Escrow: Je, Watanzania ni ignorant au tumelogwa? Tuache cherry-picking kutafuta Mbuzi wa Kafara!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Preamble
Mtu mwenye akili na mwenye busara, anapojikwaa na kuanguka, anaangalia mahali alipojikwaa, ili kuipata sababu iliyomfanya ajikwae na kuanguka, badala ya kuangalia alipoangukia tuu, anaamka na kuendelea na safari yake, hivyo huko mbele atakuja kujikwaa tena pale pale alipojikwaa mwanzo na kuanguka tena na tena!".

Fedha za escrow account ni matokeo tuu sio chanzo, tena fedha zenyewe ni kiduchu tuu ukilinganisha na fedha zote zinazomezwa na hili lidudu li IPTL, lakini watu wanashupalia matokeo badala ya kujiuliza chanzo!. Huu kama sio ujinga, yaani ignorance, ni nini hiki?!.

Watanzania ni Ignorants; yaani Sisi Watanzania ni Wajinga?
Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "ma-ignorants!", yaani wengi wetu ni watupu kabisa vichwani mwetu au ni weupe tii!, na wengine wetu ni vichwa maji kabisa!, uwezo wa kufikiri "logical thinking", wa wengi wetu ni mdogo au sifuri, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya maana, "to make informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe au mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi na kushupalia vitu vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo tuu, badala ya kudeal na issues halisi zenyewe ambazo ndicho chanzo, cha haya madhila, kilichopelekea haya yatokanayo, yatokee, vyanzo haviuliziwi, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi!, tuna deal na matokeo tuu!, huu kama sio ujinga ni nini?.

Ujinga Huu wa Watanzania, Kutojiuliza Chanzo cha Tatizo Umeanzia Wapi na Uko Wapi?
Hii ignorance ya Watanzania ina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya Bunge letu tukufu, tuna wabunge mule ni vilaza na ma ignorants wa ajabu hakuna mfano!, tuna viongozi wetu wengi tuu ni ma ignorants hadi ndani ya cabinet yetu kuna mawaziri ni ma ignorants kabisa!, uthibitisho ni jinsi mawaziri wetu wanavyotimuliwa kila ukicha, from time to time!, tuna viongozi wa taasisi za umma ambao ni ma ignorants na jambo kubwa na la ajabu, tuna hadi viongozi wetu wakuu wa taasisi nyeti hadi wakuu wa vyombo vya dola, ambao nao ni ma ignorants tuu kama ma ignorants wengine, na sisi wana jf pia, wengi wetu ni ma ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, mwenzenu Paskali, pia ni ignorant!, tofauti kati ignorance yangu na ma ignorants wengine, mimi ni ignorant ambaye ninajitambua kuwa ni ignorant , hivyo pamoja na ignorance uliyonayo ukiisha jitambua na kuusema ujinga, unakitoka, lakini wengi wa ma ignorants wenzetu, hukaa kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu ya kuogopa kuongea, tunaongea wazi wazi hivyo tunaionyesha hiyo ignorance yetu kwa uwazi kabisa kwa ku speak out our minds and expressing our opinions ignorantly.

Je, Ujinga Huu ni Mtaji?
Yes ujinga ni mtaji!. Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kimekuwa kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura ubwete za ushindi, mwaka hadi mwaka, na mwakani tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.

Kwa Nini Mtu Uwaite Watanzania Wenzako Kuwa ni Wajinga?
Naomba kuweka wazi kuwa kwenye bandiko hili, sijatukana mtu, wala sijawaita watu ni wajinga, bali nimeuliza tuu swali kuwa, Jee Sisi Watanzania ni Wajinga?. Majibu ya swali hili ndiyo yatakayosema kama sisi ni ma ignorants au la!, kama ni ma ignorants, huu ujinga wetu ni ujinga wa aina gani au tumelogwa?. Maswali haya ni kufuatia kujiuliza, haiwezekani kabisa, kwa watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ovyo ya ajabu ajabu kama haya, lakini inapofikia wakati wa kuwapima hao waliowachagua, bado wakawachagua watu wale wale, chama kile kile, na baadae kuja kufanyiwa madudu yale yale!.

Jee Hali Ilikuwa Hapo Mwanzo, Ukilinganisha na Hali Ikoje Sasa?
Wakati tulipopata uhuru toka kwa mkoloni, Tanzania tulikuwa na maadui wakuu watatu, ujinga, umasikini na maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru, sio tuu, bado tunao wale maadui wakuu watatu bali sasa, ujinga umeongezeka mara dufu!, umasikini sasa ni uliotopea!, na maradhi yamezidi hadi mengine ni janga la taifa kwa sababu hayana tiba!. Kila siku ni afadhali ya jana!. Wazee wa sasa wanasema, hali ilivyo sasa ni mbaya hadi kujiona zamani enzi za mkoloni ni afadhali kuliko sasa!. Kitu kibaya zaidi, ni sasa tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, na sasa Escrow.

Uzuri wa Watanzania ni Upi Katika Kukumbatia Umasikini, Ujinga, Maradhi, Rushwa na Ufisadi
Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa tunawapa serikali za mitaa!, mwezi April tuna wapitishia ile "Bora Katiba" kwa kura za ndio za kutosha, na zisipotosha "zitatosheshwa!",na October, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

Ignorance Kwenye Mjadala wa Escrow
Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, fedha ya escrow ni matokeo tuu ya hili jinamizi linaloitwa IPTL!, hakuna anayezungumzia chanzo, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye hiyo account ya escrow ni fedha ndogo ya capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni kwa mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, Aggreko, Simbion, Songas!, badala ya watu kujadili chanzo, na kwa nini tumefika hapa, wao wanajadili matokeo tuu!. Hii kama sio ignorance ni nini?!.

Kwanini Tufanye Cherry Picking Kwenye Kutafuta Mbuzi wa Kafara?!.
Katika kuwabaini wahusika, wa hili jinamizi la Esscrow, badala ya kuwatafuta wahusika wakuu waliosababisha tufike hapa, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia kabisa BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa kwa PAP ambaye has got nothing to do with account hiyo kabla ya kwanza kujiridhisha?!.

Je, Escrow Ndio Issue Sana Kivile? Au Issue ni IPTL? Mbona Mnashupalia Matokeo Badala ya Chanzo?!
Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo chakavu ya mtumba, inayotumia obsolete technology?, ilikubalikaje na kupitishwaje bila ripoti ya EIA?. Sisi kama Taifa, tulikubalije kutozwa capacity charges za kiasi kile kwa mitambo ile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.

Kwanini Watu Wanataja Taja Tuu Majina? Huu Kama Sio Ujinga ni Nini?!
Watu wanataja taja tuu majina!, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".

Paskali

Nianze na hili Angelico: Mie sio mshabiki wa Pasco na wala sikubaliani naye katika mijadala mingi.

Tujikite hasa katika ujumbe aliouandika bila kujali amesoma kiasi gani, namna ya uandishi wake na mengine yahusiano na mapungufuku yake Kitaaluma. Sote tukiri kwamba elimu yetu chini ya CCM imekuwa ikishuka ubora Kadri miaka inavyokwenda mpaka sasa watoto wetu wana pata "bora elimu".

Hakuna mahali aliposema tuachane na issue ya Escrow mbele yetu.

Nilivyomwelewa ujumbe wake ni kwamba tukishafanya hii short term decision ya kuadhibu wezi wa escrow, tusiishie hapo tukidhani tatizo limetatuliwa. Tuende mbali zaidi na kuchunguza kwa undani chanzo cha IPTL. Hivi sasa tunavyojadili kuna watoto wa IPTL ambao wamekomaa mfano Aggreko, songas, Richmond (aliyevunja ungo kuwa Dowans aliyejifungua Symbion).
Wote hao wanalipwa na Tanesco millions of dollars kila kukicha.hii ya Escrow inawatisha Watanzania kwa kuwa ni large amount accumulated over 10 years. Anachosema Pasco ujinga wetu hakuna hata mmoja bungeni, wanasiasa na media anayehoji kwa undani zaidi hili suala la Energy security na future yake.
Kutokana na uzoefu wake hapo Tanzania ukijumuisha na ufahamu wake wa hili tatizo anachosema Pasco (atanisahihisha) njia pekee ya kuanza kutatua ni kwa kuitoa CCM madarakani, period. Namna ya kuweza kuitoa madarakani bila kuacha nchi isiparanganyike kwa scars za kudumu ni kupitia Sanduku la Kura siku ya uchaguzi.
Tunafahamu wajinga wapo kila nchi sema kwa Tanzania (tofauti na nchi zilizoendelea) ujinga umeota mizizi katika kundi la "waliosoma".Hawa wasomi wanaonyesha ujinga wao pale wanaposhindwa kujipanga na kuitoa ccm madarakani kipindi uchaguzi unapofika. Mifano hai aliyoiongelea ni hizi chaguzi zinazokuja hapa mbeleni. Kura zinapigwa na zinaibiwa au kutosheshwa na wasomi Hawa wanabaki kulalama kama hivi sasa.

Sasa Pasco anapojaribu kusema tatizo ni sisi, tunamchukia na kusema mchumia tumbo. Nani huyo aishie nje ya Tz asiyemchumia tumbo? (Asiejali zaidi familia yake binafsi kupata huduma nzuri za afya na elimu bora).
Tanzania itabadilika pale tu wasomi wanaojali na kuheshimu utu watakaposhirikiana na likeminded citizens kuiondoa ccm madarakani.

Tujifunze kwa Waingereza, PM Winston Churchill pamoja na kuipigania UK kuishinda Germany kuonyesha strong leadership lakini ilipofikia uchaguzi wananchi walimpiga chini. Walitambua different challenge ya ku rebuild UK requires different way of thinking and mentality. Churchill standing haijawa undermined whatsover. Nas hatuna budi kuwaambia ccm sawa ukombozi umepita sasa ni challenges nyingine.

Nawasilisha.
 
Kwa mwandishi wa habari na mtu ambaye unadai umesoma sheria UDSM, sijawahi kuona mwandishi mbovu kama wewe!

Kanuni nyepesi tu za uandishi zinakushinda. Mjinga nambari moja utakuwa ni wewe.

Unaweka alama za nukuu hata pasipotakiwa. Unarudia rudia maneno yaleyale uliyoyaandika katika lugha moja na kuyaandika katika lugha ingine.

Hivi una matatizo gani wewe?
 
Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, ni matokeo tuu, hili hili jinamizi linaloitwa IPTL, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye account ya escrow ni capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni na mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, watu hawajadili chanzo, wanajadili matokeo tuu!.

Katika kuwabaini wahusika, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa PAP?!.

Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo ya mtumba, obsolete technology, ilikubalikaje kukubali kutozwa capacity charges zile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.

Pasco

Pasco.
Lakini si wewe unashindia kwenye mitandao kila siku kuwabeza wapinzani? Unapokosa posho za magamba unaungana na wapinzani. Wanapokupa mnofu unawabeza wapinzani. Hutabiriki. Wewe ni ndumila kuwili! Nadhani wewe ndiye mjinga namba moja!
 
Pasco...you are too obsessed, hadi kuwaita wana JF wote wajinga:A S-rap::A S-rap::A S-rap: .

Mkuu,kwa hili la ESCROW ni kosa tayari,wezi lazima wakamatwe.

Na hayo makosa mengine ya IPTL Yatashughulikiwa...kumbuka tunawafukuza PAP hapa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Pasco, ndugu yangu hizi ni siasa, za ujanaujanja wa serikali kutuondoa kwenye issue ya katiba.

Hivi tangu hili linaanza mpaka mkaguzi wa hesabu za serikali anaingilia kati Muhongo na utetezi wake alikuwa wapi na asitwambie watanzania ukweli?

Sioni namna ya watu kuwajibika hapa. Nimesikia baadhi ya wabunge wakimsifu J Rugemalira kwa kulipa kodi, kama ndivyo wanaonekanaje waliopewa pesa na JR kuwa ni wezi na leo mnataka wawajibike? Hapa kuna michezo inachezwa.

Je! Serikali kama iliyajua yote haya muda wote wakati wabunge wanaumana ndani ya Bunge ilikuwa wapi kuondoa sintofahamu? Inawezekanaje siku zote hakukuwa na majibu na leo ndiyo kuna majibu katika jambo lilelile la siku zote?
 
hivi Pasco tukueleweje?umekuja hapa juzi na uzi wa kudai hakuna wa kuwajibika kwenye hili,jana tena ukaingia na uzi haiwezi kujadiliwa kwa sababu mahakama imekataa,leo tena unadai Watanzania ni mambumbumbu,sasa tukueleweje kama mwandishi Professional?nafikiri huna uwezo wa kuangalia ulichokisema hapo nyuma kabla hujaja na story mpya,kwa ujumla wewe ndiye hasa una reflect watanzania uliowaongea pale juu
 
Pasco, unachosema ni kweli. Na haya yamejidhihirisha pale bungeni.

1.Wajumbe wengi wanasema CAG amesema fedha zile ni za umma. Wakati taarifavya CAG inasema inawezekana fedha zile zikawa ni za umma.

2. Kafulila anasema fedha ya escrow account imeibiwa bil 306. Taarifa zinasema kuwa fedha zilizopotea kama kodi ni bil 8.6, waziri wa fedha anasema bil 21. Wengine wanasema bil 326...na hawa ni wabunge wetu

3. PAC imesema fedha zimeibiwa. Umma sasa umeachwa njia panda. Kila mmoja na lake.

4. Kama sisi katika wingi wetu kama watanzania si wajinga ni akina nani?

Pasco, nakuunga mkono
 
Pasco ...wamekuzingua kukulipa Hawa watu wa Escrow? Mbona havishabihiani na thread yuko ya kuikandia PAC jana wakati wame extract kutoka report ya CAG?
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe!, uwezo wa kufikiri ni sifuri "logical thinking", ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi vitu vidogo vidogo na kuvishupalia vitu ambavyo ni non issues, wakati vitu ambavyo ni issue zenyewe zilizopelekea yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi!.

Hii ignorance ya Watanzania iina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila secta ya jamii ikiwemo hadi ndani ya bunge letu, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ni ma ignorants hadi ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma ni ignorants, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ni ma ignotants, na wana jf wengi pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, Pasco wa jf, tofauti na wengi maignorants wenzetu, wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine tunaionyesha hiyo ignorance yetu kwa ku speak out! na expressing it, tatizo, ni in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!,

Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM),kinaitumia ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia ushindi, na mwakani tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!, kwa sababu haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu kama tulipopata uhuru, tulikuwa na maadui watatu, ujinga, umasikini na maradhi, leo miaka 50 baada ya uhuru, sio tuu ujinga, umasikini na maradhi vimeongezeka afadhali ya zamani, bali tumeongeza maadui, wakiwemo rushwa na ufisadi, ulituletea EPA, Richimond, na sasa Escrow, kitu cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini watu wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti, hii ni nini kama sio ignorance at the highest level!, na April tutaipitisha "Bora Katiba" kwa kura za ndio, na kura za ndio zisipotosha "zitatosheshwa!", na October, tutairudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, ni matokeo tuu, hili hili jinamizi linaloitwa IPTL, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye account ya escrow ni capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni na mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, watu hawajadili chanzo, wanajadili matokeo tuu!.

Katika kuwabaini wahusika, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa PAP?!.

Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo ya mtumba, obsolete technology, ilikubalikaje kukubali kutozwa capacity charges zile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.

Watu wanataja taja majina tuu, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".

Pasco

Pasco.
mkuu mbn husomeki unaleta.....
 
Tatizo ni watawala hasa spika,mawaziri,police na usalama wa taifa.Mtu akianza kutuelekeza wapi thmekosea huwa wanamua,kumtoa kucha,kumpiga nk.Angalia jana Tindu Lisu alianza vizuri kutuongoza akajatokea Mery Nagu akazuia.
 
Mi nadhani Pasco hajui anachotakusema au anataka kila mtu afikirie kama anavyotaka. Lakini si yeye tu wengi wetu humu tumekua hatutaki hoja wala kusikia chochote tusichotaka kusikia au kilicho kinyume na misimamo yetu.

Nadhani kuna haja ya kubadilika, sisemi tusikosoane bali ifanyike kwa hoja. Si mtu anatoa hoja anaishia kutukanwa. Kiufupi tusiendeshe jukwaa kwa hisia kama lilivyo bunge ili mpiga kura akuone bali tutumie hoja.

Faida ya hisia (emotion) ni ya haraka kuliko uhalisia(logic) ila madhara ya hisia ni ya muda mrefu kuliko uhalisia.
 
Kwa mwandishi wa habari na mtu ambaye unadai umesoma sheria UDSM, sijawahi kuona mwandishi mbovu kama wewe!

Kanuni nyepesi tu za uandishi zinakushinda. Mjinga nambari moja utakuwa ni wewe.

Unaweka alama za nukuu hata pasipotakiwa. Unarudia rudia maneno yaleyale uliyoyaandika katika lugha moja na kuyaandika katika lugha ingine.

Hivi una matatizo gani wewe?

Asante.....spinning zinakera kweli .......
 
Wanabodi,

Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe!, uwezo wa kufikiri ni sifuri "logical thinking", ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi vitu vidogo vidogo na kuvishupalia vitu ambavyo ni non issues, wakati vitu ambavyo ni issue zenyewe zilizopelekea yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi!.

Hii ignorance ya Watanzania iina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila secta ya jamii ikiwemo hadi ndani ya bunge letu, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ni ma ignorants hadi ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma ni ignorants, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ni ma ignotants, na wana jf wengi pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, Pasco wa jf, tofauti na wengi maignorants wenzetu, wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine tunaionyesha hiyo ignorance yetu kwa ku speak out! na expressing it, tatizo, ni in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!,

Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM),kinaitumia ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia ushindi, na mwakani tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!, kwa sababu haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu kama tulipopata uhuru, tulikuwa na maadui watatu, ujinga, umasikini na maradhi, leo miaka 50 baada ya uhuru, sio tuu ujinga, umasikini na maradhi vimeongezeka afadhali ya zamani, bali tumeongeza maadui, wakiwemo rushwa na ufisadi, ulituletea EPA, Richimond, na sasa Escrow, kitu cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini watu wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti, hii ni nini kama sio ignorance at the highest level!, na April tutaipitisha "Bora Katiba" kwa kura za ndio, na kura za ndio zisipotosha "zitatosheshwa!", na October, tutairudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, ni matokeo tuu, hili hili jinamizi linaloitwa IPTL, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye account ya escrow ni capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni na mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, watu hawajadili chanzo, wanajadili matokeo tuu!.

Katika kuwabaini wahusika, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa PAP?!.

Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo ya mtumba, obsolete technology, ilikubalikaje kukubali kutozwa capacity charges zile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.

Watu wanataja taja majina tuu, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".

Pasco

Pasco.

sijawahi changia thread ulizoanzisha. Ila unaonaekana ni mtu mshenzi mshenzi usiyeelewa nini unataka. hivi unalipwa shilingi ngapi kwa kuandika kama unaandikia m.k.u.n.d.u.
 
Tatizo kubwa la watanzania nadhani ni elimu. Wanao tumia mitambo kama hii ya jamiiforums ni wachache kulingana na idadi ya watanzania.
Waliokua vijijini huko ndio kabisa hawajui kwanini wanaichagua ccm na wala hawajui sera za vyama vingine
Nakumbuka tulikua tunaichukia sana soma la siasa shuleni lakini ni muhimu kwa kweli kujua angalau robo ya siasa. Masuala mengi yanayo fanyika ndani ya serikali, masuala ya umma tunapaswa kujua ingawa si rahisi kujua kila kitu. Vyama vya upinzani vinatakiwa wavijue kila kinacho pangwa na chama tawala yaani masuala ya umma kwani kila shilingi itakayo tumika ni hela za umma, tuna haki ya kujua, vyama tawala wana haki ya kujua budget yote, wajue kila shilingi itakayo tolewa na mipango ya hizo hela.
Mfano utaskia kuna jengo linajengwa, hospitali au soko. ghafla itatolewa budget ilio tumika ikiwa mara 20 ya budget ya halali, Inamaana hapo mafisadi wamechakachua mehesabu na kuongeza mara 20. na bado ukasikia majengo hayaja kwisha kwa sababu ya ukosefu wa hela. Hapo ndio inapotakiwa vyama vya upinzani kujua hilo suala la ujenzi kabla hela hazijatolewa na kuangalia je haya mahesabu yanaendana.
Sweden wamefanya uchaguzi mwaka huu mwezi wa 9 na hadi leohii kuna matatizo juu ya budget kwani kila chama tawala kinapo weka budget juuya meza, vyama vya upinzan vina pinga, inamaana hiyo budget kila chama wanavyomkonini hiyo budget. Wana votei nakuangalia vyama vingapi vinakubaliana. Na kila mkoa vyama vya upinzanivinafuatia na kuangalia budget inavyotumika. Na kama kuna masula mapyayataongezeka kama vile majengo basi kila chama watapata habari na kuangaliakama mambo yako sawa.
Na Hapa TZ tunatakiwatuwe hivyo. Hapo ndio ufisadi utakapo tokomea lasivyo vyama vya upinzani naowale kwenye sahani mmoja na chama tawala na kuzichota hizo hela. Na leo hiiyasingetokea haya masuala ya ESCROW. Na kama yangetokea yange gundulika katikastage ya kwanza kabisa kabla hela hazija tolewa.
 
Hakuna mtu mshenzi mshenzi duniani. Yupo mjinga mjinga. Ila yupo mtu Mshenzi.

sijawahi changia thread ulizoanzisha. Ila unaonaekana ni mtu mshenzi mshenzi usiyeelewa nini unataka. hivi unalipwa shilingi ngapi kwa kuandika kama unaandikia m.k.u.n.d.u.
 
wewe hizo pesa za kwenye escrow account prof.benno ndulu ambaye ni gavana alishashtukia mchezo na alitaka executive order kutoka ofisi kuu ikulu na raisi ndiye aliyetoa executive order.jamani hamsikii hata nyaraka zinazosomwa kuna zingine zimezuiwa ili kumlinda raisi alie juu ambae ndie mwizi mkuu.pia account moja ya mkombozi wamegoma kuisoma ambayo ndio ilikuwa na mgao wa jumla. pia stanbic bank taarifa zake zimefichwa ni wazi raisi akitajwa basi ni mtikisiko wa nchi.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom