Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,897
"Kama Waziri Kivuli na timu yangu tutahakikisha tunaandaa muswada binafsi na kuupeleka Bungeni, ili sasa wananchi wajue nani wanatetea wafanyakazi na wastaafu, wanaowanyonga ni wakina nani, na wenye dhamira njema kwa wafangakazi ni kina nani" Mhe Ester Amos Bulaya
KikokotooNaMafao "Serikali haikusikiliza maoni ya wadau muhimu wakiwemo wafanyakazi. Bunge lichukue nafasi yake katika jambo hili kuwaponya wastaafu." Mhe Ester Amos Bulaya
#KikokotooNaMafao "Nimesoma tweets za Kigwangala amesahau kuna maisha baada ya uwaziri,kuna wazee wametoka jimboni kwake wameleta ushahidi hawajalipwa mafao yao hadi leo wamekuja niwasaidie,akumbuke aliongoza mgomo kutetea maslahi ya madaktari,atetee wafanyakazi" Ester Amos Bulaya
=====
Mbunge wa Bunda Mjini, Eser Bulaya (Chadema), amesema anakusudia kuwasilisha muswada binafsi bungeni kupinga matumizi ya vikokotoo vya pensheni kwa madai kuwa vinamnyonya mfanyakazi.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 4, Bulaya amemtaka waziri husika kujitokeza na kusema kwanini mchakato wa uandaaji vikokotoo hivyo haukuzingatia ushirikishwaji wa wadau.
“Kwanini kumekuwa na malalamiko mengi… waache kutoa majibu mepesi kwenye hoja nzito. Mimi nikishikilia jambo huwa lina ukweli na nilikaa muda mrefu sijaongea nikifanya utafiti wa kina,” amesema Bulaya.
Kuhusu pongezi za Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema zimemuongezea nguvu ya kulishughulikia suala hilo.
“Pongezi za Spika nimezipokea na zimeniongezea kasi ya kukomaa na suala hili hadi dakika ya mwisho… na kufukuzwa bungeni nimezoea,” amesema Bulaya.
Chanzo: Mtanzania