Esther Matiko: Umeme Tanzania ni Ghali sana, Kagera elfu 10 unapata unit 80 kutoka Uganda badala ya 28

Inawezekana hizo ni tarrifs kwa watumiaji wa kiwango cha chini wanaotambulika huko kwao Uganda, hata hapa kwetu utaratibu huo upo kwa waliojiandikisha.

Ila Tanesco kuhodhi uzalishaji na usambazaji umeme inaweza kuwa chanzo hapa kwetu kwa bei ya umeme kuwa juu kwa watumiaji wengi ambao hawajajiandikisha kama wale wanaotumia kiwango cha chini.
 
Wametajwa wakazi wa Kagera wanaotumia umeme wa Uganda soma vizuri kijana
aisee, wewe ndio usome vizuri

Alichosema wakazi wa kagera,mkoa ambao upo Tanzania, wanatumia umeme toka Uganda, na UNIT 80 wanauzia kwa Tsh. 10,000/= ilhali iyo elfu kumi kwa Bei ya shirika la umeme la Tanzania unapata Unit 28.1 tu

Sasa nini ujaelewa hapo kilichomaanishwa boss??;

Ni kwamba Tanzania umeme tunauziwa ghali sana chief
 
Hata mimi wakati nikiwa naishi mwenyewe 10000 nilipata init 80 ila matumizi yalipoongezeka nilitolewa kwenye ile tariff. Kuna kiwango unachotakiwa utumie kwa mwezi ili upate unit 80 kwa sh. 10000
 
Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha CHADEMA, Esther Matiko amelalamikia gharama kubwa za umeme Tanzania huku akitolea mfano wakazi wanaoishi Kagera na kutumia umeme kutoka Uganda wanalipia 10,000 na kupata unit 80 ilihali kwa fedha hiyo Tanzania inanunua unit 28 pekee...
Hapo ndo utagundua hata mashirika ya umma ni wezi, wakubwa, na sijui tutakuja kutokaje hapa tulipo ili hali Tnesco ina wateja wa kutosha , Biashara yoyote ili ikuwe na kustawa inahitaji wateja.

Tanesco ina wateja Tz nzima tena wanapitiliza . sasa inakuwaje mara tuambiwe shirika linajiendesha kwa hasara ili hali wateja ni wengi sana. Tunahitaji watu sahihi wa kuiendesha TANESCO
 
aisee, wewe ndio usome vizuri

Alichosema wakazi wa kagera,mkoa ambao upo Tanzania, wanatumia umeme toka Uganda, na UNIT 80 wanauzia kwa Tsh. 10,000/= ilhali iyo elfu kumi kwa Bei ya shirika la umeme la Tanzania unapata Unit 28....
Ulichoandika hapa na mm ndicho nilielewa mwanzoni.
 
aisee, wewe ndio usome vizuri

Alichosema wakazi wa kagera,mkoa ambao upo Tanzania, wanatumia umeme toka Uganda, na UNIT 80 wanauzia kwa Tsh. 10,000/= ilhali iyo elfu kumi kwa Bei ya shirika la umeme la Tanzania unapata Unit 28....
Hata huko Tarime kwao matiko watumiaji wengi (watumiaji wasiozidi unit 75 kwa mwezi) wanalipa sh 100 kwa unit 1.
 
Tanesco ina wateja Tz nzima tena wanapitiliza . sasa inakuwaje mara tuambiwe shirika linajiendesha kwa hasara ili hali wateja ni wengi sana. Tunahitaji watu sahihi wa kuiendesha TANESCO
TANESCO ni moja ya mashirika yaliyohujumiwa sana. Kama wangeachwa wajiendeshe bila mikono ya wanasiasa wangejiendesha kwa ufanisi sana na kutengeneza faida ya kutosha kila mwaka.
 
Asiwachongee! Kwani hajui baada kuathiliwa na vita ya Kagera walitakiwa kulipwa compesation ambayo haijatoka mpaka leo, labda serikali iliamua kuwalipa kwa njia hiyo.
 
Hata mimi najua hivyo kama ulivyosema. Kuna watumiji wadogo hasa wa vijijini wa chini ya units 75 kwa mwezi ndio wanufaika. Hii ni kwa nchi nzima na sio Bukoba tu.
Hata mimi najua hivyo, huyo mbunge utafti wake ni zero
 
aisee, wewe ndio usome vizuri

Alichosema wakazi wa kagera,mkoa ambao upo Tanzania, wanatumia umeme toka Uganda, na UNIT 80 wanauzia kwa Tsh. 10,000/= ilhali iyo elfu kumi kwa Bei ya shirika la umeme la Tanzania unapata Unit 28...
Ila Boss, tungeambiwa kwanza, huo umeme wa uganda, wanaBukoba wanalipa au kununua moja kwa moja kwa shirika la umeme la Uganda au TANESCO ndo wananunua kisha wanauza hilo eneo?

Sio tunabebwa bebwa na kiki za kisiasa za hawa watu, hakuna anayeruhusiwa kuuza umeme ndani ya pande hili la ardhi isipokuwa Tanesco tu.
 
TANESCO ni moja ya mashirika yaliyohujumiwa sana. Kama wangeachwa wajiendeshe bila mikono ya wanasiasa wangejiendesha kwa ufanisi sana na kutengeneza faida ya kutosha kila mwaka.
Pengine wasingeweza kupata hiyo faida kwakuwa wananchi wasingeweza kumudu gharama ya unit moja
 
Ila Tanesco kuhodhi uzalishaji na usambazaji umeme inaweza kuwa chanzo hapa kwetu kwa bei ya umeme kuwa juu kwa watumiaji wengi ambao hawajajiandikisha kama wale wanaotumia kiwango cha chini.
Mkuu, wawekezaji walio wengi wanakimbilia kwenye eneo la uwekezaji tu, hakuna mwekezaji aliyejitokeza kuwekeza kwenye usambazaji au usafirishaji wa umeme kwakujua fika gharama yake ni balaa kubwa.

Zaidi ni kwamba, kwenye usambazaji, wakopaji wakubwa wa umeme ni serikali wenyewe, sasa ni muwekezaji atakayekubali kukopwa au kulipwa baada ya mchakato wa malipo kukamilika serikalini, hata mwaka?
 
na advantage nyingine kukatika ni nadra sana
Mkuu umenikumbusha Miaka mingi iliyo pita kipindi nikiwa advance ihungo boys high school
Kuna muda tulitamani umeme ukatike ili tusiende prepo.....haahaa
Umeme haukatiki mzeya nadra Sana kama chozi la jogoo...
 
Back
Top Bottom