Katika kipindi cha Je, Tutafika kitakachorushwa leo jumamosi saa nne usiku Channel 10, Esther Wasira amelonga kuwa wale waliofilisi mashirika ya umma na kujiuzia nyumba za serikali kwa bei ya kutupwa watapelekwa mbele ya sheria mara tu atakapoapishwa Nyerere mpya kama rais na Sokoine mpya kama Waziri Mkuu katika serikali mpya itakayoundwa na CHADEMA 2015. Usikose kufuatilia kipindi hiki ambapo mwanaharakati huyu machachari pamoja na wana panel wengine wameelezea mambo mengi kuhusu hatima ya taifa letu kwa miaka 50 ijayo.