Escrow Kimenuka: Uongo wa Taarifa ya Kamati ya PAC kuhusu sakata la ESCROW

Kujadili na hawa wezi na vibaraka wao ni kuhujumu jitihada za kupambana na mafisadi, vibaraka wanaviwashwa washwa sana kuliko wezi ambao walishakiri kuchukua mboga na vijisenti vya ugoro
 
watakaoshinda kwenye chaguzi za 2015 ni wale watakaokuwa wanasema Escrow ni mali ya umma na waliopata mgao ni wezi, kinyume cha hayo usitegemee kupata kura
 
Kama nilivyotonywa na kuubamba kwenye mtandao: Index of /escrow/viambatanisho

Sitii langu hapa:



UONGO WA TAARIFA YA KAMATI YA PAC KUHUSU SAKATA LA ESCROW




SALIM KHATRI

SKHATRI@ORCIS.COM


Yaliyomo


Utangulizi.......................................................................................................................................... 2

Uongo wa Kuwepo kwa Shauri Namba Mbili Lililofunguliwa ICSID na TANESCO mwaka 2004 (ICSID‐2).. 2

Uongo wa Prof. Muhongo kuwa Dalali kati ya Bw. Rugemalira wa VIP na Bw. Sethi wa PAP.................. 6

Uongo Kuwa Uthibitisho na Vielelezo Alivyopata Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ni Taarifa ya

Kamati ya Wataalamu........................................................................................................................ 7

Upotoshwaji wa Agenda za Mkutano wa IPTL na TANESCO................................................................. 9

Uongo wa Nukuu ya Barua ya Mwanasheria wa TANESCO................................................................ 10

Orodha ya Viambatanisho............................................................................................................... 12

1

Utangulizi

Baada ya kuisoma Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali iliyojulikana kama “Taarifa ya Kamati Kufuatia Matokeo ya Ukaguzi Maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Akaunti ya Tegeta Escrow Iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania” (itarejewa humu kama “Ripoti ya PAC”), mwandishi wa makala hii alijaribu kutafuta Taarifa ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (CAG) iliyojulikana kama “Taarifa ya Ukaguzi Maalum Kuhusiana na Miamala Iliyofanyika katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta, Pamoja na Umiliki wa Kampuni ya IPTL” (itarejewa kama “Ripoti ya CAG”).

Walichotakiwa kufanya Kamati ya PAC ni kuwasilisha Ripoti ya CAG bungeni ikiwa na maoni na uchambuzi wao lakini kilichofanyika ni Kamati ya PAC kuwasilisha ripoti yao ambayo ni tofauti kabisa na Ripoti ya CAG. Ripoti ya PAC imeongeza hoja na ajenda zake ambazo nyingi ni za UONGO na pia kunyofoa na kuficha hoja kadhaa za Ripoti ya CAG kwa makusudi ili kuipa nguvu hoja na ajenda za Kamati ya PAC.

Baada ya kusoma Maelezo ya Serikali Kuhusu Ripoti ya CAG iliyosomwa Bungeni na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, mwandishi aliamua kuitafuta Ripoti ya CAG na viambatanisho vyake pamoja na Ripoti ya PAC na viambatanisho vyake. Baada ya kusoma ripoti zote hizo mbili pamoja na baadhi ya viambatanisho vilivyoweza kupatikana kwenye mitandao ya kijamii, mwandishi aligundua kuwa Ripoti ya PAC iliyowasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa PAC, Mh. Zitto Kabwe mwezi Novemba 2014 ilijaa uongo, udanganyifu na ulaghai wa kiwango cha juu kabisa. Ripoti ya PAC ina sifa zote za kuitwa “Utapeli wa Kisiasa”.

Kamati ya PAC imetumia mseto wa hoja zilizochanganywa kwa makusudi wakijua wazi kuwa suala la mgogoro wa IPTL na TANESCO uliopelekea kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow ya Tegeta ina mambo mengi kama mahakimu wa kesi ya ICSID namba ARB/10/20 walivyoielezea hili suala kuwa na “complex facts, multiple proceedings and multiple participants”.

Utaalamu wa kuchanganya mseto wa hoja kwa nia ya kuwachanganya na kuwahadaa walengwa unaweza kuvumilika kisiasa. Lakini uongo na udanganyifu katika kutoa “facts” za uongo na kutoa nukuu za uongo haziwezi kuvumilika sehemu yoyote ile.

Katika makala hii, mwandishi atajadili uongo, udanganyifu na ulaghai ulioko kwenye Ripoti ya PAC kama ilivyoorodheshwa hapa chini:


  1. Uongo na wa kuwepo kwa shauri namba mbili lililofunguliwa ICSID na TANESCO mwaka 2004 (ICSID‐2)


  1. Uongo wa Prof. Muhongo kuwa dalali kati ya Bwana Rugemalira wa VIP na Bwana Sethi wa PAP


  1. Uongo Kuwa Uthibitisho na Vielelezo Alivyopata Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ni Taarifa ya Kamati ya Wataalamu


  1. Upotoshwaji wa Agenda za Kikao cha Pamoja cha IPTL na TANESCO


  1. Uongo wa Nukuu ya Barua ya Mwanasheria wa TANESCO

Uongo wa Kuwepo kwa Shauri Namba Mbili Lililofunguliwa ICSID na TANESCO mwaka 2004 (ICSID‐2)

Ripoti ya PAC (Kiambatanisho No. 1) Ukurasa wa 6 inanukuliwa hivi:

2

“Mheshimiwa Spika, kutokana na kutoridhishwa na kiwango cha capacity charges kilichokuwa kinatozwa na IPTL mnamo mwaka 2004, TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya capacity charges. Uamuzi wa Baraza ilikuwa ni kwamba Wanahisa waketi na Mteja wao (TANESCO) na kukubaliana kuhusu kanuni ya ukokotoaji wa tozo hiyo.

Mheshimiwa Spika, mpaka tunapowasilisha Taarifa hii Bungeni, Uamuzi wa ICSID‐2 kwamba IPTL ikae na TANESCO kwa ajili ya kukokotoa upya capacity charges haujatekelezwa, hivyo TANESCO wanaendelea kulipa USD. 2.6 milioni (sawasawa na shilingi 4,511,000,000/= kwa mwezi) kila mwezi kama capacity charges kwa IPTL izalishe au isizalishe umeme. Hivyo, utekelezaji wa Mkataba wa uzalishaji wa umeme kati ya IPTL na TANESCO umetawaliwa na migogoro toka ulipoanza mpaka sasa.”

Paragraph ya kwanza iliyonukuliwa hapo juu inadai mwaka 2007 TANESCO ilibaini tatizo halafu kwenye paragraph inayofuatia TANESCO ikaamua kufungua shauri la pili ICSID mwaka 2004 kutokana na kutoridhishwa yale waliyoyabaini mwaka 2007. Tatizo linagunduliwa 2007 halafu unaenda kulifungulia shauri ICSID mwaka 2004?

Cha kuzingatia kwenye uongo na upotoshwaji huu ni kuwa

Hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa ICSID mwaka 2004 na TANESCO.

Kesi pekee iliyopata kufunguliwa ICSID na TANESCO ni ile kesi/shauri namba ARB/98/8 iliyofunguliwa mwaka 1998 na kutolewa uamuzi mwaka 2001. Kesi/shauri hilo linarejewa (referred as) kama ICSID‐1 kwenye Ripoti ya PAC.

Ufuatao ni ushahidi wa kuwa hii kesi ICSID‐2 inayodaiwa na Ripoti ya PAC haipo:

Ripoti ya PAC haijaweza kutuambia hiyo kesi iliyofunguliwa mwaka 2004 na kurejewa kama ICSID‐2 ilikuwa kesi/shauri namba ngapi. Kwenye Ripoti ya PAC, ICSID‐1 ilitajwa kama kesi iliyofunguliwa mwaka 1998 na namba yake kutajwa kama ARB/98/8 lakini Ripoti hiyo hiyo imeshindwa kutuambia namba ya kesi ya ICSID‐2. Hivyo hivyo, hukumu ya kesi/shauri la ICSID‐1 iliambatanishwa kwenye Ripoti ya PAC kama Kiambatanisho Na. 2 lakini Ripoti hiyo ya PAC haikuambatanisha hukumu ya hiyo kesi ICSID‐2.

Tovuti ya ICSID (https://icsid.worldbank.org) imeorodhesha kesi zote zinazosimamiwa na ICSID tokea kuanzishwa kwake. Kesi/shauri pekee lililopata kufunguliwa na TANESCO hapo ICSID ni lile shauri namba ARB/98/8.

Ukurasa wa 34 wa Ripoti ya PAC inanukuliwa “Kutekelezwa kwa uamuzi uliotolewa na Kituo cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji cha Kimataifa (ICSID) mwezi Februari 2004 (ICSID 2). Aidha, ICSID 2 ilielekeza TANESCO na IPTL kukokotoa upya kiwango cha capacity charges.”

Ni vigumu kuamini kuwa kesi iliyofunguliwa mwaka 2004 huko ICSID ikapata uamuzi mwezi Februari 2004. Hata kama hiyo kesi ilifunguliwa Januari mosi 2014 na kupatiwa hukumu tarehe ya mwisho ya Februari 29, 2004 bado ni vigumu kuamini kuwa kesi inaweza kupatiwa ufumbuzi ndani ya siku 60 tokea ifunguliwe.

3

Ripoti ya CAG haijataja hata mara moja kuhusu kesi ya ICSID‐2. Je, CAG alikuwa amepotoka ama alikuwa anajaribu kuficha kitu? Yaani inawezekana kweli CAG asiweze kuitaja ama kuijadili kesi inayodaiwa kuwa na umuhimu mkubwa kiasi hicho kama inavyodaiwa na Ripoti ya PAC?

Hoja kuu ya Ripoti ya PAC ni kuwa fedha za Escrow zilikuwa “zimechotwa” kwa sababu makubaliano kati ya TANESCO na IPTL hayakuzangatia madai ya TANESCO yaliyopelekea kufungua ICSID‐2 na uamuzi uliotolewa kwenye hukumu ya hiyo kes/shauri la ICSID‐2. Tumeona hakuna ICSID‐2 lakini uamuzi wa hukumu ya ICSID‐2 imetumiwa kujenga hoja kuu mara kadhaa kwenye Ripoti ya PAC ikiwemo kwenye ukurasa wa 6 (mara mbili), 23, 26, 34, na 40 (mara mbili).

Tuhuma kubwa zinatolewa kuwa fedha za Escrow zilitolewa kuilipa IPTL bila ya kuzingatia maamuzi ya kesi/shauri ICSID‐2 kwenye kurasa hizo zote juu. ICSID‐2 haiko, na hukumu ya ICSID‐2 na tuhuma zote zinazohusisha ICSID‐2 nazo ni tuhuma za UONGO zilizojengwa kwa UDANGANYIFU na ULAGHAI.

Utetezi wa Mwenyekiti wa PAC juu ya uongo huu

Katika midahalo ya ukumbi wa Wanazuoni (http://groups.yahoo.com/wanazuoni) Mwenyekiti wa PAC, Mh. Zitto Kabwe amejaribu kutoa utetezi wa madai ya kutokuwepo kwa shauri/kesi ya ICSID‐2 kama inavyodaiwa na mwandishi. Maelezo yake ni haya:

“Shauri la ICSID 2 lipo na limeamuliwa. Shauri lilifunguliwa na IPTL dhidi ya tanesco. IPTL walipowekwa kwenye ufilisi hapa nyumbani SCB‐HK kama wadai wa IPTL wakaomba kuingizwa kwenye shauri na mahakama ikawakubalia. Uamuzi wa mahakama tayari umetoka na unawataka tanesco wakae na IPTL kukokotoa upya tozo ya uwekezaji. Baada ya IPTL kuondolewa kwenye ufilisi walipaswa kufanya hivyo. Hawakukaa. Tanesco wameomba muda zaidi kufanya hivyo. Lakini kuomba huko muda kumefanywa fedha zimeshachotwa kutoka kwenye akaunti hiyo. PAP pia inaendelea kulipwa tozo ya $2.6m kila mwezi ( kwa kutumia tozo ya zamani).”

‐‐Mh. Zitto Kabwe (Januari 1, 2015)

“Soma hansards za bunge kwenye majumuisho nilisahihisha hilo. Tanesco ilishtakiwa na IPTL. SCB‐HK waliomba kuingizwa kwenye kesi hiyo. TANESCO walishinda kesi hiyo na ikaamriwa kuwa ufanyike ukokotozi Mpya wa tozo ya uwekezaji”

‐‐Mh. Zitto Kabwe (Januari 2, 2015)

Ni wazi Mh. Zitto Kabwe katika majibu yake aliyoyatoa kwenye ukumbi wa Wanazuoni akimjibu mwandishi wa makala hii anachanganya ICSID‐2 (kesi inayodaiwa kufunguliwa na TANESCO mwaka 2004 huko ICSID) na ICSID Case No. ARB/10/20 ambayo Decision on “Jurisdiction and Liability” (siyo final award) imetolewa Februari 12, 2014. Soma Kiambatanisho Na. 3 – Decision on Jurisdiction and Liability of ICSID Case No. ARB/10/20.

KWANZA, siyo kweli kuwa Mh. Zitto “alisahihisha” chochote kwenye hotuba yake ya majumuisho. Kitu cha kwanza cha kufanya wakati wa kusahihisha jambo lolote lililokosewa ni kukiri kuwepo kwa kosa na kubainisha palipofanyika makosa. Hili Mh. Zitto hakulifanya. Kinachofuatia baada ya kukiri kosa ni kusema waziwazi kipi kimebadilika. Mh. Zitto kaeleza tu kuwa hiyo kesi ICSID‐2 ipo na ilifunguliwa na IPTL halafu Standard Chartered Bank wakaomba kuingia kwenye kesi. Unaweza ukaangalia video hii https://www.youtube.com/watch?v=wT_R40LcZpU ya Mh. Zitto akitoa hayo maelezo. Madai ya kusema

4

kuwa alisahihisha ni UONGO na pia hayo maelezo yanayodaiwa kuwa yalisahihisha nayo yenyewe ni ya UONGO kama tutakavyoona kwenye maelezo yanayofuatia.

PILI, Mh. Zitto kagoma katakata kutupa namba ya hiyo kesi ya ICSID‐2 inayodaiwa kufunguliwa na IPTL halafu SCB‐HK wakaingia kwenye hiyo kesi baada ya kuomba kuingizwa. Anafanya hivi akijua kabisa akitoa namba ya hiyo kesi, basi maelezo yaliyomo kwenye uamuzi (decision, siyo award) ya hiyo kesi itakuwa inapingana na madai yake ‐‐ soma maelezo kwenye paragraph inayofuatia. Hivyo pamoja na kuwa namba ya kesi ya ICSID‐2 imegomewa kutolewa na Mwenyekiti wa PAC, hivyo tunachukulia kesi anayoidai na Mh. Zitto kuwa ilitolewa uamuzi ni ile ICSID Case No. ARB/10/20 (Kiambatanisho Na. 3).

TATU, hii kesi haikufunguliwa na IPTL kama inavyodaiwa na Mh. Zitto. Haya madai ni ya UONGO. Hii ni kesi iliyofunguliwa na Standard Chartered Bank, Hong Kong (SCB‐HK). Ukisoma Paragraph ya 5 ya “Decision on Jurisdictin and Liability” ya hiyo kesi ni wazi kuwa SCB‐HK ndiye aliyefungua hiyo kesi na wala siyo IPTL kama inavyodaiwa na Mh. Zitto. Hakuna popote inapoeleza kuwa IPTL ilifungua hiyo kesi na baadaye SCB‐HK ikaomba kuingizwa kwenye hiyo kesi kama inavyodaiwa na Mh. Zitto.

NNE, Mh. Zitto kaamua kutoa haya maelezo ya UONGO kwa sababu alijua wazi kuwa akikubali mbele ya umma wa Watanzania kuwa hakuna kesi ya ICSID‐2 iliyopata kufunguliwa na TANESCO mwaka wowote ule zaidi ya ile kesi iliyofunguliwa mwaka 1998 (ICSID Case No. ARB/98/8) hoja zake zote (ambao ndiyo msingi wa Ripoti ya PAC) zilizojengwa kutokana na hii kesi zitaporomoka. Sasa njia pekee ni kudai kuwa hiyo kesi ya ICSID ni ile kesi ya ICSID Case No. ARB/10/20. Tatizo la kesi hii ni kuwa mdai wa kesi ni SCB‐ HK na mdaiwa ni TANESCO. Hivyo hoja zile zote zilizojengwa na madai ya hukumu ya ICSID‐2 inawataka TANESCO na IPTL wakae pamoja inakuwa haina nguvu kwani IPTL siyo mdai wala mdaiwa kwenye hiyo kesi. Hivyo kuna ulazima kwa Mh. Zitto kuendelea kuunda UONGO mwengine ili kuwaaminisha Watanzania kuwa IPTL ni mdau wa hiyo kesi na hii ni kwa kudai kuwa IPTL ndiyo aliyefungua hiyo kesi na eti baadaye SCB‐HK wakaomba kuingizwa na kuchukua nafasi ya IPTL. Huu ni UONGO.

TANO, kama ICSID‐2 ni kesi iliyofunguliwa na IPTL (halafu SCB‐HK akaomba kuingizwa kwenye hiyo kesi) ambayo hukumu decision yake ilitoka February 2014, basi hoja hizi kwenye Ripoti ya PAC hazina mshiko:


  1. “Mheshimiwa Spika, Kamati imeshangazwa na makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya Bodi ya TANESCO na IPTL, ikizingatiwa kuwa mgogoro wa msingi uliohusu madai ya TANESCO kutozwa capacity charges kubwa na IPTL haukupatiwa ufumbuzi kama ilivyoelekezwa na ICSID.” (Ripoti ya PAC Uk. 23).

Makubaliano kati ya IPTL na Wizara ya Fedha kulipwa kwa fedha zilizoko kwenye Akaunti ya Escrow yalifanyika Oktoba 2013, na kama ICSID‐2 ni kesi iliyotolewa decision Februari 2014 basi hiyo hoja haina mshiko kwani huwezi kuwataka TANESCO na IPTL Oktoba 2013 kufuata maamuzi ya ICSID yaliyotolewa February 2014.


  1. “..na ilhali akijua fika kuwa kulikuwa na shauri lililohusu mgogoro wa capacity charges kwenye Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa migogoro ya Uwekezaji (ICSID 2), Mwanasheria Mkuu badala ya kushauri kupata suluhu ya shauri lililoamuliwa na ICSID 2 alitumia mamlaka yake kuelekeza fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW kutolewa kwenda IPTL.” (Ripoti ya PAC Uk. 26). Tena huwezi kumshikia bango mtu kwa maamuzi yaliyofanyika Oktoba 2013 eti hakushauri kupata suluhu ya shauri lililoamuliwa Februari 2014.

5

SITA, unajiuliza hivi watu 24 wanakaa pamoja siku kadhaa wanawezaje wote kwa pamoja kukosea kuandika hii miaka ya hiyo kesi? Wanawezaje kusahau kuambatanisha hukumu ya ICSID‐2? Wanawezaje kusahau hata kuandika namba ya hiyo kesi? Hivi huu uzembe unaweza kuwa uzembe wa bahati mbaya au ni uzembe by design? Ama Ripoti iliandikwa na mtu mmoja?


Uongo wa Prof. Muhongo kuwa Dalali kati ya Bw. Rugemalira wa VIP na Bw. Sethi wa PAP

Tuhuma na maelezo ya madai kuwa Prof. Muhongo alikuwa “dalali” wa kuuziana hisa za VIP kwenye IPTL kwa PAP yako kwenye ukurasa wa 24 wa Ripoti ya PAC inayonukuliwa hivi:

“Mheshimiwa Spika, Kamati imepitia Mkataba wa mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP na kuthibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo (Mb) ndiye alikuwa kiungo kati ya Bw. Harbinder Singh Sethi wa IPTL na Ndg. Rugemalira wa VIP (Kiambatisho Na. 16). Katika mkataba huo wa tarehe 19 Agosti, 2013. Ndg. James Rugemalila alithibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo alimwomba kuwasilisha kiasi cha fedha ambacho angependa kulipwa na IPTL ili kumaliza Shauri lililokuwepo mahakamani. Aidha, Bw. Sethi aliwasilisha kwa Bw. Rugemalira ushahidi kwamba PAP imenunua Hisa 7 za Mechmar katika IPTL.

“On 11th July 2013, the Minister of Energy and Minerals, Hon. Dr. Prof. Sospeter Muhongo invited VIP to submit to him the amount of money if paid VIP would conclusively settle VIP claims against IPTL”.

Mheshimiwa Spika, mchakato wote wa kutoa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW ndipo ulipoanza na mauzo ya hisa za VIP kwenda PAP na baadaye kuhitimishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013 ambayo ndiyo yaliyotumika kuhalalisha utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba, 2013.”

Katika kutilia mkazo hiyo hoja kuwa Prof. Muhongo ndiyo alikuwa “dalali” wa kuuziana hizo hisa, Ripoti ya PAC Uk. 41 unasema hivi:

“Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa Nishati na Madini ndiye alikuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi na Bwana James Rugemalira, tena katika ofisi ya Umma; na pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu ya upotoshaji huu. Waziri wa Nishati na Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya biashara kwa jina la IPTL.”

Picha iliyojengwa kwenye Ripoti ya PAC ni kuwa Prof. Muhongo alimuita Rugemalira na Sethi ofisini kwake. Akamwambia Rugemalira alete kiasi cha fedha anachotaka kulipwa na Sethi na Sethi akaambiwa alete ushahidi kwamba amenunua Hisa 7 za Mechamar katika IPTL. Wakakutana wote watatu ofisini kwa Prof. Muhongo na biashara ya kuuziana hisa ikafanyika hapo ofisini kwa Waziri – ofisi ya umma!

Madai haya ni ya UONGO kwani nukuuu ya “Mkataba wa Mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP” (tazama Kiambatanisho Na. 4) yanayodaiwa kuwa ndiyo “uthibitisho” wa madai haya yamechakachuliwa. Ukurasa wa 4 na 5 wa huo mkataba unanukuliwa hivi:

6


“(m) On 11h July 2013, the Minister of Energy and Minerals, Hon. Dr. Prof. Sospeter Muhongo, (MP) invited VIP to submit to him the amount of money which if paid, VIP would conclusively settle VIP's claims arising from the IPTL Disputes whereupon VIP wrote to the Minister raising 11 questions and proposing to be paid US$ 95million by the 31 " July 2013 for the Plant and future receivables from the PPA and US$ 465million for post damages.”

Baada ya kusoma nukuu za Ripoti ya PAC na nukuu za Mkataba wa Mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP kama ilivyonukuliwa hapo juu, basi kuna vitu kadhaa vya kuzingatia:

KWANZA, Paragraph (m) ya Mkataba kati ya VIP na PAP imenukuliwa nusu kwa makusudi kabisa. Ni vigezo vipi Kamati ya PAC walitumia kunukuu hiyo paragraph kwa kutafuta mahala pa kuimalizia? Kwanini maelezo mengine waliamua kuyanyofoa? Ni wazi kipande cha nukuu kilichonyofolewa kwenye Ripoti ya PAC ilikuwa inaelezea madai ya VIP dhidi ya Standard Chartered Bank (SCB). Kunyofolewa kwa hichi kipande hakujafanywa kwa bahati mbaya bali kwa makusudi na malengo mahsusi.

Pamoja na kunukuu hiyo paragraph iko nusu na kunyofolewa kwa maneno, pia nukuu yenyewe imechakachuliwa. Mkataba unasema “…amount of money which if paid, VIP would conclusively settle VIP’s claims arising from the IPTL Disputes..” na kwenye Ripoti ya PAC imenukuliwa hivi “…the amount of money if paid VIP would conclusively settle VIP claims against IPTL”. Kubadilisha maneno wakati wa kunukuu ni udanganyifu na uchakachuaji wa kiwango cha juu kabisa.

PILI, wanaopatanishwa hapo siyo Rugemalira wa VIP na Sethi wa IPTL kama Ripoti ya PAC inavyodangaya. Bali wanaopatanishwa ni VIP na Standard Chartered Bank (SCB) kama hiyo paragraph nzima isiyochakachuliwa inavyosema. Rejea mkataba mzima wa mauzo ya hisa kati ya kampuni ya PAP na VIP (Kiambatanisho Na. 4) ni wazi kwenye hiyo nukuu wahusika wanaojadiliwa katika muktadha wake ni VIP na SCB. Sasa Harbinder Singh Sethi na IPTL yake wametokea wapi kwenye nukuu hiyo?

TATU, PAP ilipata umiliki wa IPTL baada ya kukabidhiwa na hukumu ya Jaji Utamwa iliyotolewa Septemba 5, 2013. Sasa Agosti 19, 2013 (wakati Mkataba wa Mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP uliposainiwa) na Julai 11, 2013 (siku inayodaiwa Bw. Sethi na Bw. Rugemalira waliitwa ofisini kwa Prof. Muhongo), PAP wala Sethi walikuwa siyo wamiliki wa IPTL. Sasa Ripoti ya PAC inapodai kuwa Prof. Muhongo alikuwa kiungo kati ya Sethi wa IPTL na Rugemalira wa VIP ni UONGO uliotungwa na Kamati ya PAC na hiyo nukuu ya Mkataba imechakachuliwa kwa makusudi ili ionekane inawalenga Bw. Sethi na Bw. Rugemalira na siyo VIP na SCB kama nukuu halisi ya mkataba inavyojieleza.

Uongo Kuwa Uthibitisho na Vielelezo Alivyopata Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ni Taarifa ya Kamati ya Wataalamu

Ukurasa wa 18 wa Ripoti ya PAC unaeleza hivi:

“(ii) Kuhusu ushahidi kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya IPTL na TANESCO kuhusiana na overcapacity charges umepatiwa suluhu na imeafikiwa kwamba IPTL ilipwe fedha husika, Kamati yangu, imethibitisha kwamba hakukuwa na makubaliano kati ya TANESCO na IPTL ambao ndiyo washirika wa Akaunti ya Tegeta ESCROW. Uthibitisho huu unatokana na maelezo ya kipengele Na. 3.2 na 7.1 cha Taarifa ya Kamati ya Wataalam iliyokutana tarehe 24 Septemba, 2013 kuhusu utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW. Taarifa hiyo ya Wataalam ndiyo

7

iliyotumika kama kielelezo cha ushahidi kuwa mgogoro uliokuwepo kati ya IPTL na TANESCO kuhusiana na capacity charges umepatiwa suluhu jambo ambalo ni kinyume na yaliyomo katika kipengele 3.2 na 7.1 cha Taarifa husika (Kiambatisho Na. 9). Vipengele hivyo vinasomeka kama ifuatavyo:‐

“3.2 Discussions between TANESCO and IPTL on disputed capacity charges are ongoing, therefore, the team could not make concrete observation on this issue.”

“7.1 TANESCO and IPTL should conclude the ongoing verification of the outstanding capacity charges invoices and issues relating to it and submit a joint resolution to PS‐ MEM as soon as possible to enable other process to take off.”

Mheshimiwa Spika, Kamati imethibitisha kuwa uthibitisho na vielelezo alivyopata Gavana wa Benki Kuu katika kufikia maamuzi ni Taarifa ya Kamati ya Wataalam kama ilivyotajwa hapo juu. Hata hivyo Kamati imefanikiwa kuona nyaraka iliyosainiwa na Ndugu John Kabadi kwa niaba ya TANESCO na Mwakilishi wa Kampuni ya IPTL ya tarehe 8 Oktoba, 2013 kwamba wamekubaliana kuwa fedha zote za ESCROW zilipwe kwa IPTL mara moja. Uamuzi huu uliwasilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini tarehe 9 Oktoba, 2013. Makubaliano haya hayaonekani katika mawasiliano yoyote ya Kiserikali na badala yake Kamati iliona Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akiingia makubaliano na IPTL ya utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW (Kiambatisho Na. 10).”

Kuna tuhuma kadhaa kwenye nukuu hapo juu. Tuhuma hizi ni kama zifuatazo:

Tuhuma Na. 1 ‐‐ Hakukuwa na makubaliano kati ya TANESCO na IPTL ambao ndiyo washirika wa Akaunti ya Tegeta ESCROW

Tuhuma Na. 2 ‐‐ Kamati imethibitisha kuwa uthibitisho na vielelezo alivyopata Gavana wa Benki Kuu katika kufikia maamuzi ni Taarifa ya Kamati ya Wataalam

Tuhuma Na. 3 ‐‐ Japo inadaiwa kuwa hakukuwa na makubaliano (namba 1 hapo juu) inadaiwa kuwa kulikuwa na makubaliano yaliyofanyika kati ya TANESCO na IPTL kwenye kikao cha tarehe 8 Oktoba, 2013 ambapo makubaliano haya hayaonekani katka mawasiliano yoyote ya kiserikali

Kuhusiana na Tuhuma Na. 1, kwanza siyo kweli kuwa washirika wa Akaunti ya Tegeta Escrow ni TANESCO na IPTL. Washiriki wa Mkataba wa Akaunti ya Escrow ni Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini (kama mdhamini wa TANESCO kwenye Mkataba wa Power Purchase Agreement [PPA] na Implementation Agreement [IA]) na IPTL huku BOT akiwa kama msimamizi wa hiyo akaunti, yaani Escrow Agent.

Halafu siyo kweli kuwa kulikuwa hakuna makubaliano yoyote kati ya TANESCO na IPTL. Kikao cha Pamoja cha Uhakiki wa Malipo ya Tozo kati ya IPTL na TANESCO Oktoba 8, 2004 ulifikia makubaliano ya malipo ya capacity charges kama ilivyoelezwa kwenye Ukurasa wa 14 wa Ripoti ya CAG (Kiambatanisho Na. 1):

Kupitia kikao cha tarehe 8 Oktoba 2013 TANESCO na IPTL walikaa na walikubaliana kuhusu madai ya IPTL kama ilivyonukuliwa hapa chini “Monies in the Escrow Account be released to IPTL as soon as possible to enable IPTL sort out its legitimate creditors as per the order of the High Court (Hon. Utamwa J.) dated 5th September, 2013. All other outstanding amounts payable to IPTL be paid in accordance with the timelines proposed herein above to enable IPTL restructure its other obligations.”(Kielelezo53).

8

Na ukurasa wa 24 wa Ripoti ya CAG unasema hivi:

TANESCO na IPTL walikaa katika kikao cha tarehe 8 Oktoba 2013 na kukubaliana kuhusu madai ya IPTL ya USD 79,049,724.50(Kielelezo 53).Katika Kikao hicho TANESCO iliomba kuondolewa kwa kiasi cha USD 33,564,004.53 ambacho kilikuwa ni riba na adhabu itokanayo na malimbikizo ya tozo ya gharama za uwekezaji. IPTL ilikubaliana na ombi hilo endapo TRA ingeisamehe kodi ya kiwango sawa na hicho.

Angalia Muhtasari wa Kikao cha Pamoja Kati ya TANESCO na IPTL kilichofanyika Oktoba 8, 2013

(Kiambatanisho Na. 5)

Kuhusu Tuhuma Na. 2, hizi ni tuhuma za UONGO kabisa. Kwa mujibu wa Ripoti ya CAG inasema hivi:

“Makubaliano ya kutolewa kwa fedha baina ya Wizara ya Nishati na Madini yalifanyika kwa mujibu wa Kipengele Na. 7.7(ii) cha makubaliano ya Escrow, ambayo yaliruhusu BoT (wakala wa akaunti ya Escrow) kuilipa IPTL fedha husika (Kielelezo 21).” – Ukurasa wa 13

“Baada ya kupokea mapendekezo ya Bodi ya TANESCO kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa IPTL, tarehe 21 Oktoba, 2013 Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi pamoja na Mwanasheria wa Wizara hiyo Bi. Salome Makange kwa niaba ya Serikali waliingia makubaliano na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Harbinder Singh Sethi na Mwanasheria wa IPTL Bw. Joseph Makandege juu ya utolewaji wa fedha katika akaunti ya Escrow (Agreement for delivery of funds to Independent Power Tanzania Limited (IPTL) (Rejea Kielelezo 21).” – Ukurasa wa 24

Mkataba “Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited (IPTL)” uliosaniwa na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na IPTL, (angalia Kiambatanisho Na. 6), ndiyo uliotumika kufikia maamuzi, na siyo “Taarifa ya Kamati ya Wataalam” kama inavyodaiwa na Ripoti ya PAC. Huu nao ni UONGO.

Kuhusu Tuhuma Na. 3, ukweli ni kuwa barua yenye kumbukumbu namba SAB.88/417/01/5 ya Oktoba 21, 2013 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kwenda kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (Kiambatanisho Na. 7), ikiambatanisha “Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited (IPTL)” (Kiambatanisho Na. 6). Mkataba huu umeambatanisha Muhtasari wa Kikao cha Pamoja kati ya TANESCO na IPTL (Kiambatanisho Na. 5). Sasa kudai kuwa “makubaliano kati ya TANESCO na IPTL hayaonekani kwenye mawasiliano yoyote ya kiserikali ni UONGO usiokuwa na chembe ya uthibitisho.

Upotoshwaji wa Agenda za Mkutano wa IPTL na TANESCO

Ukurasa wa 23 wa Ripoti ya PAC inanukuliwa hivi:

“Mheshimiwa Spika, Kamati imeshangazwa na makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya Bodi ya TANESCO na IPTL, ikizingatiwa kuwa mgogoro wa msingi uliohusu madai ya TANESCO kutozwa capacity charges kubwa na IPTL haukupatiwa ufumbuzi kama ilivyoelekezwa na ICSID. Kamati imefanikiwa kuona muhtasari wa kikao cha Menejimenti ya TANESCO na IPTL kilichofanyika

9

tarehe 8 Oktoba, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam ambapo imebaini kuwa walizungumzia mambo yafuatayo:


  1. Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania chini ya Mhe. Jaji Utamwa, J iliyotolewa tarehe 5 Septemba 2013


  1. Uhamishaji wa mali za IPTL ikijumuishwa Mitambo ya kufua Umeme na madai ya fedha za IPTL kwa TANESCO yaliyowekwa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW kwenda kwa PAP.


  1. Madai ya ziada ya IPTL kwa TANESCO kama yalivyoainishwa hapo juu.

Mheshimiwa Spika, hakukuwa na uthibitisho kuwa walizungumzia suala la kutafuta maridhiano kuhusu madai ya TANESCO kutozwa capacity charges kubwa ili kuwezesha kutolewa kwa fedha zilizokuwemo kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW ingawa inaonyesha kwenye mawasiliano mbalimbali yaliyofanyika kati ya Serikali, TANESCO na IPTL walikuwa wanajua kuwa wanapaswa kufanya maridhiano katika suala husika.”

KWANZA, kuna upotoshwaji wa agenda/issues zilizojadiliwa katika kikao cha pamoja kati ya TANESCO na IPTL. Kwa mujibu wa Muhtasari wa Kikao hicho (Kiambatanisho Na. 5) agenda/issues zilizojadiliwa ni hizi hapa:


  1. AGENDA/ISSUES FOR DISCUSSION


  1. Capacity Charges


  1. Interests and Penalties on Outstanding Capacity Charges


  1. VAT on Capacity Charges


  1. Equivalent availability factor Bonus


  1. Supplemental Charges


  1. Pre‐shipment costs


  1. EWURA Levy


  1. City Service Levy


  1. Workers Welfare Fund (NSSF)


  1. The gas conversion meeting expense


  1. Mode of Paymen & Duration

Kamati ya PAC iliamua kuchukua paragraph ya Introduction ya Muhtasari wa Kikao cha Pamoja cha TANESCO na IPTL na kuzigeuza kuwa agenda za kikao na kuzitupilia mbali ajenda khasa za kikao hicho kama zilivyoelezwa kwenye muhtasari wa kikao. Hii ni wazi hapa Kamati ya PAC ilikuwa inafanya hila kwa makusudi kabisa kuficha ukweli na kudanganya Bunge na Umma wa Watanzania kwa ujumla.

PILI, Kamati ya PAC pia inatumia hila na ujanja wa kurudiarudia kueleza kuwa kulikuwa hakuna maridhiano kuhusu madai ya TANESCO. TANESCO inapo‐dispute (kutokubaliana) na Capacity Charges halafu baada ya kikao cha pamoja ikaridhia kulipa hizo capacity charges, tayari hayo ni maridhiano. Sasa sijui maridhiano yepi ambayo Kamati ya PAC inataka yawepo ili kuwaridhisha wao.

Uongo wa Nukuu ya Barua ya Mwanasheria wa TANESCO

Ukurasa wa 22 wa Ripoti ya PAC inasema:

10

“Mheshimiwa Spika, katika barua ya Mkuu huyo wa Sheria wa TANESCO kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji yenye Kumbukumbu Na. SEC.427/IPTL/11/2013 ya tarehe 7 Novemba, 2013 alisema:

“Nilishuhudia nyaraka kwamba Piper Link ilinunua hisa za Mechmar na katika mauziano hayo Kampuni hiyo iliwakilishwa na Bw. Harbinder Singh Sethi hivyo huyu bwana ndiye Piper Link na ndiye PAP”

Hata hivyo, Bodi ya TANESCO haikukubaliana na ushauri huo na hatimaye kumwachisha kazi Bwana Godwin Ngwilimi. Kosa lake kubwa ni kutahadharisha kuwa nchi inatapeliwa. Kama ushauri huu ungefuatwa tusingefika hapa tulipo leo kwa sababu hadi hapa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW zilikuwa hazijatolewa.”

Tuhuma zote za Ripoti ya PAC kama zilivyonukuliwa hapo juu ni tuhuma za UONGO. Kuna vitu kadhaa vya kuangalia hapo.

KWANZA, hiyo barua yenye kumbukumbu Na. SEC.427/IPTL/11/2013 ya tarehe 7 Novemba, 2013 (Kiambatanisho Na. 8) ni barua yenye kurasa tatu ambayo haina maneno yoyote siyo tu yanayoweza kutafsiriwa kama ilivyonukuliwa na Ripoti ya PAC bali haina maneno yoyote yanayokaribia na maana ya maneno yaliyonukuliwa na Ripoti ya PAC. Nukuu ya maneno kutoka kwenye barua hiyo ni nukuu ya UONGO.

PILI, hiyo barua haina “ushauri”wowote uliokuwa tofauti na ule ushauri wa Kamati ya Wataalam kutoka BOT, Wizara ya Fedha, Wizara ya Madini na Nishati, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na TANESCO. Madai ya kuwa TANESCO haikukubaliana na ushauri wa mwanasheria huyo ni UONGO.

TATU, barua ya mwanasheria huyo iliandikwa Novemba 7, 2013 na Mkataba wa Agreement for Delivery of Funds to IPTL (Kiambatanisho Na. 6) ulifanyika Oktoba 21, 2013. Sasa inakuwaje Bodi ya TANESCO ituhumiwe kutokubaliana na ushauri ambao uliwasilishwa baada ya zaidi ya wiki mbili tokea maamuzi yafanywe na bodi?

Isitoshe mwanasheria huyo alienda nchini Malaysia kati ya tarehe 14 na 20 Septemba 2013 na ripoti ya safari yake aliwasilisha Novemba 7, 2013 yaani siku 48 baada ya kurejea kutoka safarini.

NNE, pamoja na kuandika nukuu za UONGO kutoka kwenye barua ya mwanasheria wa TANESCO, Ripoti ya PAC imetoa tuhuma za mwanasheria huyo kufukuzwa kazi bila ya ushahidi wowote. Katika hotuba yake ya majumuisho ya mjadala, Mwenyekiti wa PAC alibadilisha tuhuma za mwanasheria wa TANESCO kufukuzwa kazi na badala yake akaeleza kuwa eti mwanasheria huyo alitishiwa kifo na hatimaye alilazimishwa kuacha kazi. Hii ni baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kuwathibitishia kwa nakala ya barua ya kuacha kazi ya mwanasheria huyo wa Tanesco. Mwenyekiti huyo wa PAC pia alidai kuwa taarifa za vitisho alivyokuwa anavipata mwanasheria huyo viliripotiwa polisi. Pamoja na kuwa tuhuma zilibadilishwa “hadithi” bado Mwenyekiti wa PAC hakuona umuhimu wowote wa kuwasilisha ushahidi wowote wa madai yake hayo mapya. Hizi tuhuma za UONGO na ndiyo maana hadithi imekuwa ikibadilika.

11


Orodha ya Viambatanisho


Kiambatanisho Na. 1 – Ripoti ya CAG (Taarifa ya Ukaguzi Maalum Kuhusiana na Miamala Iliyofanyika Katika Akaunti ya “Escrow” ya Tegeta, Pamoja na Umiliki wa Kampuni ya IPTL) http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/01_Report_CAG.pdf

Kiambatanisho Na. 2 – Ripoti ya PAC (Taarifa ya Kamati Kufuatia Matokeo ya Ukaguzi Maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Akaunti ya Tegeta Escrow Iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania)

http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/02_Report PAC.pdf

Kiambatanisho Na. 3 – Decision on Jurisdiction and Liability of ICSID Case No. ARB/10/20 http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/03_ICSID_Decision_On_Jurisdiction_And_Liability.pdf

Kiambatanisho Na. 4 ‐‐ Mkataba wa Mauzo ya Hisa kati ya Kampuni ya PAP na VIP http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/05_Meeting_Minutes_IPTL_And_TANESCO.pdf

Kiambatanisho Na. 5 – Muhtasari wa Kikao cha Pamoja Kati ya TANESCO na IPTL kilichofanyika Oktoba 8, 2013 http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/05_Meeting_Minutes_IPTL_And_TANESCO.pdf

Kiambatanisho Na. 6 – Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited (IPTL) http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/06_Agreement_For_Delivery_Of_Funds.pdf

Kiambatanisho Na. 7 – Barua kutoka kwa Katibu wa Wizara ya Nishati na Madini kwenda kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (Kumbukumbu Na. SAB.88/417/01/5) http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/07_Letter_From_PS_MEM_To_Governor.pdf

Kiambatanisho Na. 8 – Barua kutoka kwa Bw. Godwin Ngwilimi kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Kumbukumbu Na. SEC.427/IPTL/11/2013 ya tarehe 7 Novemba, 2013 http://www.orcis.com/escrow/viambatanisho/08_Letter_From_TANESCO_Lawyer.pdf


12

Kwa viambatanisho vyote vilivyotajwa na chanzo. Bofya hapa: Index of /escrow/viambatanisho


Maoni haya yanahitaji kupembuliwa na CAG
 
Hivi umeshapitia yote yaliyoandikwa na kupitia viambatanisho kwa dakika mbili tu? na kuja na majibu ya jumla jumla kuwa ni maigizo? hebu kuwa mkweli wa nafsi yako.

Sasa nieleze lipi ni igizo na kwanini ili nilipitie, usije na hoja za kuponda jumla jumla kabla hata hujasoma, unajishushia hadhi na uelewa wako.

Kweli faizafox unazeeka vibayaa ishu ya escrow imeshahamuliwa na imeshaifedhehesha serikali kimapata na bado tu mnazidi kuwaaminisha watu uongo ufai kabisa wewe.
 
Huu ni Ujinga tu! tunaomba Orodha ya waliopewa pesa kupitia Bank ya Stanbic, mimi nilidhani utatuambia hili kumbe bado ni ngonjera zile zile za mwaka jana?

Wabongo mkilishwa uongo na wasaka tonge, huwa hamjishughulishi tena kutafuta ukweli! nyie ni kupelekeshwa tu kama ng'ombe eti kuunga mkono chadema baasi!
 
Kweli faizafox unazeeka vibayaa ishu ya escrow imeshahamuliwa na imeshaifedhehesha serikali kimapata na bado tu mnazidi kuwaaminisha watu uongo ufai kabisa wewe.

Hizo zako ni porojo zisizo na hoja.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom