Ethiopia: Shule zafungwa ili Wanafunzi wasaidie uvunaji wa Chakula

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Wizara ya Elimu ya Ethiopia imetangaza kufungwa kwa shule zote za sekondari kwa muda mfupi, ili kuwaruhusu wanafunzi kusaidia katika kuvuna chakula katika mashamba ya Waethiopia wanaopigana vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa TPLF.

Shirika la habari lenye uhusiano na serikali ya Ethiopia, FANA, limeripoti kwamba waziri wa elimu Berhanu Nega amesema kwamba shule zitafungwa kwa muda wa wiki moja.

Serikali ilisema Jumatatu kwamba zaidi ya wanafunzi milioni 1.2 hawapo shule kutokana na mapigano yanayoendelea kaskazini mwa nchi hiyo.

Mapigano yameharibu mamia ya shule.

Serikali ilitangaza hali ya dharura ya miezi sita kuanzia mwezi Novemba ili kukabiliana na wapiganaji wa Tigray wenye lengo la kuingia mji mkuu wa Addis Ababa na kuuangusha utawala wa waziri mkuu Abiy Ahmed.
 
Hata sie sec tulikuwa tuna off shule nzima kuvuna na kupukuchua mahindi.. kwenye mashamba ya shule tuliyolima wenyewe and then next day kama bado kuisha tena after that inakuwa ukifanya kosa adhabu ni kupukuchua mahindi tu.. tulipata experience sana tuliokuwa hatujawahi ishi maisha ya familia za wakulima... ni tabu nyingi sana
 
Back
Top Bottom