Escrow inakuzwaje na media?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,467
33,407

attachment.php


MOTO uliowashwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila juu ya ukwapuaji wa fedha za umma katika akaunti ya Tegeta Escrow bado unafukuta kwani wakati wowote kuanzia sasa, Rais Jakaya Kikwete atafunguka juu ya maazimio nane yaliyowasilishwa kwake na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watanzania wote walishuhudia kupitia televisheni jinsi wabunge walivyokuwa wakiijadili ripoti ya Kamati ya Hesabu za serikali (PAC) iliyochambua taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu wa serikali (CAG) pamoja na TAKUKURU.

Waliona jinsi hoja za wabunge, kutoka kwa vyama vyote walivyokuwa wakikemea wizi ule mkubwa, ambao mwisho wa siku, bunge likakubaliana kwa pamoja kuwa serikali ina wajibu wa kufanya jambo katika suala hilo.

Lakini katika hali ya kusikitisha, baadhi ya wanasiasa, hasa wa Chama Cha Mapinduzi, wanadiriki kuendelea kulitetea jambo hili kupitia majukwaa ya kisiasa, wakidai kuwa suala hilo wala hata siyo muhimu kwa wananchi, bali linakuzwa na vyombo vya habari kwa kuliandika mara kwa mara.

Kauli hii ya kuudhi ilitolewa wiki iliyopita na Katibu wa Itikadi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, ambaye alidai kuwa madai ya wapinzani kuwa chama chao kitashindwa katika uchaguzi mkuu ujao kwa sababu ya kashfa ya Escrow ni kujidanganya, na kwamba wao wataibuka na ushindi mkubwa kwa vile wananchi bado wanakiamini na kuwa suala la wizi wa mabilioni hayo ni la media kwa sababu watu hawalifuatilii.

Tumekuwa kila siku tukipiga kelele juu ya nyendo za watendaji wetu katika ofisi za umma, ambazo zinawaumiza wananchi, lakini bahati mbaya wenye wajibu wa kuwakumbusha na kuwasukuma, wanawachekea.

Huenda kwa kuwa Nape amekulia katika mfumo anaoutetea ndiyo maana haoni ubaya wa watendaji wa serikali kubariki vitendo vya wizi na matumizi mengine ya ovyo ya ofisi za umma. Ni jambo la ajabu kwamba katika ziara anazoandamana na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana huko vijijini, hatishwi na umasikini wa wananchi wengi.

Nilidhani, yeye kama kiongozi, tena kijana anayehitaji mabadiliko ndani ya chama chake kilichoharibiwa na mfumo mbovu wa kulinda na kutetea mafisadi, asingezungumza maneno kama hayo, yanayoonyesha kuwa wananchi wameshasahau.

Vilevile ni dharau kwa wananchi hao kuwa eti hata kama watuhumiwa wa wizi huu hawataadhibiwa, kitu ambacho kwa asilimia kubwa kinaweza kuwa kweli, eti bado CCM itapeta kwenye uchaguzi kwa vile inapendwa.

Kwanza ni kujidanganya kuamini kuwa watu wamesahau na kama anafikiri habari hizi zinakuzwa na media, basi ni lazima atambue kuwa media zinafanya kazi kulingana na mahitaji ya walaji wake, ambao ni wananchi. Akiona tunaandika sana, ni kwa sababu tunaowaandikia, wanataka kujua nini hatima ya wezi wale wa fedha za umma.

Katika hili, viongozi wa CCM wangeungana na wananchi kutaka watendaji wanaotajwa katika kashfa hiyo waadhibiwe na mamlaka zinazohusika. Hii ingethibitisha kuwa chama kimeunda serikali inayopaswa kuwajibika.

Huenda ni kweli bado chama tawala kinapendwa na kwamba hadi wakati huo watu watakuwa wameshasahau, lakini kitu cha msingi ambacho ningependa Nape na chama chake waelewe ni kuwa kauli na matendo yao, yanazidi kuwaamsha watu na kupata uelewa mpya.

Wanatambua kwamba kumbe wanaonekana wajinga, yaani wakubwa wanaiba, wanagawana fedha, halafu hawafanywi lolote na siku zinakwenda. CCM inapaswa ifanye tathmini ya makusudi, ya ukweli, ili itambue ni kwa kiasi gani wananchi bado wana imani nacho. Matumizi makubwa ya fedha yanayofanywa na chama pamoja na makada wao kwenye chaguzi mbalimbali, ni uthibitisho tosha kuwa kura za imani zinazidi kupungua, zinabakia kura za pesa! chanzo.GBP


UNGANA NASI KATIKA FACEBOOK, TWITTER , INSTAGRAM , YOUTUBE

 

Attachments

  • Nape.jpg
    Nape.jpg
    31.8 KB · Views: 405
Kuna siri nchi hii, watu wamesha jua hata kabla hajatoa matangazo ya hatua alizochukua
 
Back
Top Bottom