Ethiopia: Facebook yafuta ujumbe wa Waziri Mkuu uliowataka wananchi "kuwazika" TPLF

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mtandao wa Kijamii wa Facebook umefuta Ujumbe wa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed uliowahimiza Wananchi kujipanga na kuandamana kwa njia isiyovunja Sheria wakiwa na silaha ili kuzuia Waasi wa TPLF

Facebook imesema imeondoa Ujumbe huo kwasababu unakiuka Sera yake kuhusu kuchochea ghasia. TPLF ambayo hivi karibuni imethibiti Miji muhimu imekuwa ikipambana na Vikosi vya Serikali kwa mwaka mmoja

========

Facebook has removed a post from Ethiopia's prime minister for violating its policies against inciting violence.

On Sunday, Abiy Ahmed called on citizens take up arms to block the advance of the rebel Tigray People's Liberation Front (TPLF).

The TPLF has fought a year-long campaign against government forces, capturing key towns in recent days.

Facebook has been criticised for failing to do more to stop its platform being used to incite violence.

In the post, Mr Abiy said that the rebel advance was "pushing the country to its demise," and he urged citizens to "organise and march through [any] legal manner with every weapon and power... to prevent, reverse and bury the terrorist TPLF".

A spokesperson for Facebook, whose parent company recently rebranded to Meta, told the BBC: "We were made aware of a post by Ethiopia's Prime Minister and removed this for violating our policies against inciting and supporting violence.

"At Meta, we remove content from individuals or organizations that violates our Community Standards, no matter who they are."

In a massive leak of documents last month it was revealed that Facebook had been warned that its platform was being used by armed groups in Ethiopia to incite violence against ethnic minorities.

Speaking to a US Senate hearing in October, whistleblower Frances Haugen said that the company was "literally fanning ethnic violence" in conflict zones such as Ethiopia due to its failure to properly police its services outside of the US.

Thousands of people have been killed by the conflict in Ethiopia, millions more have been displaced and hundreds of thousands are facing famine conditions, according to the UN.

The war broke out on 4 November last year, when Ethiopian Prime Minister Abiy ordered a military offensive against regional forces in Tigray.

He claimed that his government did so in response to an attack on a military base that housed government troops.

The TPLF has been designated a terrorist organisation, while it says it is Tigray's legitimate government.

Source: BBC
 
Waziri mkuu kibri kitamponza. Aliamua kushugulikia tatizo kijeshi. Sasa haooo wanakuja capital city. Mwisho wa kibri ni anguko la aibu. Huu ni mfano mdogo wengine pia wajifunze. Ethiopia inaendeshwa kwa propaganda kuonesha kuwa mambo ni safi. Lkn ukiachilia mbali uasi wa Tigray...tizama vile vijana wanaikimbia nchi yao kila kukicha hali mbaya ya uchumi hakuna ajira. Wahamiaji haramu toka ethiopia ni wengi sana nchini hapa nchini. This means something is going wrong in Addis Ababa
 
Angelikiwa wewe ungefanyaje yani watu wanajitangazia uhuru wao wanavamia kambi za jeshi. Assume mwanza leo inasema si party ya tz inavamia kambi za jeshi na kushikilia silaha na wewe ni raisi ni hatua gani utachukua?
 
Abiy kaapa kulinda katiba na mshikamano wa kitaifa. Ni heri nife nikipigania hilo kuliko kukaa kikekike nikirembua. Ethiopia si ni kama Nigeria, assume Nigeria isingepambana na Biafra leo hii wangeanza wale kujitenga na baadae makabila mengine yakajitenga na sasa tungekuwa na nchi tatu au nne zinazotokana na Nigeria.

Ethiopia ni ngumu, Oromia wanajitenga na Tigray wanajitenga na Eritrea walishajitenga. Sasa Abiy angefayaje wakati nchi ndio alijaribu kuondoa ukabila ila makabila yenyewe hayataki. Wangekuwa hawa walalamikaji hapa Tanga inajitenga wangezubaa, Mtwara nayo ingeona kumbe easy tu ikajitenga, Kigoma nayo ikajitenga. Miaka 30 baadae hakuna nchi
 
Yani ukabila ndo unewajaa na wanaenda kumwondoa ili warudi madarakani waendelee kuwakandamiza wengine.
 
Angelikiwa wewe ungefanyaje yani watu wanajitangazia uhuru wao wanavamia kambi za jeshi. Assume mwanza leo inasema si party ya tz inavamia kambi za jeshi na kushikilia silaha na wewe ni raisi ni hatua gani utachukua?
Shida inayoisumbua Ethiopia ni ukabila uliopitiliza, Ahmed alikuja vizuri kuondoa ukilitimba wa watu wa Tigray lakini yamemshinda kwa sabababu alichagua njia mbaya (mabavu) kutatua tatizo hilo. Pole kwa watu wa Ethiopia wanaotaabika kwa sasa.
 
Hakukuwa na njia nyingine. Watu wamebeba silaha unataka suruhu ya nini? Mbona hamfikirii, Iddi Amin alipotuvamia ungetaka suruhu gani ya mazungumzo
 
Mkuu Unahabari kuwa at any time abiy atakuwa sio prime minister tena?,tigray Ni watu hatari Sana!! Wale Ni sawa na kula na kipofu
 
Najua hilo na nishasema hata ingekuwa mimi ningefanya kama alivyofanya yeye. Huwezi vamiwa ukajificha uvunguni, wewe hufai kuwa kiongozi
Abiy alikosea tangu mwanzo,..akijua hawa Watigray wamekuwepo madarakani miongo mitatu lazima udeal nao kidiplomasia zaidi kuliko mabavu.

Walipoamua kuitisha uchaguzi kipindi cha Covid-19 angeongea nao tu maana hata yeye muda wake kikatiba ulikuwa umefika mwisho ila akasogeza mbele uchaguzi kisa Covid-19, kuwavamia akishirikiana na Eritrea ilikuwa kosa.
 
Hakukuwa na option zaidi. Tangu alipochaguliwa akaunda umoja wa kitaifa kuondoa ukabila walikataa wao wenyewe, baada ya kupokea Nobel. Walikuwa wanatafuta sababu tu na na wakasingizia yeye kusitisha uchaguzi kufanya uchaguzi wao. Isitoshe aliwavamia mapema kuharibu silaha zao maana walikuwa kwenye maandalizi ya kushambulia. By any means hakuwa na solution ya haraka zaidi ya hiyo

Ile WW2 UK walianza na sera kama hizi mpaka Hitler alipoivamia Poland. Ndipo ilibidi PM ajiuzuru akaja Winston Churchill. Hata Nigeria wasingepigana na Biafra wakasubiri mazungumzo yangekuwa mambo mengine. Hata USA wasingepigana vita wakasubiri mazungumzo tungekuwa na nchi mbili pale. Kuna wakati mashambulizi hayaepukiki, kushinda au kushindwa ni matokeo
 
Ila kitendo cha kushirikiana na Eritrea kulishambulia jimbo lake la Tigray lilikuwa ni usaliti mkubwa kwa mamlaka yake.
 
Hakuna usaliti katika kupambana na waasi. Ni sawa na kusema serikali ya Msumbiji ilifanya usaliti kwa mamlaka yake ilipokaribisha majeshi ya Rwanda kupigana na magaidi wa jimbo la Cabo Delgado. Au kusema Somalia ilifanya usaliti kukaribisha Kenya kupambana na Al Shabaab.

Watu vitani hutafuta allies wala sio kulala kwenye mawazo ya usaliti. Hayo Tigray wenyewe binafsi wameungana na Oromia kupigana na Federal government, na cha ajabu ni hivi baada ya vita wakishakuwa huru Tigray na Oromia watapigana. Sababu za wazi za kupigana zipo kabisa, ni ardhi.

Hata hii Eritrea Meles Zenawi alipoiangusha serikali ya Derg ya kina Mengistu Haile Mariam, Isaias Afwerki aliyeshirikiana na Zenawi aliitisha uchaguzi ghafla wa jimbo la Eritrea kujitenga. Imagine Zenawi mwenyewe alikuwa Eritrea kipindi uchaguzi unafanyika. Na baadae walipigana kugombea eneo la mpakani. Ambalo eneo hilo lilitoka Tigray na ikaamuliwa ni la Eritrea. Tigray ikiwa huru inaweza lidai ndio maana unaona Abey Ahmed hana wasiwasi na Eritrea ila Eritrea ina wasiwasi na TPDF
 
Waziri mkuu kibri kitamponza. Aliamua kushugulikia tatizo kijeshi. Sasa haooo wanakuja capital city. Mwisho wa kibri ni anguko la aibu. Huu ni mfano mdogo wengine pia wajifunze. Ethiopia inaendeshwa kwa propaganda kuonesha kuwa mambo ni safi. Lkn ukiachilia mbali uasi wa Tigray...tizama vile vijana wanaikimbia nchi yao kila kukicha hali mbaya ya uchumi hakuna ajira. Wahamiaji haramu toka ethiopia ni wengi sana nchini hapa nchini. This means something is going wrong in Addis Ababa
Wewe hujui lolote kuhusiana na Ethiopia..hebu niambie kosa lake ni nini? Abey ndo waziri mkuu wa kwanza kwa zaidi ya miaka 30 ameleta demokrasia nchini mwake. Labda kama wewe ni mfuasi wa sera za Magu za udikteta
 
