Escrow: Je, Watanzania ni ignorant au tumelogwa? Tuache cherry-picking kutafuta Mbuzi wa Kafara!

Kwa mwandishi wa habari na mtu ambaye unadai umesoma sheria UDSM, sijawahi kuona mwandishi mbovu kama wewe!

Kanuni nyepesi tu za uandishi zinakushinda. Mjinga nambari moja utakuwa ni wewe.

Unaweka alama za nukuu hata pasipotakiwa. Unarudia rudia maneno yaleyale uliyoyaandika katika lugha moja na kuyaandika katika lugha ingine.

Hivi una matatizo gani wewe?

Pasco is a dickhead! Pretender,
 
Yaah PASCO kwa unacho ongea ni sahihi kabisa kwani wengi wa wananchi ni Ignorants na hawataki kufunguka kwa wanacho kiona na kusikia ila kwa hili tuna hiachia serikari yenyewe na bunge lake ili tujionee kitakacho tokea maana hiyo serikari si ndiyo inayo tuongoza sisi na hao waliochukua hizo hela wapo ndani ya hiyo serikari.Ok basi tuangalie mpaka mwisho wa hayo malumbano yao ili tuone kama wanaendelea kutufanya maboya au wameelimika kwa hili
 
Heshima mbele mkuu, mabandiko yako mengine kuhusu saga la escrow yanachanganya lakini ninaelewa wapi unataka tujiegemeze, Lisu alieleza vizuri, 1994 alienegotiate na kuitambua IPTL ni mkuu wa kaya akiwa maji, nishati na mdini, 1995 akiwa fedha, 2014 akiamuru fedha zitoke kwa ushauri wa AG, bunge hili suala wamegoma kabisa lisijadiliwe maana yake nini? Wananchi hatutaki kabisa kujiongeza? Hatuwezi kuungana na wale wachache wanaotutetea? Hebu tuamke uchunguzi mara ngapi? Tutaifishe IPTL na H.S. Seth akamatwe kama PAC ilivyoazimia kabla ya saga kuanza kujadiliwa. KWELI ITUWEKE HURU.
 
wewe hizo pesa za kwenye escrow account prof.benno ndulu ambaye ni gavana alishashtukia mchezo na alitaka executive order kutoka ofisi kuu ikulu na raisi ndiye aliyetoa executive order.jamani hamsikii hata nyaraka zinazosomwa kuna
zingine zimezuiwa ili kumlinda raisi alie juu
ambae ndie mwizi mkuu.pia account moja ya
mkombozi wamegoma kuisoma ambayo ndio
ilikuwa na mgao wa jumla. Pia stanbic bank

taarifa zake zimefichwa ni wazi raisi akitajwa

basi ni mtikisiko wa nchi.

tupaze sauti watanzania huu ndio ukwelI

Kama nchi inatikisika itikisike na ianguke, kuanza upya sio ujinga watanzania wenzangu... PAC walisema kwa kuwa hatuna mamlaka kwake tuanze na PM mimi nasema wote waliojua wakakaa kimya, walioshiriki na wahusika wakuu tuwawajibishe, tunalindana hadi lini, tumeumia sana, kama kesho MUHONGO, MASWI, PINDA NA WEREMA wataachia ngazi tusiridhike, tuendelee kupeana elimu na kuchukua hatua za kuwawajibisha wahusika wakuu,
 
Hela zilizoelekea kwa mzee WA teziiiiii dume AC yke bank imefichwa, CAG hajapewa!!!
Kulikoni?!!!
CCM branch la ibilisi!!!!!
 
Hata kama tutam-criticize Pasco kwavile anaandika vitu tusivyopenda kuvisikia lakini bado ukweli upo pale pale kwamba maamuzi ya PAC yanaonesha wazi kwamba yanalinda baadhi ya watu na kuwashupalia baadhi ya watu... na mmoja wa ambao PAC imemshupalia ni Muhongo! Hata ukimsikiliza Zitto wakati anahitimisha mjadala, alitumia muda mrefu sana kumwa-attack Muhongo kuliko muda alioutumia kum-attack Werema ambae kwa maoni yangu WErema ndio muhusika namba moja katika sakata hili! Unless kama Werema alikuwa anatekeleza maagizo ya wakubwa wake, lakini nafasi ya Werema katika sakata hili ni kubwa kuliko Muhongo ambae PAC ilimkomalia... lakini hata hivyo, siwezi kushangaa kwavile Muhongo ni msema hovyo na ameshawahi kuwachana hadharani baadhi ya wajumbe wa PAC kwahiyo PAC ni kama wanalipiza kisasi na kutaka kumchinjia baharini!!

Tukirudi kwenye suala la PAC kulinda baadhi ya watu! Hivi unaiache BOT katika sakata hili? Wakati Zitto anasoma Ripoti yake alikuwa anaonesha wazi kwamba anamlinda Gavana wa BOT kwa maneno kama vile "Gavana wa BOT alijitahidi sana...." na upuuzi mwingine kama huo! This's stupid, I repeat, it's stupid kwavile hakuna chochote ambacho Zitto alikuwa anakifanya zaidi ya kumlinda Gavana!

Labda niwajuze jambo wasiofahamu taratibu za kibenki! Tunapoingia benki hizi za kawaida, mtu mwenye daraja la chini kabisa benki(apart from supporting staffs) ni Teller... narudia, staff wa daraja la chini kabisa bank ni Teller!!! Lakini ingawj Teller ndie staff wa daraja la chini kabisa; yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho kabisa ya kulipa au kutolipa transaction iliyopo mbele yake! Hata Branch Manager hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa kitu ambacho Teller ana mashaka nacho! Hata CEO hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa malipo ambayo Teller hajajiridhisha kama ni genuine payments! Kama iliyopo mbele ya desk la Teller ni Cheque... basi cheque hiyo hata iwe na mihuli ya RPC, IGP, CAG, TAKUKURU, IKULU na takataka zote unazozijua wewe, bado Teller kama anajiamini, na hajajiridhisha if the payment is genuine, anayo haki with no offense, kukataa kulipa cheki husika na humfanyi chochote kile kwa mujibu wa sheria! Pamoja na mamihuri yote hayo, Teller anayo haki ya kugoma na kumwambia yeyote asiye na mashaka juu ya transaction husika, basi na alipe yeye!!!

Sasa ikiwa ka-Teller tu kana maubavu yote haya, what about BOT? BOT walikuwa na uwezo na haki ya kukataa kufanya malipo ikiwa hawajajiridhisha hata kama ingekuwa ni maagizo kutoka kwa MoF au Ikulu! Na sitaki kuamini kwamba Ndulu haifahamu hii role yake, anaifahamu lakini aliamua kulinda kibarua chake!!!! Sasa ili mradi PAC imetumia kila nafasi kumsafisha Ndulu, ni wazi kwamba iliamua kwa makusudi uwachinjia baharini wale isiowataka na kuwalinda wale inaowataka...
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana, jamaa anashangaza sana kusema kweli, halafu hata kujishtukia hajishtukii kuhusu pumba zake anazoandika mara kwa mara. Mtu wa ajabu sana huyu.

Kwa mwandishi wa habari na mtu ambaye unadai umesoma sheria UDSM, sijawahi kuona mwandishi mbovu kama wewe!

Kanuni nyepesi tu za uandishi zinakushinda. Mjinga nambari moja utakuwa ni wewe.

Unaweka alama za nukuu hata pasipotakiwa. Unarudia rudia maneno yaleyale uliyoyaandika katika lugha moja na kuyaandika katika lugha ingine.

Hivi una matatizo gani wewe?
 
... wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?...
Tundu Lissu alizungumzia hilo hadi akaombewa mwongozo wa eti wa 'kulitumia jina la rais kwa dhihaka!'. Soma kipande hiki kwa ajili ya rejea:
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Akichangia Ripoti ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) alisema ilijulikana miaka 20 iliyopita kwamba IPTL itakuja kuwaumiza Watanzania. "Mwaka 1994 wakati IPTL wanaandika MoU (makubaliano ya awali) na Serikali, Waziri wa Nishati na Madini alikuwa Kanali Jakaya Kikwete, mwaka 1995 wakati mkataba wa kununua umeme unasainiwa kati ya Serikali na wawekezaji hawa, Waziri wa Fedha alikuwa mtu aitwaye, Kanali Jakaya Mrisho Kikwete. "Miaka 20 baadaye Sh321 bilioni za Watanzania zimeibiwa, Rais wa Tanzania ni Jakaya Mrisho Kikwete, tunataka fedha zetu zirudi," alisema Lissu. Mara baada ya kauli hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu alisimama na kuomba mwongozo kuhusu matumizi ya jina la rais bungeni.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kwa hiyo, si watanzania wote ni ignorant, ila labda useme miongoni mwa wale wafanya maamuzi. Mfano ni wewe uliyeliona hilo, una mahali pa kulizungumzia zaidi ya JF ambako hakuna wafanya maamuzi? Jibu ni hapana, ila CCM ni janga!
 
Hata kama tutam-criticize Pasco kwavile anaandika vitu tusivyopenda kuvisikia lakini bado ukweli upo pale pale kwamba maamuzi ya PAC yanaonesha wazi kwamba yanalinda baadhi ya watu na kuwashupalia baadhi ya watu... na mmoja wa ambao PAC imemshupalia ni Muhongo! Hata ukimsikiliza Zitto wakati anahitimisha mjadala, alitumia muda mrefu sana kumwa-attack Muhongo kuliko muda alioutumia kum-attack Werema ambae kwa maoni yangu WErema ndio muhusika namba moja katika sakata hili! Unless kama Werema alikuwa anatekeleza maagizo ya wakubwa wake, lakini nafasi ya Werema katika sakata hili ni kubwa kuliko Muhongo ambae PAC ilimkomalia... lakini hata hivyo, siwezi kushangaa kwavile Muhongo ni msema hovyo na ameshawahi kuwachana hadharani baadhi ya wajumbe wa PAC kwahiyo PAC ni kama wanalipiza kisasi na kutaka kumchinjia baharini!!

Tukirudi kwenye suala la PAC kulinda baadhi ya watu! Hivi unaiache BOT katika sakata hili? Wakati Zitto anasoma Ripoti yake alikuwa anaonesha wazi kwamba anamlinda Gavana wa BOT kwa maneno kama vile "Gavana wa BOT alijitahidi sana...." na upuuzi mwingine kama huo! This's stupid, I repeat, it's stupid kwavile hakuna chochote ambacho Zitto alikuwa anakifanya zaidi ya kumlinda Gavana!

Labda niwajuze jambo wasiofahamu taratibu za kibenki! Tunapoingia benki hizi za kawaida, mtu mwenye daraja la chini kabisa benki(apart from supporting staffs) ni Teller... narudia, staff wa daraja la chini kabisa bank ni Teller!!! Lakini ingawj Teller ndie staff wa daraja la chini kabisa; yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho kabisa ya kulipa au kutolipa transaction iliyopo mbele yake! Hata Branch Manager hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa kitu ambacho Teller ana mashaka nacho! Hata CEO hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa malipo ambayo Teller hajajiridhisha kama ni genuine payments! Kama iliyopo mbele ya desk la Teller ni Cheque... basi cheque hiyo hata iwe na mihuli ya RPC, IGP, CAG, TAKUKURU, IKULU na takataka zote unazozijua wewe, bado Teller kama anajiamini, na hajajiridhisha if the payment is genuine, anayo haki with no offense, kukataa kulipa cheki husika na humfanyi chochote kile kwa mujibu wa sheria! Pamoja na mamihuri yote hayo, Teller anayo haki ya kugoma na kumwambia yeyote asiye na mashaka juu ya transaction husika, basi na alipe yeye!!!

