Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,443
- 113,452
Wanabodi,
Najua wengi wetu, tumehamanika na mjadala wa Escrow na Ripoti ya PAC, kwetu sisi wengine wenu, ile Ripoti ya PAC ya jana, tunaiona hakina kitu wala haina jipya bali ni sehemu tuu ya mihemuko ile ile kuhusu sakata hili tangu mwanzo.
Escrow ni matokeo tuu, watu humu wanashangilia matokeo tuu, nikadhani ripoti hiyo ingetupeleka kwenye chanzo cha jinamizi hili la IPTL ili tung'oe tangu mizizi!, IPTL ni rushwa mwanzo mwizo!, hivi mnamjua ni nani aliyewaleta?!.
Hayo ya Ripoti ya PAC ni cha mtoto, kikubwa kwangu Escrow: Mahakama Imedhalilishwa!. Imedharauliwa!, Imefedheheshwa!-Ili Kulinda Heshima Yake inabidi Mahakama itoe statement, kwanza kukitafsiri Ibara ya 100 ya Katiba ya JMT, kuhusu nani yuko right kati ya Mahakama kutoa amri halali kulizuia Bunge kujadili issue iliyoko mahakamani, au mahakama ndio iliyokosea kutoa amri kwa Bunge, uwezo ambao mahakama haina.
Na ili kuilinda heshima yake, kama ni Jaji alikurupuka, then mahakama itamke wazi kwa kumvua ujaji jaji huyo aliyopelekea Mhimili wa Mahakama kudhalilishwa!, kudharauliwa! na kufedheheshwa!, hali itakayopelekea stop orders za mahakama zitakuwa zinadharauliwa kila siku. Vinginevyo wakitamka zuio lile lilikuwa ni amri halali, then Mahakama italifanya nini Bunge kwa kuidhalilishwa!, kuidharauliwa! na kuifedhehesha Mahakama?!.
Kwa watu wote wanaojua utawala wa sheria, "the doctrine of separations powers!", kati ya mihimili hii mitatu ya dola, hawawezi kuiacha hali hii ikapita tuu hivi hivi!.
Paskali
NB-Mode, hii mada inahusu hoja za kisheria na sio hoja za kisiasa!.