakitawala Ethiopia.

Hili lilisababisha mauaji makubwa Tigray. Baada ya kelele za kimataifa Eritria ikandoka. Kwa hiyo vacuum chap chap TPLF ikatwaa maeneo mengi.

Kosa wa likafanywa na Watigray ni kuvamia Jimbo la Wahmara na kutishia kutwa adidas Ababa. Hapa likaamsha kabila la WaAhmara na mengine yakaungana KIKAMILIFU.

Abiy PM Sasa akaingia vitani kifua mbele ana wapiganaji royal.
 
Wanajeshi wa Ethiopia wakiwa katikati ya miji ilikombilewa
IMG_20211128_195119.jpg


Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Jeshi la Serikali limeafanikiwa kukomboa Jimbo zima la Afar na miji yake. Chefra, Kisingita Libella na nk.

Ikumbukwe Waasi wa TDF walifanikiwa kuteka majimbo mawili zaidi. Afar na Ahmara.
Mapigano yanaendelea huko aAhmara baada ya hapo Ahmara vita itamalizikia Jimbo la Tigray.

Inshor Watigray wana Historia ya kutopenda mapigano yafanyikie kwenye Jimbo lao. Matarajio ni wakizidiwa Ahamara tu watakimbilia maporini kujificha. Hawataki vita ipiganiwe Tigray kwa kuhofia uhalibifu.



Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom