Uchaguzi 2020 Esther Bulaya achukua Fomu ya Bunge, afanyiwa sala na Viongozi wa Dini

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,643
24,748
17 Agosti 2020
Bunda Mjini
Tanzania

ESTER BULAYA ALIVYOCHUKUA FOMU YA UBUNGE, MASHEHE, MAPADRI WAMPIGIA MAOMBI, SALA NA DUA KWA SAA NA NUSUAliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Ester Bulaya akikabidhiwa fomu ya Kuwania ubunge wa jimbo hilo na Msimamizi wa Uchaguzi Janeth Mayanja ili kutetea nafasi yake katika uchaguzi Mkuu 2020.

Msimamizi wa uchaguzi Janet Mayanja amewakumbusha waliochukua fomu wanatakiwa wazirejeshe tarehe 25 Agosti 2020 lakini wanaweza kufika ofisini kwake siku 3 kabla ya tarehe hiyo ili kuweza kupata nafasi ya kuzihakiki na kuzisahihisha kama itahitajika

Esther Bulaya akiongea mbele ya wana Bunda alisema anashukuru kupewa imani hiyo na kwa kuwa anajua kusoma na kuandika fomu hiyo itajazwa kwa umakini mkubwa na kusema hamasa waliyoionesha na imani ya wanaBunda 2020 imempa imani kubwa zaidi kuliko chaguzi zingine zilizopita.

Chanzo: Mwananchi digital
 
Anasubiria kuapishwa tuu + Heche + Matiku kila la kheri kwao

Mara hoyee!

Mwisho sio ila sio kwa umuhimu,tuzidi kumuombea zaidi Mdee naye apite kwa kishindo.
 
Toka maktaba

7 Julai 2020
VIDEO: BALAA LA ESTER BULAYA AKIFANYIWA PARTY JIMBONI KWAKE BAADA YA MIAKA MITANO YA UBUNGE 2015 -20207 Jul 2020
Mbunge wa Bunda Ester Bulaya alivyorudi Jimboni kwake akitokea Dodoma baada ya Bunge kuvunjwa nakufanyiwa party na wananchi, wanachama na viongozi wa Chadema ya kumpongeza kwa kukamilisha kazi yake ya Ubunge kwa miaka mitano.
 
Steven Wassira: 2020 nachukua fomu, 2015 tulihujumiwa na kudhulumiwa
Ninawania ubunge 2020 kupitia CCM Mpya mazingira yanaruhusu, 2015 CCM hata tungempeleka malaika asingeweza kushinda - mwisho wa kumnukuu Mzee Wassira.


Source : wasafi Media
 
Back
Top Bottom