Mngendalyasota
Senior Member
- Jan 22, 2011
- 171
- 48
WanaJF,
Kwanza nimesikitishwa sana na uteuzi wa Estelina Kilasi (mbunge wa zamani wa Mbalali) kuwa mkuu wa wilaya mpya ya Wanging'ombe yenye makao yake makuu Igwachanya. Huyu mama alibwagwa vibaya sana na Mh Kilufi (mbunge wa sasa) kwenye kura za maoni 2010 kutokana na kushindwa kuwaletea Wana-mbalali maendeleo waliyoyataka. Miongoni mwa mapungufu aliyoyaonyesha akiwa mbunge ni kama ifuatavyo: kwanza wakati wafugaji wakihamishwa kutoka Ihefu kwenda mikoa ya kusini, rushwa ilitawala sana ktk kupembua nani ahame na nani abaki bonde la Usangu tena kinara wa kula rushwa akiwa mkuu wa wilaya wa wkati huo Hawa Ngurumo. Estelina Kilasi hakuwasaidia hata kidogo wale wafugaji kuona haki inatendeka. Pili wakati Gilbert Dololo(marehemu kwa sasa) mkuu wa wilaya wa zamani pia wa Mbalali alipokuwa anawaweka rumande wafanyabiashara ya mpunga wa Mbalali-Rujewa na Igulusi eti tu kwa kutokuelewana viwango vya ushuru wa magunia ya mchele yanayotoka nje ya wilaya, Estelina Kilasi alikaa kimya. Mwisho mama huyu huyu akiwa mbunge alikaa kimya wakati wakulima wa mpunga wa Mbalali na Kapunga walipokuwa wananyanyaswa na wawekezaji kwa kupandishiwa kodi ya kukodi majaruba ya mpunga na kunyimwa maji ya kunyweshea mipunga yao kwenye matoleo.
Huyu ndo leo kateuliwa na JK aende akaijenge Wanging'ombe wilaya mpya kabisa wakati jimbo lake lilimshinda.
Nawasilisha.