Esther Bulaya: Nyakilanganyi Construction LTD ni akina nani hawa miaka 12 ya upigaji fedha za maji Bunda! Rais, Waziri Mkuu wote wakwama

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,312
2,000
Mmenikumbusha Mzee wa Kulialia alituasa kwamba Mafisadi wana Nguvu saana Tanzania....huku yakitoka chozi la u uchungu Bungeni!!

Kweli huu ni mfano wa antachabos!!
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,107
2,000
Huyo Nyakirang'ani hana record ya kumaliza contracts anazopewa ni mbabaishaji sana na ni a very corrupt person tabia ambayo ndio aliyomponzea Magesa Mulongo the former Mara RC.

Ila kwa hili la Bunda utakuwa ni mkakati wa Magufuli kupambana na wapinzani which is a very foolish exercise.
 
Jikombe

JF-Expert Member
May 13, 2010
375
250

Unamaanisha Bunda imekuwa chini ya upinzani kwa muda wote wa kuanza kwa mradi?
Hapo tatizo linaonekana kuwa ni financier kabadilika wala siyo issues za siasa za vyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jikombe

JF-Expert Member
May 13, 2010
375
250
Usiwaamini sana politicians.
Kama mjumbe alivyosema hapo awali. Ukiyatafakari malalamiko ya Mh. Mbunge utaona kuwa yeye anadhani tatizo liko kwa Mkandarasi. Alitakiwa aonyeshe/ asema kuwa mkandarasi kafanya kazi ya kiasi kadhaa na kishalipwa zaidi ila hatekelezi mradi na serikali inamuohopa, hapo ningemuelewa kidogo. Kwa mantiki ya kawaida inaonekana serikali ndiyo inadaiwa na mkandarasi maybe kutokana na financier kubadilika ama kujitoa
Mbunge hawezi kuongea bila uhakika, Atakuwa anafahamu vema nini kinafanyika kwa miaka yote 12

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bichwa mtoto

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
274
1,000
Usiwaamini sana politicians.
Kama mjumbe alivyosema hapo awali. Ukiyatafakari malalamiko ya Mh. Mbunge utaona kuwa yeye anadhani tatizo liko kwa Mkandarasi. Alitakiwa aonyeshe/ asema kuwa mkandarasi kafanya kazi ya kiasi kadhaa na kishalipwa zaidi ila hatekelezi mradi na serikali inamuohopa, hapo ningemuelewa kidogo. Kwa mantiki ya kawaida inaonekana serikali ndiyo inadaiwa na mkandarasi maybe kutokana na financier kubadilika ama kujitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkandarasi alilipwa na mpaka sasa yuko ndani kwa uhujumu uchumi mbunge anaongea bila kuwa na data za kutosha ingawa kweli mradi bado haujakamilika kutokana na mkandarasi huyo kutafuna fedha ila kwa serikali hii makini imewezeshwa kukamatwa na yuko ndani akiendelea na kesi ya uhujumu uchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ABC ZA 2020

Senior Member
May 2, 2018
116
250
Mkandarasi alilipwa na mpaka sasa yuko ndani kwa uhujumu uchumi mbunge anaongea bila kuwa na data za kutosha ingawa kweli mradi bado haujakamilika kutokana na mkandarasi huyo kutafuna fedha ila kwa serikali hii makini imewezeshwa kukamatwa na yuko ndani akiendelea na kesi ya uhujumu uchumi

Sent using Jamii Forums mobile app

Unauhakika na unachoongea hebu msikilize tena Mh Mbunge Bulaya
 
Frank King

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
1,311
2,000
Kwanini bado anaendelea kupata miradi?

Nikwasababu Viongozi wote watoa tenda,,wapo mfukoni mwake.
Nimesema huyu mjamaa akipata dili la bilioni moja,,,atahakikisha million mia tano amenunua serikali,yaani yupo radhi apate faida ndogo lakini tenda ziwe zake kila iitwapo leo.
 
uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,220
2,000
Nyakirang'anyi constructions ltd , ni familia ya mwasisi mmoja . haigusiki na mama bado yupo , sasa unafikiri ataishije , jamaa alitumikia nchi kwa moyo wote hata ,kutuunganisha watanzania leo hii tunaongea lugha ya kiswahili tofauti na nchi za wenzetu . leo hii sisi sote ni ndugu . Hivyo ninyi mnaopiga kelele , mnatakiwa kunyamaza kabisa . afterall kazi inafanyika , hakuna kisicho fanyika .
 
Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
17,006

Muasisi hilo ni suala lake binafsi. Kama amepewa kazi na hajakamilisha, hapo ni suala la uwajibikaji na sio yeye ni nani. Watu wanataka maji, hivyo hana Audi kutimiza hill kwanza.
 
goggles

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,424
2,000
UTANGULIZI
Mbunge wa Bunda Mjini na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Esther Amos Bulaya( Mb) Jana/juzi ameendelea kurusha makombora mazito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na Ufisadi wa kutisha Kwenye mradi wa maji wilayani Bunda.

Mh Esther Bulaya aishangaa Serikali ya CCM kwa kujinasibu kuwa inapiga vita Wizi na Ufisadi wakati huohuo Kuna Wezi wanadunda tu mtaani kwa nguvu ya Serikali hiyo hiyo,

Mh Esther Bulaya kwa Uchungu anasema mkandarasi Nyakilanganyi Construction LTD ameshindwa kukamilisha mradi wa maji Wilaya Bunda kwa zaidi ya miaka 12 Sasa,Watanzania hebu
tusaidieni hivi hawa Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani kwa kiburi hikii kweli wako peke yao??

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh Khasim Majaliwa Khasim aliamuru Watu hawa wakamatwe kwa Uhujumu Uchumi lakini cha ajabu wakaachiliwa na kuendelea na mradi huo Kama kawaida,Watanzania Wenzangu hebu tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani hawa na ninani yuko nyuma/mbele yao?

Mh Bulaya anasema kunawakati akaunti za Nyakilanganyi Constraction LTD zilifungwa na TAKUKURU kwaajili ya Uchunguzi,Wizara chini ya aliyekuwa Waziri wa Maji wakati huo Prof Jumanne Maghembe wakamkopesha pesa nyingine na jamaa wakarejea site Kama kawaida, Nasisitiza Watanzania tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani Mbona Si Watu wa kawaida hawa??

Mh Bulaya anaendele kusimulia, Rais John Pombe Joseph Magufuli naye wakati wa ziara yake Mkoa wa Mara aliyaona ya Nyakilanganyi akamkabidhi kwa TAKUKURU wamchunguze, Chaajabu Wizara ikamruhusu tena aendelee na mradi wake,Watanzani hebu tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani haya maguvu wanayatoa wapi hawa yakupingana mpaka na Rais wa nchi??

Huu ni mwaka wa 12 Bunda wanasota na Kero ya maji,Kwa Msiofahamu ziwa Victoria liko km 2 tu toka yalipo makazi ya Watu, Mkandarasi kashindwa kufikisha maji site miaka 12,Watanzania tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni nani hasa?
_____
Pia,
Mh Bulaya pia amewaonya vikali Serikali ya Tanzania waache mara moja kuwakopa Pamba watoto wa masikini toka Kanda ya Ziwa, Serikali tajiri hii Kama inavyojinasibu kwanini inaamua kuwadhulumu Watu masikini kabisa Kama wakulima? Tunakwenda msimu mwingine wa Pamba lakini mpaka sasa wakulima wa Pamba Kanda ya ziwa bado wanadai zaidi ya Tsh 4bln,Hii Si Sawa kwa donor country Kama Tanzania,

Msikilize hapa
Ester Bulaya ni nani huyu!! Miaka mitano uko bungeni, umewasaidia nini wapiga kura wako??!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkaruka ataja rinu

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,177
2,000
Nyakirang’ani ni mfupa ulimshindaga fisi....
Jambaka lililoiweka serikalI MFUKONI tangu enzi ya Kikwete,,,mbabaishaji flani hivi mwenye kula na wakubwa,akipewa mradi wa ml 800 aidha wakukwangua tu barabara,atahakikisha ml 400 anainunua nayo serikali....yaani hiki kikampuni cha ajabu mno.
Ndo mmiliki wake anaitwa Mauza, huyo ni tapeli mkubwa. Ina maana hata mjomba kamshindwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ruhi

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
2,433
2,000
Mimi ni Mkazi wa Bunda naomba kumuhakikishia Mh Bulaya kuwa tunafahamu namna CCM inavyomuhujumu hapa Bunda ila Sisi tutakufa na Bulaya Bunda
CCM inamuhujumu mh Esther Bulaya asipate mshahara wake Bungeni au inahujumu wananchi wa Tanzania wasipate maendeleo jimboni Bunda?
Kama hujuma ufanyika kwa wananchi wa Bunda basi CCM siyo chama tena na usilitaje kwa kuanza na jina chama cha...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom