Esther Wassira for Presidency 2015...

Nilishawahi kusema hapa, waliokuwa katikati ya jangwa la Sahara hata chemchemi yenye maji ya vumbi wataisifia tu.

Sio kwa sababu maji ni mazuri sana, bali kwa sababu hamna matumaini zaidi.

Tukiendelea na mifano ya maji.Mfa maji heshi kutapatapa, atataka kushikilia hata unywele ueleao kwa matumaini kwamba utamsaidia.

Sasa huyu binti ndo kwanza kamaliza shule hata political compass hajaipata vizuri, let alone kufikisha umri wa kugombea urais, hajapata hata ubunge wa viti maalum for half a term tu.

Mshaanza kumsema urais. What's next?
 
She is gud. Bt anashindwa kutofautisha kati ya hoja ya nguvu na nguvu ya hoja.
 
Mtu yoyote akifanya vizuri kuna slogan tunatupia
'For urais'
Duh nacomment huku RVP wawawawa 3 !
 
Nilishawahi kusema hapa, waliokuwa katikati ya jangwa la Sahara hata chemchemi yenye maji ya vumbi wataisifia tu.

Sio kwa sababu maji ni mazuri sana, bali kwa sababu hamna matumaini zaidi.

Mfa maji heshi kutapatapa, atataka kushikilia hata unywele ueleao kwa matumaini kwamba utamsaidia.

Sasa huyu binti ndo kwanza kamaliza shule hata political compass hajaipata vizuri, let alone kufikisha umri wa kugombea urais, hajapata hata ubunge wa viti maalum for half a term tu.

Mshaanza kumsema urais. What's next?

Hii ndiyo maana ya forum mpenzi.
Siyo lazima useme wewe tu au si lazima mawazo yote yawe chanya.
 
Moony Ni kweli.

Ni kweli pia hilo halimaanishi niachie upuuzi utambae hapa kwa sababu tu kila mtu ana haki ya kujieleza. Forum inatoa uwanja wa kupambanisha mawazo, ili yenye mshiko yashinde. Na ndiyo maana nakandamiza msimamo wangu, ili uwakilishwe vilivyo.

I mean let's say I am a CHADEMA fan. And we are not exactly talking about 2015, but sometime down the line so the age factor is moot. Why this Wassira lady, someone with no track record by the way, as opposed to a John Mnyika? One does not have to look outside of CHADEMA to see that her inexperience is screaming out loud.

The presidency is not something to gamble with. Tumeona hata baada ya Mkapa kumuweka Kikwete kwenye matayarisho kwa miaka 10 Foreign Affairs, on top of everything else, the Kikwete administration is clumsy to say the least.

Mshindanisheni ubunge huko tuone performance yake bungeni, kama atashinda.
 
Last edited by a moderator:
Huu ni upuuzi yaani sasa mtu akitoka na rhetoric hata hatujaona utendaji wake basi tunalipuka apewe Urais!! Hivi kwanza tunahitaji marais wangapi na hiyo nafasi imetangazwa lini?

Tena ni bora tuwe macho kuwa, si kila apigae kelele na kutokwa na povu kuwa ndicho kigezo cha kuwa anajali maslahi ya wananchi. Hata wezi, matapeli na wasio na moyo wa kuendeleza nchi yetu nao wanafanya rehearsal za nguvu za kusimama majukwaani kuongoea kwa nguvu bila kupumua na kabla ya kuanza kuongea mengi, watasema Mafisadi wote wanyongwe !!! nchi hii ni yetu sote !!! n.k Tuliobaki tunapiga makofi hata bila kumchunguza mzungumzaji ni mtu wa aina gani na ukweli anasimamia nini na kabla ya leo huko nyuma alisimamia nini.

Binti anaweza kuwa ana sifa fulani lakini ni kichekesho kuwa kasimama sijui wapi na kuongea kesho tunasema awe Rais. Mbona mmeurahisi Urais kiasi hiki Watanzania?

Zamani matapeli na wezi walikuwa ni watu wanaovaa vibaya; siku hizi matapeli na wezi wanavunja suti na briefcase mikononi. Kama bado unafikiri kuwa Viongozi wanaofaa ni wale wanaoongea kwa sauti za juu, hisia,machozi na bila kituo majukwaani basi hata vijana wa OK wanafaa kuliko yeyote. Fikiri mfano huu uchukue hatua!
 
Wana jamvi, salaam.

Jana katika kongamano la miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika Chuo kikuu Dar. Mwanaharakati Ester Wassira aliahidi kuweka hotuba yake humu jamvini na kwenye mitandao yote ya kijamii.

Ki ukweli ilinigusa sana nimeitafuta niisome yote sijaipata takriban saa 18 sasa. Mwenye Idea au hata Ester mwenyewe aiweke hapa basi kama alivyo ahidi au kama ipo kwenye majukwaa mengine humu naomba kuelekezwa.

Nawasilisha.
 
Bado anajipanga vizuri maana jana alikuwa mkali sana. Huenda ukali ule wa jana umemuongezea presha yule mzee wake aliyewakana kuwa si watoto wake maana akiangalia Chadema yuko Ester na CCM yuko Ester na wote hawa wamemshika pabaya.
 
Back
Top Bottom