Et tu Brute? Wajueni Ma-Yuda Iskariote wenu!

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Ewe Mtanzania,

Chukua muda utafakari unachokisoma hapa, chambua kwa undani ndani ya roho yako ujilize machungu unayoyapata kwa KUSALITIWA na hawa wafuatao ambao ni wawakilishi wako katika Serikali.

Uliwachagua kwa kuwapigia kura na kuwapa dhamana wawe Wabunge na Wawakilishi wako katika kujenga Serikali.

Jee utendaji kazi zao na kauli wanazotoa ni kweli zinakuwakilisha wewe kama Mwananchi na kukusaidia wewe Mwenye Nchi? Au kauli na matendo yao ni kujinufaisha na kulinda maslahi ya Chama chao CCM?

Jiulize, mwaka 2010, uko tayari kumuongezea huyu Msaliti wa maslahi yako na familia yako miaka mingine mitano ya kukulaghai kuwa yeye ni Mbunge wako?

1. Anna Abdallah
2. Abdalla Kigoda
3. Peter Msola
4. Peter Serukamba
5. Andrew Chenge
6. Mustafa Mkullo
7. Hawa Ghasia
8. Bernard Membe
9. Maua Daftari
10. Mohamed Seif Khatib
11. Nizar Karamagi
12. Ibrahimu Msabaha
13. Charles Keenja
14. Emmanuel Nchimbi
15. Edward Lowassa
16. Mary Nagu
17. Milton Mahanga
18. Rostam Aziz

........add to the list
 
19. Basil Pesambili Mramba
20. Nimrodi Mkono (mrefu)
21. Muhidhiri Muhidhiri
 
Benjamini Wiliiamu Mkapa, Daniel Yona , Kapuya na Helcoppter Mbovu za jeshi na kujipatia Machimbo ya merereani, na kutoa bahasha za pesa kwa waandishi alipokuwa elimu, Na tenda za NSSF alipokuwa wizara ya Kazi
 
Rev,
nadhani ungefanya kama alivyofanya August ,kwanini usituambie ni namna gani na ni kwa
vipi wametusaliti?

kuna baadhi yao hapo juu kwenye listi yako matendo yao tunayajua ye wale tusiowajua huoni kuwa tutakuwa tunahukumu bila kusoma shitaka?
Ni maoni yangu tu
 
Benjamini Williamu mkapa
Daniel Yona
Kapuya

27. Prof Jumanne Maghembe

Na ufisadi wake aliyooufanya (pamoja na tenda karibia zote za Uvuvi, uwindaji na kampuni zake feki alizoanzisha) Wizara ya Utalii ndani ya miezi 4 baada ya kukabidhiwa Wizara.
 
Benjamini Wiliiamu Mkapa, Daniel Yona , Kapuya na Helcoppter Mbovu za jeshi na kujipatia Machimbo ya merereani, na kutoa bahasha za pesa kwa waandishi alipokuwa elimu, Na tenda za NSSF alipokuwa wizara ya Kazi

Mkubwa, kwa mada hii BEN unamuonea maana yeye si mbunge na wala haji kugombea mwaka 2010. Kapuya sawa maana Mungu Mkubwa bwana wakati anapata Ajali na jamaa wakaiba Compressor kwenye Mgodi wake. Nani angejua kama jamaa anamgodi bila ya kuwa hivyo.
 
Ewe Mtanzania,

Chukua muda utafakari unachokisoma hapa, chambua kwa undani ndani ya roho yako ujilize machungu unayoyapata kwa KUSALITIWA na hawa wafuatao ambao ni wawakilishi wako katika Serikali.

Uliwachagua kwa kuwapigia kura na kuwapa dhamana wawe Wabunge na Wawakilishi wako katika kujenga Serikali.

Jee utendaji kazi zao na kauli wanazotoa ni kweli zinakuwakilisha wewe kama Mwananchi na kukusaidia wewe Mwenye Nchi? Au kauli na matendo yao ni kujinufaisha na kulinda maslahi ya Chama chao CCM?

Jiulize, mwaka 2010, uko tayari kumuongezea huyu Msaliti wa maslahi yako na familia yako miaka mingine mitano ya kukulaghai kuwa yeye ni Mbunge wako?

1. Anna Abdallah
2. Abdalla Kigoda
3. Peter Msola
4. Peter Serukamba
5. Andrew Chenge
6. Mustafa Mkullo
7. Hawa Ghasia
8. Bernard Membe
9. Maua Daftari
10. Mohamed Seif Khatib
11. Nizar Karamagi
12. Ibrahimu Msabaha
13. Charles Keenja
14. Emmanuel Nchimbi
15. Edward Lowassa
16. Mary Nagu
17. Milton Mahanga
18. Rostam Aziz

........add to the list

Reverend,

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.

Vitu kama hivi inabidi viwekwe kwenye vipeperushi na kusambazwa tanzania nzima kwani ndugu zetu wa kiteto na wengine waliopo vijijini hawajabahatika kupata wasaa wa kuona maneno mazuri kama haya.

Vipeperushi vitakuwa more effective, na tuanze sasa kuvituma huko vijijini. Kama ndugu zetu waliona kwamba kufanya kampeni kwa kutumia helikopta ni more efficient way ya kuwafikia watu wa vijijini basi sioni tatizo lolote wao kukodi ndege ndogo itakayotumika kuvimwaga vipeperushi huko vijijini. I tell you, ndugu zetu wa vijijini wakiona ndege inaruka chinichini na kumwaga hivyo vipeperushi kitendo icho kitawafanya wakimbilie ivyo vijikaratasi ili kuweza pata ujumbe.
 
Benjamini Wiliiamu Mkapa, Daniel Yona , Kapuya na Helcoppter Mbovu za jeshi na kujipatia Machimbo ya merereani, na kutoa bahasha za pesa kwa waandishi alipokuwa elimu, Na tenda za NSSF alipokuwa wizara ya Kazi

Mkapa na Yona si wabunge.
 
Rev,
nadhani ungefanya kama alivyofanya August ,kwanini usituambie ni namna gani na ni kwa
vipi wametusaliti?

kuna baadhi yao hapo juu kwenye listi yako matendo yao tunayajua ye wale tusiowajua huoni kuwa tutakuwa tunahukumu bila kusoma shitaka?
Ni maoni yangu tu

Mchelea Mwana,

Waliotajwa ni wabunge, wawakilishi wa wananchi ambao kauli na utendaji wao unaonyesha wazi kuwa si kwa manufaa ya Wananchi wa majimbo yao ya uchaguzi, bali ni kwa matumbo yao na chama Chao CCM.

Wote aliotajwa hapo juu, kwa namna moja au nyingine wamechangia kudorora kwa ustawi wa Mtanzania, ili kulinda maslahi ya kikundi kidogo cha watu kwa mgongo wa Chama au Serikali.
 
FMES,

Kwenye gazeti la majira leo, kuna habari kuhusiana na mgawanyiko wa Wabunge wa CCM.

Kuna pande tatu kuu.

Upande wa kwanza ni wale ambao wanapiga vita hujuma na kutaka kusafisha chama.

Upande wa pili ni ule unolinda hujuma na ufisadi na kuzuia mazungumzo ya wazi kati yao CCM kuhusiana na hujuma na ufisadi.

Kundi la tatu, ni la wale waoga wasiokuwa tayari kujitangaza misimamo yao kwa woga wa kutokata kukosa marafiki au kukorofisha mtu.

Hili kundi la tatu ambalo ni kubwa, ni baya sana kwa Taifa. Watu wasiokuwa na msimamo hawafai hata siku moja kutuwakilisha Serikalini.

Kundi hili la tatu na lile la pili, ndio sasa inabidi tuanze kuwafanyai kazi na kuhakikisha hawaendelei kuvuna haki na kura zetu na tuaianza vita hii kupinga ugoigoi wa Wabunge wetu kuanzia sasa tukielekea kwenye Uchaguzi 2010.
 
Ongezeni Wilson Masilingi na wengine ambao wameongea Upupu tangu Bunge lianze.

Hawa ni lazima majimbo yao Upinzani uweke nguvu na kuyachukua.

Simple way, associate ufisadi wao na umasikini wa Wananchi!
 
Katika CCM ya sasa ukichunguza kwa MAKINI kabisa HAKUNA anayepaswa kubaki! Wasafi walioko CCM wako nje ya UONGOZI kama akina Waryoba, Kaduma, SAS, Jenerali, Profesa Mmari,...
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom