Escrow: Stanbic Bank kuchafua hali ya hewa

100% ni Kheri Wafe kwa Pressure Kwa maana Masikini Walalahoi Wanakufa kwa Mafua tu baada ya Kukosa hata Confline... Ebu na wafe wala hatutasikitika sana.
Pressure ni kubwa na ni swala la muda tu. Nguvu ya uvundo inakaribia ya Tsunami na kumbukeni Tsunami haizuiliki. Ni kama radi, ukishaona tu mwanga, kaa tayari kwa ngurumo...kuweka pamba masikioni hakusaidii.

EAHarbinderSinghSethi.jpg

Uhusiano wa huyu mtoaji na hawa wapokeaji ulitakiwa uwe kama wa panya na paka lakini masikini Tanzania...paka na panya wameshibana utadhani ni ndugu wa kuzaliwa! Anyway pole pole tutafika, a luta continua!
 
Santeee mkuu tena hata miaka ya baadae itabidi tuulize nyerere alikufaje na afukuliwe ili tumpime upya tuone
Jamani hebu waacheni wenzenu wapumue hili halijesha bado tena unakumbushia na hili mkuu
 
nasikia wanaogopa kuweka wazi sababu mkulu wa kaya anahusika na hata watunga sheria kule mjengoni wameogopa kumwajibisha mkulu wa kaya maana serikali ingevunjika na wabunge wangekosa kiinua mgongo chao .
 
Nimepenyezewa taarifa na mnene mmoja wa Stanbic kuwa Viongozi waandamizi wa Stanbic Bank huko majuu wanakaribia kuchafua tena hewa ya nchi.Waandamizi hao wameagiza kuanikwa kwa majina ya waliochota malumbesa ya fedha za Escrow. Wamewaagiza wakuu wa hapa Tanzania kuhakikisha ifikapo Aprili mosi mwaka huu,majina hayo yawe public pamoja na mihamala yao ili kusafisha taswira ya Stanbic.

Ukisikia kusafisha hapa na kuchafua pale ndio huku.Siombi hilo litokee.Hawa wa Mkombozi Bank aka wa Rugemalira wametuhenyesha hivi.Wa Stanbic itakuwaje? Stanbic Bank,please and please, re-think and re-decide. Tumechoka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Ni bora UNGA uanikwe leo ukilala utavunda ,hata paka atashindwa kuula.Hivyo Mzee wangu daima kwakoniwe Tanzania Kwanza mafusadi baadaye.Hata kama MKULU ameonja sumu waache stanbic bank watuanikie unga tu.Ni bora leo kuliko kesho.Na ngoja ngoja huumiza matumbo
 
Pressure ni kubwa na ni swala la muda tu. Nguvu ya uvundo inakaribia ya Tsunami na kumbukeni Tsunami haizuiliki. Ni kama radi, ukishaona tu mwanga, kaa tayari kwa ngurumo...kuweka pamba masikioni hakusaidii.

EAHarbinderSinghSethi.jpg

Uhusiano wa huyu mtoaji na hawa wapokeaji ulitakiwa uwe kama wa panya na paka lakini masikini Tanzania...paka na panya wameshibana utadhani ni ndugu wa kuzaliwa! Anyway pole pole tutafika, a luta continua!
...hawa paka na panya wa aina hii mwisho wao uko njiani mkuu....hakika ni suala la mda tu....watu wako kazini...haya mambo wala yanaweza yasifanyiwe kazi mwaka huu...ila yataibuka hata baada ya miaka...na hawa mchwa watajibu tu..hata kama watakua wamekimbia nchi na family zao.....siku hizi dunia hii ni kijiji...ukiiba utakamatwa tu......
 
Nchi imejaa wezi hadi basi. Haiwezekani Benki iliyo chini ya BOT ifanye miamala ya mabilioni ya shilingi bila BOT kuwa aware hizo fedha zimekwenda kwa nani, na wao standbic kutokuweka wazi hizo taarifa, ama kwa law inforcement agents au wananchi.

