Esther Wasira: Waliofilisi Mashirika ya Umma na Kujiuzia nyumba za umma kukiona 2015: Angalia Ch 10

matasha

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
378
400
Katika kipindi cha Je, Tutafika kitakachorushwa leo jumamosi saa nne usiku Channel 10, Esther Wasira amelonga kuwa wale waliofilisi mashirika ya umma na kujiuzia nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa watapelekwa mbele ya sheria mara tu atakapoapishwa Nyerere mpya kama rais na Sokoine mpya kama Waziri Mkuu katika serikali mpya itakayoundwa na CHADEMA 2015. Usikose kufuatilia kipindi hiki ambapo mwanaharakati huyu machachari pamoja na wana panel wengine wameelezea mambo mengi kuhusu hatima ya taifa letu kwa miaka 50 ijayo.
 
Esther Wassira, ni nani kwenye nchi? kaishatoa mchango gani katika ujenzi wa taifa la Tanzania?
 
Unamaanisha nini? Maana hata mchango wa mawazo ni mchango, tena mawazo ndio yanaendesha nchi. Kwani hao viongozi wa CCM wametoa mchango gani zaidi ya kufilisi nchi? Chukulia mtu kama maji marefu, ameifanyia nini nchi hii au ana mawazo gani kuhusu nchi hii? In my view, Esther is a young, brilliant and strong politician who is out to defend the rights of the voiceless!
 
esther wassira, ni nani kwenye nchi? Kaishatoa mchango gani katika ujenzi wa taifa la tanzania?

mr dahaifu wako ametoa mchango gani katika taifa hili???
Usitumie makalio kufikiri wewe...!!
 
Boss wako mpayukaji Nape ana mchango gani kwenye taifa letu?
Unasema kweli, mtu kama Nape ni mzigo kwa taifa, kazi kupiga domo tu kwa mambo ambayo hayana manufaa. Ni afadhali Esther anazungumza mambo yenye kuamsha fikra na ana mvuto
 
Asante kwa taarifa mkuu.wacha nape aendelee kudai kadi zilizo Xpire.sisi tendelee na ukombozi.
 
Wewe Pol Pot umechangia nini katika nchi hii?

Esther Wassira amejiunga na CHADEMA na vijana wengine wazalendo, jasiri na wenye uchungu na adha wanayopata Watanzania wanyonge.

Tumsikilize na tumuulize maswali atakapokuwa Channel 10 leo.
 
Katika kipindi cha Je, Tutafika kitakachorushwa leo jumamosi saa nne usiku Channel 10, Esther Wasira amelonga kuwa wale waliofilisi mashirika ya umma na kujiuzia nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa watapelekwa mbele ya sheria mara tu atakapoapishwa Nyerere mpya kama rais na Sokoine mpya kama Waziri Mkuu katika serikali mpya itakayoundwa na CHADEMA 2015. Usikose kufuatilia kipindi hiki ambapo mwanaharakati huyu machachari pamoja na wana panel wengine wameelezea mambo mengi kuhusu hatima ya taifa letu kwa miaka 50 ijayo.
matasha hakuna mtu aliyefilisi shiriza la umma zaidi ya sera za wakati za "Full employment". Ilikuwa vijana wakimaliza vyuo wanapangiwa makampuni ya kwenda kufanya kazi bila kuangaliamahitaji ya kampuni; hii ilipelekea kuwa na watumishi wengi kuliko uwezo wa kampuni na kufanya mashirika yajiendeshe kwa hasara
 
Last edited by a moderator:
Sijui kwa nini wafuasi wa Cdm wanakuwa na akili za kushikiwa sasa huyu mwanamziki wa bongo freva naye eti anatisha watu.:crazy:
 
Esther Wassira, ni nani kwenye nchi? kaishatoa mchango gani katika ujenzi wa taifa la Tanzania?
Huyo ni mwananchi mzalendo wa Tanzania. Mchango wake katika ujenzi wa Taifa la Tanzania upo katika hayo maneno yake...au wewe huuoni?
 
matasha hakuna mtu aliyefilisi shiriza la umma zaidi ya sera za wakati za "Full employment". Ilikuwa vijana wakimaliza vyuo wanapangiwa makampuni ya kwenda kufanya kazi bila kuangaliamahitaji ya kampuni; hii ilipelekea kuwa na watumishi wengi kuliko uwezo wa kampuni na kufanya mashirika yajiendeshe kwa hasara
Kwa hiyo unataka kusema shirika kama ATC watu wanakula hadi wanakomba mboga, TTCL na mengine bado ni kwa sababu uliyoitoa? 2015 lazima kieleweke
 
Sijui kwa nini wafuasi wa Cdm wanakuwa na akili za kushikiwa sasa huyu mwanamziki wa bongo freva naye eti anatisha watu.:crazy:
Hahahaaaaaaaaaaaaaaa. Kama unadhani anatishia subiri 2015, Chadema hawatanii!
 
Wewe Pol Pot umechangia nini katika nchi hii?

Esther Wassira amejiunga na CHADEMA na vijana wengine wazalendo, jasiri na wenye uchungu na adha wanayopata Watanzania wanyonge.

Tumsikilize na tumuulize maswali atakapokuwa Channel 10 leo.
Mie nalipa kodi serikali kuu unadhani mie kama nyie wafuasi wa Cdm mnashinda vijiweni mnasubiri eti Cdm wachukuwe nchi mpewe kazi serikalini.
 
Huyu anafaa kwenye mambo ya urembo siyo siasa.
3.jpg
 
Back
Top Bottom