Esther Bulaya Bungeni: "vijiji 54, tayari vina umeme wa REA lakini wakandarasi wamelipwa tena waende wakaweke umeme Huu ni wizi"

Mhere Mwita

Verified Member
Jan 24, 2012
235
1,000
HOTUBA YA MBUNGE WA BUNDA MJINI MHE ESTHER AMOS BULAYA LEO BUNGENI JUU YA UFISADI KWENYE UMEME NA KUJIENDESHA KWA HASARA.
__________________________________________
Mheshimiwa Mwenyekiti Mimi ni Mbunge wa Awamu ya Pili na Tangu Nimeingia kwenye Bunge hili Serikali ya chama cha mapinduzi Haijawahi kutoa Pesa za REA zote Bali ya kwamba Pesa zipo kwenye Uzio, Na Mheshimiwa Mwenyekiti wote tunajua kwamba Pesa zikiwekwa kwenye uzio zinatakiwa ziende zote kwa Mujibu wa katiba na kwa Mujibu wa Taratibu zetu tulizojiwekea, Sasa naanza na awamu ya nne.

Mwaka 2010 na 2011 tulitenga Bilioni 56.883 zilizotolewa ni Bilioni 114; 2013 na 2014 zilitengwa Bilioni 53.158 zilizotolewa ni Bilioni 6.757; 2015 na 2016 zilitengwa Bilioni 420 zilizotolewa ni 141 Sawa na asilimia 34. 2017/18 awamu ya tano sasa ya Majigambo Mengi zilitengwa Bilioni 499 zimetolewa Bilioni 249 sawa na asilimia 49, Mheshimwa Mwenyekiti hii ndio Trend ya Serikali ya chama cha mapinduzi kushindwa kupeleka Pesa sehemu husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti tumesema Pesa kwenye Uzio zinaenda kwenye matumizi Maalumu lazima niende zote ndio hoja iliopo hapa ziko kwenye Link phase ndicho ninachokisema hapa na hiyo Trend ilianza tangu bunge lililopita na hili la Serikali ya awamu ya tano bado hamjafanikiwa kutoa Pesa zote, Mheshimiwa Mwenyekiti tunaenda awamu hii amejipambanua inashughulika na ufisadi, imeanza na mishahara hewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti mbali ya kwamba Fedha za REA haziendi zote lakini kumekuwa na ufisadi kuna malipo Hewa, REA imeipa kampuni HIFAB, Dollar za kimarekani elfu 81 na usheni, wakati ilipaswa kulipa Dollar Elfu 9 na hili jambo halijafanyika 2010, 2011, limefanyika 2017 kipindi cha Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani huu ni wizi kama wizi Mwingine unatakiwa wahusika washughulikiwe na mpaka sasa hivi kwenye hotuba yetu tumesema bado dollar za kimarekani elfu 44 bado hazijarudishwa REA,

Ambako huko Serikali hii inasema ya wanyonge ndio Pesa za wanyonge zinapopigwa, Huko ndiko ambako tunahitaji umeme vijijini, Huko ndiko ambako Serikali hii imewapa wakuu wa Mikoa waanzishe viwanda wakati kuna uchafu huu hivyo viwanda vitakamilikaje, lakini Mheshimiwa Mwenyekiti kuna ukaguzi ulifanywa, Kwa mikataba mitatu iliyoghalimu shilingi Bilioni 984 ambapo imegundulika vijiji 54, kwenye mikoa ya Tanga, Mwanza, Arusha, Manyara vijiji tayari vinaumeme lakini wakandarasi wamelipwa tena waende wakaweke umeme Huu ni wizi, na tunaposema wizi hatuwezi kunyamanza eti tukachagua awamu,

huu ni wizi kama uliofanyika hawamu zingine tunahitaji ukaguzi maalum ufanywe, Ili hiyo dhamira sasa ya kuzima vibatari mikoani na vijijini itekelezwe, kwa hiyo tutahitaji Majibu sahihi, Sasa kama vijiji 55 umetokea ufisadi huu, je kwa nchi nzima tumeingizwa mkenge kiasi gani, Huo wizi upo kiasi gani kwa hiyo haya lazima yafanyiwe kazi, Lakini Mheshimiwa Mwenyekiti kumekuwa pia na Malalamiko kwenye suala zima la kuunganishiwa umeme vijijini wanasema wenye Pesa ndio wamekuwa wakipewa kipaumbele kuunganishiwa umeme wananchi wa kawaida huko majimboni kwetu wanalia,

lakini Mheshimiwa Mwenyekiti jambo lingine ambalo ningependa kulizungumuzia kuhusiana na swala la Tanesco, Tanesco mpaka sasa hivi shirika linajiendesha kwa hasara imeshafika Bilioni 300 na, kipindi cha awamu ya nne wakati kinaondoka madarakani hasara ilikuwa Bilioni 124 yaani ongezeko la zaidi ya Bilioni 122 sasa tulitengemea Serikali hii inayokusanya kodi ingeenda kuondoa ile hasara nakuleta faida, bado kuna madeni kutoka Bilioni 700 mpaka 958 na TPDC pekee yake inaidai Tanesco Bilioni 340, Ndio maana kambi rasmi ya pinzani tulisema shirika hili litaenda kufa, sisi sio wa kwanza tumeshauri ligawanyeni kuwepo na mashirika mawili, Shirika hili limezidiwa uwezo, Athari hii ya kujiendesha kwa hasara inaenda kuathiri kwenye mtaji haya ndio huwa tunayasema Mheshimiwa Mwenyekiti.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom