Ester Bulaya awabwaga Waliofungua kesi ya Kupinga Ushindi wake wa Ubunge jimbo la Bunda Mjini

SCOOBY DOO

Member
Dec 16, 2013
76
69
Hukumu ya Kesi iliyofunguliwa na wapambe (wapiga kura) wa mzee Wasira ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Bunda yaliyompa ushindi Mhe Ester Bulaya imekamilika.

Katika hukumu hiyo Mhe Ester Bulaya kaibuka kidedea baada ya pingamizi lake aliloliweka Katika kesi hiyo kukubaliwa na mahakama hiyo na hivyo kufanya kesi hiyo kutupiliwa mbali.

Kesi hiyo ya madai imefunguliwa Novemba 19, mwaka 2015 na Magambo Masato na wenzake 30, ikipinga matokeo yaliyompa ushindi bulaya pamoja na wenzake 20 akiwamo mkurugenzi wa wilaya ya Bunda ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi na mwanasheria mkuu

=========

View attachment 319144
Mbunge wa Bunda amejihakikishia kuwatumikia wananchi wake bila Muwashawasha, baada ya kesi Iliyofunguliwa na Masato Wassira Kutupiliwa mbali na mahakama.

Hiki ndicho alichokiandika Mh. Mbunge Ester Bulaya;

''Nimemshinda Wasira kwa wananchi na leo nimemshinda mahakamani. Mahakama imetupilia mbali kesi yake dhidi ya Ushindi wangu.'

Wassira alipinga matokeo ya Uchaguzi jimbo la Bunda Mjini Mahakamani kuwa matokeo hayo sio halali na kwamba kuna hujuma zimefanywa ili kumuangusha na kumpendelea Esther Bulaya.
View attachment 319145
Wassira ambaye pia alikuwa Waziri wa Chakula na Ushirika, alidai kuwa matokeo yaliyotangazwa yana kasoro kubwa ikiwa ni pamoja na idadi ya kura zinazoonekana kuwa zilipigwa zinazidi jumla iliyopo kwenye matokeo hayo.

Alisema kuwa msimamizi wa uchaguzi alimhujumu kwa kuongeza tarakimu kwenye matokeo hayo na kwamba tarakimu hizo zilipelekea idadi ya wapiga kura kwenye kituo kimoja kuzidi idadi iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mwanasiasa huyo mkongwe pia alidai kuwa msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo bila kuzingatia sheria ya uchaguzi.
View attachment 319146
Wakili upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza, Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya.

Walioleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yalipingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.
 
Attachments

  • esta.jpg
    esta.jpg
    27.2 KB · Views: 161
  • wassira.jpg
    wassira.jpg
    30.8 KB · Views: 168
Wasira bado tu!!? ...............!! Nilifikiri alishakubali yakaisha!!

MiCCM ni migumu kweli kukubali!!
 
Namshauri Wasiri asikubali akate rufaa kwani wanaume wa Bunda hawawezi kuongozwa na mwanamke.
 
inabidi alipe gharama za kesi na usumbufu pia, hata hivyo zee limeuumbuka mara ya pili
 
TAARIFA:
Kesi iliyofunguliwa na Mzee Wasira na watu wake ya kupiga matokeo yaliyompa ushindi Mhe Ester Bulaya Jimbo la Bunda imetupiliwa mbali leo na mahakama kuu Mwanza
 
esta.jpg

Mbunge wa Bunda amejihakikishia kuwatumikia wananchi wake bila Muwashawasha, baada ya kesi Iliyofunguliwa na Masato Wassira Kutupiliwa mbali na mahakama.

Hiki ndicho alichokiandika Mh. Mbunge Ester Bulaya;

''Nimemshinda Wasira kwa wananchi na leo nimemshinda mahakamani. Mahakama imetupilia mbali kesi yake dhidi ya Ushindi wangu.'

Wassira alipinga matokeo ya Uchaguzi jimbo la Bunda Mjini Mahakamani kuwa matokeo hayo sio halali na kwamba kuna hujuma zimefanywa ili kumuangusha na kumpendelea Esther Bulaya.
wassira.jpg

Wassira ambaye pia alikuwa Waziri wa Chakula na Ushirika, alidai kuwa matokeo yaliyotangazwa yana kasoro kubwa ikiwa ni pamoja na idadi ya kura zinazoonekana kuwa zilipigwa zinazidi jumla iliyopo kwenye matokeo hayo.

Alisema kuwa msimamizi wa uchaguzi alimhujumu kwa kuongeza tarakimu kwenye matokeo hayo na kwamba tarakimu hizo zilipelekea idadi ya wapiga kura kwenye kituo kimoja kuzidi idadi iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mwanasiasa huyo mkongwe pia alidai kuwa msimamizi wa uchaguzi alitangaza matokeo bila kuzingatia sheria ya uchaguzi.
2.JPG

Wakili upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza, Kushoto ni mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya.

Walioleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yalipingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.
 
Vizur... Mzee akubali yaishe tu... Sio kupoteza muda..
Kuna nafasi za kichama, nadhani mzee yuko vizur
 
Isije tu kuwa lowasa ameshaikamata mahakama maana sasa,naona kila kesi inaegemea upande wa ukawa
 
Ester Bulaya ni damu changa Wasira atamuweza wapi? atulie tu tena kama mzee SIX.
 
Arudi sasa kijijini Gombe akashirikiane na ndugu zake katika suala zima la ustawi wa jamii.
 
Hukumu ya Kesi iliyofunguliwa na Wapambe wa Mzee Wasira ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Bunda yaliyompa ushindi Mhe Ester Bulaya imekamilika. Katika hukumu hiyo Mhe Ester Bulaya kaibuka kidedea baada ya pingamizi lake aliloliweka Katika kesi hiyo kukubaliwa na mahakama hiyo na hivyo kufanya kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Huyo wasira ni sawa na friends rangers kushindana na yanga
 
Back
Top Bottom