Uchaguzi 2020 Esther Matiko afichua Ufisadi wa kutisha TBC kwa Mwamvuli wa "Star Times " mwaka wa 11 hatujawahi Pokea devident, 35% ya hisa zetu nazo zayayuka

ABC ZA 2025

JF-Expert Member
May 2, 2018
1,158
701
Mbunge wa Tarime Mjini Mh Esther Nicholas Matiko ( Mb) aibua Ufisadi wa kutisha TBC.

Kampuni ya Star Media Tanzania LTD( Star Times & TBC ) kwa pamoja wameidanganya Serikali ya Tanzania kwamba hawajapata faida tangu kuanzishwa kwa kampuni hii mwaka 2009 takribani miaka 11 mfululizo.

Kwenye kampuni ya "Star Media Tanzania LTD"Serikali ya Tanzania kwa usimamizi wa TBC tunamiliki hisa 35% huku Star Times wakimiliki hisa 65%

Mwaka 2009 wakati Star Media Tanzania LTD inaanzishwa Sisi tulikuwa na US$ 83mil Sawa na tsh190bln wakati mradi mzima Ulikuwa na thamani ya US$ 238Mil takribani Tsh 547Bln

2019/2020 hadi Desemba 2019 walipapata hasara ya US$ 3,743,803, takribani tsh 6.8bln

Mwaka 2018 walipata hasara ya Tsh 19bln yaani kila mwaka wao ni hasara, hasara, hasara,

Mwaka Mmoja tu wa 2013/2014 ilipata hasara ya US$ 8,005,236 Sawa na tsh 17bln

Pamoja na kwamba hatujapata faida kwa miaka yote 11 Hata Mtaji wetu wa US$ 83mil Sawa tsh 191bln nao tumepigwa wote,

Sasa kampuni inamtaji (Negative equity) US$ 51.989 Sawa na takribani Tsh 119bln( Maana yake haina mtaji)
lakini kila tukiwaita Kwenye Kamati ya PAC hawatokei,

Je nani Yuko nyuma ya huu mchezo?
Je ni kweli CCM inapambana na Ufiasadi?

Je pamoja na hasara zote hizi kwanini Tanzania bado tunaendelea na Ubia? Nini maana ya haya yote?
 
TBC ni janga kama Corona tu,Juzi si wametoa gawio tena baada ya mkwara mzito kwamba muda ukipita watu wanakosa Vibarua vyao!

Swali la kujiuliza hio hela wametoa wapi kama wanapata hasara kila mwaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mliomsikiliza tuambieni. Yote kwa yote vyombo vya habari vimefungwa midomo waliobaki ni mavuvuzela na waimba pambio wa "Kishindo cha awamu ya tano".

Tanzania imekuwa na kikundi cha watu wanaofurahia watanzania kufikia kwenye ugoto huu wa akili. Hakuna tena anayepaza sauti ya kuonesha maovu bali kila mtu anapigania kupata nafasi ya kusifu na kuabudu.
 
Mbona walileta gawio? Gawio si linatokana na faida? Kwa hiyo walileta gawio feki sababu ya vitisho?
Usilete utaalamu wako wa (Dividend) hapa. Gawio kwa mujibu wetu sisi, ni neno lolote linalosemwa hadharani kuonesha kwamba tumefanikiwa kuliko waliotutangulia.

Gawio si lazima iwe ni faida halisi hata pongezi tu ni gawio. Au unataka tugawane faida wakati haipo?

Nyie ndio maana huwa mnaitwa vibaraka wa mabeberu na wasaliti wa maslahi ya nchi yetu. Mnajifanya kuhooji kila kitu.

Ha! Ha! Ha! Ha!
Pokea gawio la kicheko changu.
 
Atuambie capital invested so fa was how much, shida yenu mkiona loss mnajipa moyo kwamba ni kosa. Biashara ni profit and loss. Kama TBC walifanya uwekezaji unategemea watapata faida ndani ya mwaka mmoja. Wabunge wetu mnashida mahala. TBC imefanya uwekezaji mkubwa sana ndani ya miaka minne ningeshangaa kama wangekuja na faida. Dividend ni sehemu ya gharama za uendeshaji.Someni sheria ya Treasure Registrar
 
Mmeshawahi kumwona msimamizi wa mirathi ya familia kila mkimwita yeye ni chenga? kila akija na mahesabu unakuta madeni ambayo hayakuwahi kuwa na familia! Tatizo hapo ni walezi na wasimamizi wa kodi za wananchi ambao ni serikali
 
Atuambie capital invested so fa was how much, shida yenu mkiona loss mnajipa moyo kwamba ni kosa. Biashara ni profit and loss. Kama TBC walifanya uwekezaji unategemea watapata faida ndani ya mwaka mmoja. Wabunge wetu mnashida mahala. TBC imefanya uwekezaji mkubwa sana ndani ya miaka minne ningeshangaa kama wangekuja na faida. Dividend ni sehemu ya gharama za uendeshaji.Someni sheria ya Treasure Registrar

Soma vizuri andiko hilo umeambiwa miaka 11 wanapata hasara hiyo devident waitoe wapi?
 
Atuambie capital invested so fa was how much, shida yenu mkiona loss mnajipa moyo kwamba ni kosa. Biashara ni profit and loss. Kama TBC walifanya uwekezaji unategemea watapata faida ndani ya mwaka mmoja. Wabunge wetu mnashida mahala. TBC imefanya uwekezaji mkubwa sana ndani ya miaka minne ningeshangaa kama wangekuja na faida. Dividend ni sehemu ya gharama za uendeshaji.Someni sheria ya Treasure Registrar
Umekuja kutetea ufisadi kama kawaida yenu halafu mnajifanya wasafi! Miaka 11 hakuna faida mtaanza kupata faida lini tuwasubiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atuambie capital invested so fa was how much, shida yenu mkiona loss mnajipa moyo kwamba ni kosa. Biashara ni profit and loss. Kama TBC walifanya uwekezaji unategemea watapata faida ndani ya mwaka mmoja. Wabunge wetu mnashida mahala. TBC imefanya uwekezaji mkubwa sana ndani ya miaka minne ningeshangaa kama wangekuja na faida. Dividend ni sehemu ya gharama za uendeshaji.Someni sheria ya Treasure Registrar

Sasa unaambiwa wamepata hasara miaka yote tangu kuanza kwa Kampuni Sasa hiyo devident wataitoa wapi? Soma vizuri hili andiko
 
Back
Top Bottom