Jibu jepesi ni kuwa Serikali inayalinda majina ya hao waliofanyiwa hiyo miamala, je, kwa nini serikali iwalinde?

Ukifika hatua hii, unaanza kumuona JK na genge la washkaji zake kama matapeli tapeli flani hivi.
 
Stanbic wamevujisha kwa wafadhili hasa USA ili kulinda credit yake kwao ila kwa hapa bongo si rahisi...

JK heri angeachana na hizi double standards zinamzalilisha Sana mbele ya hawa wazungu coz wanaelewa kila kitu ndio maana wamemkazia Uzi mpaka sasa serikali iko hoi kifedha....

Haiwezekani Tibaijuka na Maswi waondolewe ofisini halafu akina Gurumo wabakie ofisini kwa kesi ile ile...

Siku majina ya Stanbic yakiwekwa hadharani hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe.....

Kaka.lusungo hawa wadhungu walishaipata ile lipoti yetu ya tangikulu mapema sana.Wala hawajaambiwa ni stanbiki benki.Ila se
Ilikali yetu ipo wazi yaani imejivua mpaka ule msulupwete wa ndani yaani kabla ya thuti.....
 
Mimi nilikuwa na akaunti yangu STANBIK ilibidi niifunge mara moja siwezi kufanya dhambi na wezi.Naomba na watanzania wenzangu tuige mfano huo.
 
Hii nchi sijui iuishwe na nani. Hao waliochukua hizo pesa wajitokeze haraka tume ya maadili. Hawawezi kubaki salama.
 
Kwa hiyo misaada tutaisikia kwa wenzetu tu? Lakini on serious note,inawezekanaje Tibaijuka et all uwatimue halafu hao wenye mapesa kila mfuko wa suruali tena wakiwa wafanyakazi wa Ikulu ufanye kama vile hakuna kitu? Hivi kweli hata hao Wazungu hata kama ndio kuwadanganya kuwa umechukua hatua nani atakuamini?

Hapo ndipo JK amekosa weledi Wa kudeal na complex issues...
Kwakuwa ameondoa wengine na kuacha wengine kwa kosa lile lile....
 
Mimi nilikuwa na akaunti yangu STANBIK ilibidi niifunge mara moja siwezi kufanya dhambi na wezi.Naomba na watanzania wenzangu tuige mfano huo.

Lengo la STANBIK kutaka kuwaanika wanufaika hao ni kutaka tusifunge account zetu kwao. Mimi yangu sitaifunga waweza ukute wakati wanarudisha hiyo mihela kiaccount change kikabahatika kuingia vumbi la hela nikajikuta silazimiki kufuatilia JAY millionaire.
 
Nimepenyezewa taarifa na mnene mmoja wa Stanbic kuwa Viongozi waandamizi wa Stanbic Bank huko majuu wanakaribia kuchafua tena hewa ya nchi.Waandamizi hao wameagiza kuanikwa kwa majina ya waliochota malumbesa ya fedha za Escrow. Wamewaagiza wakuu wa hapa Tanzania kuhakikisha ifikapo Aprili mosi mwaka huu,majina hayo yawe public pamoja na mihamala yao ili kusafisha taswira ya Stanbic.

Ukisikia kusafisha hapa na kuchafua pale ndio huku.Siombi hilo litokee.Hawa wa Mkombozi Bank aka wa Rugemalira wametuhenyesha hivi.Wa Stanbic itakuwaje? Stanbic Bank,please and please, re-think and re-decide. Tumechoka!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam

Uwiiiiiiiiii pamekucha
 
Mzee Tupatupa nasikia ndugu zako walikorofisha CCTV ya hapa stanbic bongo na kuchezea mitambo ila sauzi walidaka kila kitu sijui mtaponea wapi? tunasubiri agizo moja la bunge kuitangaza benki ya stanbic kuwa ni "money laundering concern" unadhani watakubali wasauzi kutolewa kafara? lazima wafe na mtu.Na msipotekeleza maagizo yote ya bunge basi msahau kabisa fedha za wafadhili.
 
Back
Top Bottom