Esther Bulaya: Nyakilanganyi Construction LTD ni akina nani hawa miaka 12 ya upigaji fedha za maji Bunda! Rais, Waziri Mkuu wote wakwama

ABC ZA 2020

Senior Member
May 2, 2018
116
250
UTANGULIZI
Mbunge wa Bunda Mjini na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Esther Amos Bulaya( Mb) Jana/juzi ameendelea kurusha makombora mazito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na Ufisadi wa kutisha Kwenye mradi wa maji wilayani Bunda.

Mh Esther Bulaya aishangaa Serikali ya CCM kwa kujinasibu kuwa inapiga vita Wizi na Ufisadi wakati huohuo Kuna Wezi wanadunda tu mtaani kwa nguvu ya Serikali hiyo hiyo,

Mh Esther Bulaya kwa Uchungu anasema mkandarasi Nyakilanganyi Construction LTD ameshindwa kukamilisha mradi wa maji Wilaya Bunda kwa zaidi ya miaka 12 Sasa,Watanzania hebu
tusaidieni hivi hawa Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani kwa kiburi hikii kweli wako peke yao??

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh Khasim Majaliwa Khasim aliamuru Watu hawa wakamatwe kwa Uhujumu Uchumi lakini cha ajabu wakaachiliwa na kuendelea na mradi huo Kama kawaida,Watanzania Wenzangu hebu tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani hawa na ninani yuko nyuma/mbele yao?

Mh Bulaya anasema kunawakati akaunti za Nyakilanganyi Constraction LTD zilifungwa na TAKUKURU kwaajili ya Uchunguzi,Wizara chini ya aliyekuwa Waziri wa Maji wakati huo Prof Jumanne Maghembe wakamkopesha pesa nyingine na jamaa wakarejea site Kama kawaida, Nasisitiza Watanzania tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani Mbona Si Watu wa kawaida hawa??

Mh Bulaya anaendele kusimulia, Rais John Pombe Joseph Magufuli naye wakati wa ziara yake Mkoa wa Mara aliyaona ya Nyakilanganyi akamkabidhi kwa TAKUKURU wamchunguze, Chaajabu Wizara ikamruhusu tena aendelee na mradi wake,Watanzani hebu tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni akina nani haya maguvu wanayatoa wapi hawa yakupingana mpaka na Rais wa nchi??

Huu ni mwaka wa 12 Bunda wanasota na Kero ya maji,Kwa Msiofahamu ziwa Victoria liko km 2 tu toka yalipo makazi ya Watu, Mkandarasi kashindwa kufikisha maji site miaka 12,Watanzania tusaidieni Nyakilanganyi Constraction LTD ni nani hasa?
_____
Pia,
Mh Bulaya pia amewaonya vikali Serikali ya Tanzania waache mara moja kuwakopa Pamba watoto wa masikini toka Kanda ya Ziwa, Serikali tajiri hii Kama inavyojinasibu kwanini inaamua kuwadhulumu Watu masikini kabisa Kama wakulima? Tunakwenda msimu mwingine wa Pamba lakini mpaka sasa wakulima wa Pamba Kanda ya ziwa bado wanadai zaidi ya Tsh 4bln,Hii Si Sawa kwa donor country Kama Tanzania,

Msikilize hapa
 

Frank King

JF-Expert Member
Oct 7, 2012
1,311
2,000
Nyakirang’ani ni mfupa ulimshindaga fisi....
Jambaka lililoiweka serikalI MFUKONI tangu enzi ya Kikwete,,,mbabaishaji flani hivi mwenye kula na wakubwa,akipewa mradi wa ml 800 aidha wakukwangua tu barabara,atahakikisha ml 400 anainunua nayo serikali....yaani hiki kikampuni cha ajabu mno.
 

Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
17,006
2,000
Nyakirang’ani ni mfupa ulimshindaga fisi....
Jambaka lililoiweka serikalI MFUKONI tangu enzi ya Kikwete,,,mbabaishaji flani hivi mwenye kula na wakubwa,akipewa mradi wa ml 800 aidha wakukwangua tu barabara,atahakikisha ml 400 anainunua nayo serikali....yaani hiki kikampuni cha ajabu mno.
Kwanini bado anaendelea kupata miradi?
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,613
2,000
'Mh Bulaya pia amewaonya vikali Serikali ya Tanzania waache mara moja kuwakopa Pamba watoto wa masikini toka Kanda ya Ziwa, Serikali tajiri hii Kama inavyojinasibu kwanini inaamua kuwadhulumu Watu masikini kabisa Kama wakulima? Tunakwenda msimu mwingine wa Pamba lakini mpaka sasa wakulima wa Pamba Kanda ya ziwa bado wanadai zaidi ya Tsh 4bln,Hii Si Sawa kwa donor country Kama Tanzania'

Sawasawa.

dodge
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom