Ester Matiko: Nimegundua wapinzani tulimpinga bila sababu Magufuli kafanya suala la maana kwenye DreamLiner

Nathan Jr

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
1,437
1,875
Mbunge wa upinzani Easter Matiko amesema jana kapanda ndege ya dreamliner na kujionea uzuri wake ;
Ameendelea kusema kwamba mara zote amekuwa akiisema serikali ya Kikwete kutonunua ndege lakin huyu kafanya,

Pia kashauri kwa uzuri ukubwa n.a. uwezo, wa ndege hiyo ATCL hawaitendei haki kuruka ndani ya nchi yaan domestic routes, kashauri ianze route za mbali kama ulaya na Asia,

Akaendelea kusema kwamba baada ya kuipanda amegundua kitu na kuwasihi wabunge wote wa upinzani na chama tawala kuipongeza serikali na kushauri inunue ndege nyingine zaid kama za bombadier na fast jet ili zifanye routes za ndani then tuongeze ndege kama dreamliner tufanye international routes

Dalili za kuhama hizi ili kesi ifutwe.

Wanachopinga wapinzani ni namna ndege hizi zinavyonunuliwa(kunuliliwa kwa cash n.k), kutokuwa na business plan na mambo mengine kama kuelekeza fedha nyingi kwenye ununuzi wa ndege na kusahau sekta zinazogusa watu wengu kama kilimo, n.k. na hata yeye (Ester) anafahamu hivyo.
 
Mbunge wa upinzani Easter Matiko amesema jana kapanda ndege ya dreamliner na kujionea uzuri wake ;
Ameendelea kusema kwamba mara zote amekuwa akiisema serikali ya Kikwete kutonunua ndege lakin huyu kafanya,

Pia kashauri kwa uzuri ukubwa n.a. uwezo, wa ndege hiyo ATCL hawaitendei haki kuruka ndani ya nchi yaan domestic routes, kashauri ianze route za mbali kama ulaya na Asia,

Akaendelea kusema kwamba baada ya kuipanda amegundua kitu na kuwasihi wabunge wote wa upinzani na chama tawala kuipongeza serikali na kushauri inunue ndege nyingine zaid kama za bombadier na fast jet ili zifanye routes za ndani then tuongeze ndege kama dreamliner tufanye international routes

Ester tunakusubiri Lumumba!
 
Mwanasiasa huyo hajui lolote... Pilots wetu wanahitaji kufikia kiwango fulani cha masaa ya kuruka na ndege hiyo ndipo waweze qualify international long distance routs...kwa sasa ndio watafuta hayo masaa.
Uko sahihi. Ila sio tu masaa ya kuruka bali pia Shirika la Ndege linatakiwa kuwa na ndege mbili (Dreamliner) na kuendelea ili kupata kibali cha kuruka kimataifa. Lakini kwa kuwa wengi hawajui na hata kama wanayajua haya watapotosha tu kwa manufaa binafsi....Mungu awasamehe.
 
..atcl ni KUPE.

..serekali ijiepushe na umiliki wa mashirika yanayosiyoweza kusimama bila RUZUKU toka ktk kodi za wananchi.

..mashirika ya ndege ya Kenya na Rwanda yanaendeshwa kwa HASARA. Shirika la ndege la Uganda limekufa.

..Hizo ni dalili mbaya kwamba atcl nayo itaendeshwa kwa hasara kwa muda mrefu.
 
Du! Hahahahaa...sasa ya nini kujitesa na gubigubi jamani...ndege ni yetu hata kama tuliiponda wakati inanunuliwa tuifurahie sasa mbona ni nzuri tuu...
Halima wa Kawe alifotolewa picha kinyemela akiwa amefura utafikiri katoka kung'olewa meno..hahaha.
 
Back
Top Bottom