Wewe lofa Magu ameingiaje hapa? Nawewe Ni Nani humu jf Hadi unipangie namna ya kufikiri na kuwaza
 
Hakuna usaliti katika kupambana na waasi. Ni sawa na kusema serikali ya Msumbiji ilifanya usaliti kwa mamlaka yake ilipokaribisha majeshi ya Rwanda kupigana na magaidi wa jimbo la Cabo Delgado. Au kusema Somalia ilifanya usaliti kukaribisha Kenya kupambana na Al Shabaab.

Watu vitani hutafuta allies wala sio kulala kwenye mawazo ya usaliti. Hayo Tigray wenyewe binafsi wameungana na Oromia kupigana na Federal government, na cha ajabu ni hivi baada ya vita wakishakuwa huru Tigray na Oromia watapigana. Sababu za wazi za kupigana zipo kabisa, ni ardhi.

Hata hii Eritrea Meles Zenawi alipoiangusha serikali ya Derg ya kina Mengistu Haile Mariam, Isaias Afwerki aliyeshirikiana na Zenawi aliitisha uchaguzi ghafla wa jimbo la Eritrea kujitenga. Imagine Zenawi mwenyewe alikuwa Eritrea kipindi uchaguzi unafanyika. Na baadae walipigana kugombea eneo la mpakani. Ambalo eneo hilo lilitoka Tigray na ikaamuliwa ni la Eritrea. Tigray ikiwa huru inaweza lidai ndio maana unaona Abey Ahmed hana wasiwasi na Eritrea ila Eritrea ina wasiwasi na TPDF
Mkuu mzozo wa Kenya na Alshabaab au Msumbiji na Isis sio Vita vya wenyewe kwa wenyewe kama Ethiopia.

Huko Ethiopia ni vya wenyewe kwa wenyewe lakini Abiy amealika taifa hasimu ili kupiga raia wake waasi, isitoshe jeshi la Eritrea limeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita huko Tigray , hayo ni makosa makubwa kwa Abiy.
 
Jamaa analinganisha vitu ambavyo havifanani kabisaaa.
 
Mkuu mzozo wa Kenya na Alshabaab au Msumbiji na Isis sio Vita vya wenyewe kwa wenyewe kama Ethiopia.

Huko Ethiopia ni vya wenyewe kwa wenyewe lakini Abiy amealika taifa hasimu ili kupiga raia wake waasi, isitoshe jeshi la Eritrea limeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita huko Tigray , hayo ni makosa makubwa kwa Abiy.
No sio makosa shida ni vyanzo vya habari unavyosikiliza au kusoma.

Kabla Eritrea hawajaingia Tigray kupambana na hao waasi, TPLF walishambulia mara 17 Eritrea kwa kutumia maroketi waliyoiba kwenye kambi za majeshi ya serikali. Walichofanya TPLF ni uasi kwa seikali kuu ya Ethiopia na ugaidi kwa seikali ya Eritrea.

Eritrea na Ethiopia wana mahusiano mazuri kwahiyo hakukuwa na sababu ya Ethiopia kuwakataza Eritrea kupambana na adui wao wote.

Marekani ina ushirika wa muda mrefu na TPLF ndomaana hata vyombo vyao vya habari vipo biased, havielezi mauaji pamoja na uporaji wa maeneo unaofanywa na TPLF wala chanzo cha mgogoro nini. Ni mara ngapi uliwahi kusikia Mai Kadra massacre ikiripotiwa na BBC au CNN.

Baada tu ya jeshi la serikali kuingia Tigray, Marekani na washirika wake wakaomba serikali ya Ethiopia itoe jeshi lake Tigray kwa sababu hali ya usalama inazidi kuwa mbaya lakini hakujawahi kuwa na kauli nzito juu ya uasi wa TPLF kwa serikali.

Kitu kimoja ninachomlaum Abiy ni uamuzi wake wa kutoa jeshi Tigray baada ya shinikizo huku akiwa hana plan yoyote ya kuwapunguza kasi TPLF.

Mfano wa Kenya na Alshabaab aliotoa jamaa hapo juu ukilinganisha na mazingira ya Eritrea na TPLF upo sawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom