Aliyefukuzwa kazi ni mmoja tu na si kwa wizi, kumbuka hilo, kafukuzwa kwa ujinga wake wa kushindwa kufata kanuni za maadili ya kazi.
Mengine yote uliyosema ni porojo za hapa na pale, pitia ripoti vizuri uelewe ukweli ulivyo.
Ni lini lilikwisha? wakati hata Rais alisema uchunguzi wa kina utafanyika, na bunge limeomba uchunguzi wa kina ufanyike, umesahau? jee, ulishatangaziwa kuwa uchunguzi umekwisha? Fikiri.
Escrow hakuna wizi, sijaona mpaka aliyenyooshewa kidole kuwa kaiba.
Ni nani?
PAP inaendelea kuzalisha umeme na wanalipwa kila mwezi toka account ya escrow ifungwe, jee, unalijuwa hilo?
kwa nchi hii sio ajabu kama mpaka sasa bado wanamtafuta mtu aliyemuua Mwangosi wakati mkanda unaonyesha wazi jinsi anavyolipuliwa na bomu, ila iko siku mamboyote hayo yatakwisha kwani hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. hizi ni busara zetu sisi kina gogo la shamba
Yaelekea wewe umeishakuwa msemaji wa ikulu na ndio wanaotoa porojo kama hizi unazoziandika hapa,huo uchuguzi unaousema mbona raisi aliomba muda afanye uchunguzi wake na akafikia utoa hotuba kwa wezee wezio pale Diamond Jubilee?,kama uchunguzi haukufanyika yeye alikuwa anatoa uamuzi kwa misingi gani?,Aliyefukuzwa hakuiba,kwa mtazamo wako Fine! alikiuka maadili gani na yanayohusu nini?,hakuna kufikiri hapa,muda wa kuwaongopea wananchi umekwisha na mtapambana na upinzani mkubwa tu mbele ya safari.
Na aliyeko ndani na kwenda mahakamani kila siku hujaona? wewe kweli umelala doroooo.
Mahakama ndio jela au alioko mahakamani tangu lini ukaambiwa ana kosa kweli wewe ndie uliolala sisi kina gogo la shamba ni wasema kweli wala usije hata siku moja ukafikiria tuna upendeleo na mtu au chama kama unasikia tunawasema ccm ni kwa ubaya wao, wala ingawaje tunajali mawazo ya watu makini
Wewe hata sikuelewi mantiki yako wala maandiko, yako na huyo ndiyo kachota fedha za escrow?
Ulitaka umeme wa bure?
Siku si nyingi utaliwa tigo na wanaokutumia
Tazama post yangu nimebandika saa ngapi na dakika ngapi? na post yako umebandika saa ngapi na dakika ngapi? kwa dakika mbili tu, usome, uangalie vielelezo, na urudishe majibu?
Hapana, si kweli.
Kuwa mkweli wa nafsi yako. Usijidanganye.
Hivi umeshapitia yote yaliyoandikwa na kupitia viambatanisho kwa dakika mbili tu? na kuja na majibu ya jumla jumla kuwa ni maigizo? hebu kuwa mkweli wa nafsi yako.
Sasa nieleze lipi ni igizo na kwanini ili nilipitie, usije na hoja za kuponda jumla jumla kabla hata hujasoma, unajishushia hadhi na uelewa wako.
Faiza Foxy jaribu angalau kidogo kufungua ubongo na akili yako, think out of this ''CCM box''. Tatizo lako hadi akili yako imejaa U-ccm, sasa yanapokuja maswala ya msingi unapata shida sana kutenganisha lipi ni CCM na lipi ni swala la msingi la maendeleo. Watuhumiwa wote wanakiri kupokea fedha, wanashindwa kuelezea umma ni fedha za nini, hadi sasa hakuna hata mmoja aliyetoa maelezo ya maana, wewe bado tu unataka kuwasafisha. Acha fikra mgando.
Kizazi chako kitapata tabu sana
Sikuelewi unachotaka kukisema haswa ni nini, naona unahororoja bila mpango.