Sasa ikiwa ka-Teller tu kana maubavu yote haya, what about BOT? BOT walikuwa na uwezo na haki ya kukataa kufanya malipo ikiwa hawajajiridhisha hata kama ingekuwa ni maagizo kutoka kwa MoF au Ikulu! Na sitaki kuamini kwamba Ndulu haifahamu hii role yake, anaifahamu lakini aliamua kulinda kibarua chake!!!! Sasa ili mradi PAC imetumia kila nafasi kumsafisha Ndulu, ni wazi kwamba iliamua kwa makusudi uwachinjia baharini wale isiowataka na kuwalinda wale inaowataka...

Wanabodi,

Mtanisamehe sana kwa kuanza huu mjadala kwa maneno makali, kuwa sisi Watanzania tulio wengi ni "ignorants!", vichwa maji kabisa!, vichwani ni weupe!, uwezo wa kufikiri, "logical thinking", ni sifuri, ndio maana hatuna uwezo wa kufanya maamuzi ya maana, "informed decisions", hali inayopelekea, tunapelekwa pelekwa tuu kama mazuzu!, kiasi kwamba, wengi wetu tunashabikia zaidi na kushupalia vitu vidogo vidogo ambavyo ni non issues, na immaterial, ambazo sio chanzo bali ni matokeo tuu, badala ya kudeal na issue zenyewe ambazo ndicho chanzo, kilizopelekea haya yatokanayo, havishungulikiwi, havizungumzwi!, haviguswi!.

Hii ignorance ya Watanzania ina cut across society yetu na ku reflect ndani ya kila sekta ya jamii yetu kuanzia ndani ya familia zetu, mitaa yetu, vitongoji vyetu, vyama vyetu, hadi ndani ya bunge letu, tuna wabunge ma ignorants mule!, tuna viongozi wetu ma ignorants hadi ndani ya cabinet yetu!, tuna viongozi wa taasisi za umma ma ignorants hadi t, tuna viongozi wetu wa vyombo vya dola ni ma ignotants, na wana jf wengi pia ni ignorants tuu, nikiwemo mimi mwana JF, Pasco wa jf, tofauti na wengi maignorants wenzetu, wanajikalia kimya, hivyo kuificha hiyo ignorance yao, lakini sisi wengine ambao kwa bahati mbaya sana, hatukujaliwa aibu, tunaionyesha hiyo ignorance yetu kwa ku speak out and expressing our minds, tatizo, ni, in so doing, tunajikuta tumewaambukiza ignorance, hata wengine ambao hawakuwa ignorants!. Sorry for this.

Ni kufuatia ignorance hii, Chama cha Mapinduzi, (CCM), kinaitumia ignorance hii ipasavyo kwa kuifanya ndio mtaji wake wa kupatia kura za ushindi, mwaka hadi mwaka, na mwakani tutaichagua tena CCM kwa kuipa ushindi wa kishindo!.

Hisia za kujiuliza, kama sisi ni ma ignorants au tumelogwa, ni kufuatia kuwa na mtazamo, ya kuwa haiwezekani, watu wenye akili zao timamu, wakafanyiwa mambo ya ajabu ajabu kama haya, lakini bado tunaichagua CCM tena na tena!.

Wakati tulipopata uhuru toka kwa mkoloni, tulikuwa na maadui wakuu watatu, ujinga, umasikini na maradhi, lakini hadi leo miaka zaidi ya 50 baada ya uhuru, sio tuu, wale maadui wakuu watatu bado wapo, bali ujinga umeongezeka mara dufu, umasikini sasa ni uliotopea, na maradhi hadi mengine ni janga, vimeongezeka afadhali ya zamani na enzi za mkoloni, bali pia, tumeongeza idadi ya maadui wakuu, wakiwemo rushwa na ufisadi, ambapo mazao yake ni pamoja na DCP, Deep Green, Meremeta, TanGold, Alex Stewart, EPA, Richimond, na sasa Escrow.

Kitu kizuri cha ajabu kuhusu sisi Watanzania ni kujifanya kupiga kelele sana as if tunauchukia umasikini, ujinga, maradhi, rushwa na ufisadi, lakini sisi wale wale, mwaka hadi mwaka, tunawachagua watu wale wale, chama kile kile, sera zile zile, tukitegemea matokeo tofauti!, hii ni nini kama sio ignorance at the highest levels?!. Keshokutwa tunawapa serikali za mitaa!, mwezi April tuna wapitishia ile "Bora Katiba" kwa kura za ndio za kutosha, na zisipotosha "zitatosheshwa!",na October, 2015, tunamalizia kazi, kwa kuirudisha CCM kwa ushindi wa kishindo!.

Ignorance hii imejidhihiri wazi kwenye huu mjadala wa Escrow unao endelea sasa, ambapo wengi wetu, tumejikita kwenye issue ya fedha za Escrow tuu, ambayo sio a very big deal!, fedha ya escrow ni matokeo tuu ya hili jinamizi linaloitwa IPTL!, na hiyo pesa iliyokuwa inawekwa kwenye account ya escrow ni capacity charges only, bado Tanesco inalipa mabilioni kwa mabilioni ya kulipia Utilities huko huko IPTL, Aggreko, Simbion, Songas!, badala ya watu kujadili chanzo, na kwa nini tumefika hapa, wao wanajadili matokeo tuu!. Hii kama sio ignorance ni nini?!.

Katika kuwabaini wahusika, watu wanafanya "cherry picking ya kumchagua huyu na yule, na kumuepusha yule na yule ili mradi tuu apatikane "mbuzi wa kafara!", na miongoni mwa wahusika, sijaisikia BOT ikitajwa tajwa, simply kwa sababu yeye ni dalali tuu!. Kama escrow ni account ya ubia kati ya serikali na IPTL, BOT ililipaje zile pesa PAP?!.

Escrow sio issue sana kivile!, escrow ni matokeo tuu, issue yenyewe haswa ni IPTL, ilikujaje, ilipitaje, ilikubalikaje kutuwekea mitambo ya mtumba, obsolete technology, ilikubalikaje kukubali kutozwa capacity charges zile?!, hii kama sio ignorance ni nini?!.

Watu wanataja taja tuu majina!, wananyooshea watu vidole!, wanawapigia kelele waliolipwa na JR tuu, waliolipwa na PAP wao wako wapi?, Walioileta IPTL wako wapi?, hii ni nini kama sio ignorance?!, au tumelogwa?!. Tunapaswa kuwatafuta responsible people tangu hili jinamizi la IPTL limekuja nchini, tuwawajibishe!, na sio kutafuta mbuzi wa kafara, au kama kawaida yetu, tufunike kombe mwanaharamu apite!".

Pasco

Imekaa vizuri! Ati -Spika analalamikia wabunge wasichukue uamuzi kwani yeye ameshaumizwa kwa kukwaruzana na mhimili wz mahakama na asingependa tena mkwaruzo na serikali! Amejiona yeye kama Makinda na sio Taasisi. Anaogopa na anaogopa maslahi binafsi sio ya taifa .

Ila katika orodha ya igmorants ningewaondoa Tundu na Mbowe. Bahati mbaya Zito ni mwenzetu ktk ignorance
 
Last edited by a moderator:
Heshima mbele mkuu, mabandiko yako mengine kuhusu saga la escrow yanachanganya lakini ninaelewa wapi unataka tujiegemeze, Lisu alieleza vizuri, 1994 alienegotiate na kuitambua IPTL ni mkuu wa kaya akiwa maji, nishati na mdini, 1995 akiwa fedha, 2014 akiamuru fedha zitoke kwa ushauri wa AG, bunge hili suala wamegoma kabisa lisijadiliwe maana yake nini? Wananchi hatutaki kabisa kujiongeza? Hatuwezi kuungana na wale wachache wanaotutetea? Hebu tuamke uchunguzi mara ngapi? Tutaifishe IPTL na H.S. Seth akamatwe kama PAC ilivyoazimia kabla ya saga kuanza kujadiliwa. KWELI ITUWEKE HURU.

Umenena mkuu. watanzania tusifanywe wajinga kiasi hiki, tusiwe waoga kupitiliza tuamke tuwaunge mkono watetezi wetu waliowachache ukawa. Kuna TETEZI ARUSHA KUMENUKA WANANCHI HAWAKULALA WANAPANGA MIKAKATI YA KUINGIA BARABARANI KUDAI HAKI ZETU. NAWASIHI WANANCHI WOTE TULIOKO KUSINI NA MAENEO YOTE TZ TUAMKENI JAMANI TUWAPE SUPPORT WATETESI WETU.
 
Wanabodi,

Nianze na hili Angelico: Mie sio mshabiki wa Pasco na wala sikubaliani naye katika mijadala mingi.

Tujikite hasa katika ujumbe aliouandika bila kujali amesoma kiasi gani, namna ya uandishi wake na mengine yahusiano na mapungufuku yake Kitaaluma. Sote tukiri kwamba elimu yetu chini ya CCM imekuwa ikishuka ubora Kadri miaka inavyokwenda mpaka sasa watoto wetu wana pata "bora elimu".

Hakuna mahali aliposema tuachane na issue ya Escrow mbele yetu.

Nilivyomwelewa ujumbe wake ni kwamba tukishafanya hii short term decision ya kuadhibu wezi wa escrow, tusiishie hapo tukidhani tatizo limetatuliwa. Tuende mbali zaidi na kuchunguza kwa undani chanzo cha IPTL. Hivi sasa tunavyojadili kuna watoto wa IPTL ambao wamekomaa mfano Aggreko, songas, Richmond (aliyevunja ungo kuwa Dowans aliyejifungua Symbion).
Wote hao wanalipwa na Tanesco millions of dollars kila kukicha.hii ya Escrow inawatisha Watanzania kwa kuwa ni large amount accumulated over 10 years. Anachosema Pasco ujinga wetu hakuna hata mmoja bungeni, wanasiasa na media anayehoji kwa undani zaidi hili suala la Energy security na future yake.
Kutokana na uzoefu wake hapo Tanzania ukijumuisha na ufahamu wake wa hili tatizo anachosema Pasco (atanisahihisha) njia pekee ya kuanza kutatua ni kwa kuitoa CCM madarakani, period. Namna ya kuweza kuitoa madarakani bila kuacha nchi isiparanganyike kwa scars za kudumu ni kupitia Sanduku la Kura siku ya uchaguzi.
Tunafahamu wajinga wapo kila nchi sema kwa Tanzania (tofauti na nchi zilizoendelea) ujinga umeota mizizi katika kundi la "waliosoma".Hawa wasomi wanaonyesha ujinga wao pale wanaposhindwa kujipanga na kuitoa ccm madarakani kipindi uchaguzi unapofika. Mifano hai aliyoiongelea ni hizi chaguzi zinazokuja hapa mbeleni. Kura zinapigwa na zinaibiwa au kutosheshwa na wasomi Hawa wanabaki kulalama kama hivi sasa.

Sasa Pasco anapojaribu kusema tatizo ni sisi, tunamchukia na kusema mchumia tumbo. Nani huyo aishie nje ya Tz asiyemchumia tumbo? (Asiejali zaidi familia yake binafsi kupata huduma nzuri za afya na elimu bora).
Tanzania itabadilika pale tu wasomi wanaojali na kuheshimu utu watakaposhirikiana na likeminded citizens kuiondoa ccm madarakani.

Tujifunze kwa Waingereza, PM Winston Churchill pamoja na kuipigania UK kuishinda Germany kuonyesha strong leadership lakini ilipofikia uchaguzi wananchi walimpiga chini. Walitambua different challenge ya ku rebuild UK requires different way of thinking and mentality. Churchill standing haijawa undermined whatsover. Nas hatuna budi kuwaambia ccm sawa ukombozi umepita sasa ni challenges nyingine.

Nawasilisha.
 
Siongezi neno kaka.halipo la kupunguza. Mifano imeshiba. Ahsante

Hata kama tutam-criticize Pasco kwavile anaandika vitu tusivyopenda kuvisikia lakini bado ukweli upo pale pale kwamba maamuzi ya PAC yanaonesha wazi kwamba yanalinda baadhi ya watu na kuwashupalia baadhi ya watu... na mmoja wa ambao PAC imemshupalia ni Muhongo! Hata ukimsikiliza Zitto wakati anahitimisha mjadala, alitumia muda mrefu sana kumwa-attack Muhongo kuliko muda alioutumia kum-attack Werema ambae kwa maoni yangu WErema ndio muhusika namba moja katika sakata hili! Unless kama Werema alikuwa anatekeleza maagizo ya wakubwa wake, lakini nafasi ya Werema katika sakata hili ni kubwa kuliko Muhongo ambae PAC ilimkomalia... lakini hata hivyo, siwezi kushangaa kwavile Muhongo ni msema hovyo na ameshawahi kuwachana hadharani baadhi ya wajumbe wa PAC kwahiyo PAC ni kama wanalipiza kisasi na kutaka kumchinjia baharini!!

Tukirudi kwenye suala la PAC kulinda baadhi ya watu! Hivi unaiache BOT katika sakata hili? Wakati Zitto anasoma Ripoti yake alikuwa anaonesha wazi kwamba anamlinda Gavana wa BOT kwa maneno kama vile "Gavana wa BOT alijitahidi sana...." na upuuzi mwingine kama huo! This's stupid, I repeat, it's stupid kwavile hakuna chochote ambacho Zitto alikuwa anakifanya zaidi ya kumlinda Gavana!

Labda niwajuze jambo wasiofahamu taratibu za kibenki! Tunapoingia benki hizi za kawaida, mtu mwenye daraja la chini kabisa benki(apart from supporting staffs) ni Teller... narudia, staff wa daraja la chini kabisa bank ni Teller!!! Lakini ingawj Teller ndie staff wa daraja la chini kabisa; yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho kabisa ya kulipa au kutolipa transaction iliyopo mbele yake! Hata Branch Manager hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa kitu ambacho Teller ana mashaka nacho! Hata CEO hana ubavu wa kumlazimisha Teller kulipa malipo ambayo Teller hajajiridhisha kama ni genuine payments! Kama iliyopo mbele ya desk la Teller ni Cheque... basi cheque hiyo hata iwe na mihuli ya RPC, IGP, CAG, TAKUKURU, IKULU na takataka zote unazozijua wewe, bado Teller kama anajiamini, na hajajiridhisha if the payment is genuine, anayo haki with no offense, kukataa kulipa cheki husika na humfanyi chochote kile kwa mujibu wa sheria! Pamoja na mamihuri yote hayo, Teller anayo haki ya kugoma na kumwambia yeyote asiye na mashaka juu ya transaction husika, basi na alipe yeye!!!

Sasa ikiwa ka-Teller tu kana maubavu yote haya, what about BOT? BOT walikuwa na uwezo na haki ya kukataa kufanya malipo ikiwa hawajajiridhisha hata kama ingekuwa ni maagizo kutoka kwa MoF au Ikulu! Na sitaki kuamini kwamba Ndulu haifahamu hii role yake, anaifahamu lakini aliamua kulinda kibarua chake!!!! Sasa ili mradi PAC imetumia kila nafasi kumsafisha Ndulu, ni wazi kwamba iliamua kwa makusudi uwachinjia baharini wale isiowataka na kuwalinda wale inaowataka...
 
Last edited by a moderator:
Kuna very strong message kwenye hii thread, ila I'm a bit concerned kama wadau wengine waliotangulia- Pasco umekuaje mkuu!! Uandishi wako unabadirika siku hadi siku, msg nzuri ila huandiki kama mwanahabari au pasco yule wa siku za nyuma. Nimekuelewa lakini.
 
Last edited by a moderator:
Lakini si wewe unashindia kwenye mitandao kila siku kuwabeza wapinzani? Unapokosa posho za magamba unaungana na wapinzani. Wanapokupa mnofu unawabeza wapinzani. Hutabiriki. Wewe ni ndumila kuwili! Nadhani wewe ndiye mjinga namba moja!

Niliposoma bila kuangalia author nilijaribu kuielewa mistari. Mwisho nilipojua ni Pasco nikabaki njia panda. Mkuu Pasco unajua hueleweki kabisa! Thread zako zinasigishana
 
Last edited by a moderator:
Pasco,

Umeandika sana hapo juu! Nimejaribu kusoma neno kwa neno!!

Mwishowe nimekuja na summary au conclusion moja tu, kua SISI WATANZANIA NI WAJINGA SABABU YA KUENDELEA KUICHAGUA CCM PAMOJA NA MAPUNGUFU YAKE CHUNGU NZIMA!!
 
Last edited by a moderator:
Niliposoma bila kuangalia author nilijaribu kuielewa mistari. Mwisho nilipojua ni Pasco nikabaki njia panda. Mkuu Pasco unajua hueleweki kabisa! Thread zako zinasigishana
Mkuu Maendeleo Tu, pole, sisi binadamu tunatofautiana uwezo wa kujieleza, uwasilishaji mada na kueleweka, ndio maana wengine huwa ni waliimu wa kufundisha wengine waelewe, sisi wengine ni wasema onyo, kazi yetu ni kusema chochote tunachokiona, na kuiacha kazi ya uelewa kwa wale tuu watakaoelewa, au kama hivi wachache wanaoelewa, kuwaelewesha na wengine kama hivi, anavyofanya huyu Mkuu Shark
Pasco,

Umeandika sana hapo juu! Nimejaribu kusoma neno kwa neno!!

Mwishowe nimekuja na summary au conclusion moja tu, kua SISI WATANZANIA NI WAJINGA SABABU YA KUENDELEA KUICHAGUA CCM PAMOJA NA MAPUNGUFU YAKE CHUNGU NZIMA!!

Mkuu Shark, asante kuelewesha.

Pasco
 
Pasco... hebu tuache tafadhali.
Sisi ni wale tuaochangia misiba kuliko matibabu.
Sisi ni wale tunaochangia harusi kuliko elimu.
Sisi ni wale tunaoazimia kuandamana bila kikomo huku mkononi tukiwa na tiketi za ndege kwenda ughaibuni.
Sisi ni wale tunaolalamikia wizi huku tukipiga deals maofisini mwetu.
Sisi ni wale tunaolalamika bila kutimiza wajibu wetu.
Sisi ni wale "TUNAOPIGANIA MIZENGO PINDA AJIUZULU huku tukiisahau IPTL kama ndio zimwi linalotuua.
Sisi ni wale tunaofurahia KAGASHEKI KUJIUZULU huku tukisahau Tembo na vifaru wanavyoteketea.
Sisi ndio wale TUNAOLALAMIKIA KUIBIWA KURA huku tukikwepa kupiga kura.
Sisi ni waleeee tunaoMkashifu ZZK leo na kumuita MSALITI na mchumia tumbo kisha kesho tukamuita shujaa na mzalendo.
Hebu tuache bana. Sisi ndio sisi
 
Back
Top Bottom