Erring on the Side of Caution: Kikwete usiwaapishe mawaziri wasioapishwa kuwa wabunge kwanza!

Kwenye hii katiba yetu inasema watakachoamua baraza la mawaziri hakitapingwa Mahakamani. Kwa kuwa baraza la mawaziri linaongozwa na Rais, basi by implication hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji teuzi za Rais. Hio ndio katiba yetu kama tutapata nafasi ya kuirekebisha basi tuiandike ili makosa haya au mianya hii isitokee tena.
 
Nachotaka kujua mimi kuna kiapogani kilichokusudiwa ktk ibara hii?..kama hakuna kwa nini kifungu hiki kipo kwenye katiba. Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.


Katiba ni a top law/document. Ina set a broad net. Kwa hiyo kufikiri kwamba katiba inaandikwa mahsusi kwa kiapo fulani ni makosa.

Kifungu kipo kwenye katiba kwa sababu katiba inataka viapo vyote vinavyohusiana na utendaji wa kazi yake viapwe kabla ya mtu kuanza kazi.

Kiapo cha uaminifu bungeni hakihusiani na kazi za waziri, kwa hiyo hakihusiani na uwaziri.
 
Kweli kabisa! Aisee mtafute Warioba na timu yake utoe hayo maoni maana ifike mahali tuwe kama Marekani na Ghana mawaziri wasitokane na wabunge. Wanasiasa wanatuvuruga sana kupewa kazi za wataalamu na watendaji serikalini. Ndio maana tupo hapa tulipo.

Watanzania tumezoea kuburuzwa buruzwa tu. Mpaka sasa hata hatujui rais analipwa mshahara kiasi gani wakati sisi wananchi ndiyo waajiri wake. Sasa wewe umeona wapi mwajiri ambaye hajui mshahara wa mwajiriwa wake? Kuna watu huwa wanasema eti mshahara wa mtu ni siri yake kati yake na mwajiri wake. Huwa naishia kutikisa kichwa tu.

Binafsi nina wasiwasi sana na hiyo katiba mpya. Lakini tusubiri tuone...
 
Kwenye hii katiba yetu inasema watakachoamua baraza la mawaziri hakitapingwa Mahakamani. Kwa kuwa baraza la mawaziri linaongozwa na Rais, basi by implication hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji teuzi za Rais. Hio ndio katiba yetu kama tutapata nafasi ya kuirekebisha basi tuiandike ili makosa haya au mianya hii isitokee tena.

Mkuu tujuze, ibara gani hii tuipitie?
 
Unakifahamu kiapo cha Ubunge kinavyosema? na kwanini ni kiapo muhimu kwa mbunge yeyote yule. Mbunge wa viti maalum kwanini anaapishwa kuwa mbunge wakati uteuzi wake unafanywa automatically? Kiapo cha Ubunge ni pre-condition ya vitu vyote ambavyo mbunge anaweza kuvifanya baadaye - kwa maoni yangu. Uwaziri basi una presume ubunge. Labda nikuulize swali jingine je mbunge anaweza kukataa kula kiapo cha ubunge na bado akabakia kuwa mbunge kwa vile kateuliwa au kachaguliwa?
Mkuu, mbunge anaapishwa kabla ya kufanya "National Assembly" Bussiness.

Parliamentary bussiness is different from National Assembly. The later is just a part of the whole parliamentary bussiness, like Local govt issues for example.
 
Kuna sehemu nimeulizia kuhusu compensation za mawaziri - hivi huwa wanapokea mishahara na marupurupu kotekote?
 
Kiranga

Kazi ya mbunge ni nini kabla ya kuapa ukiacha kuchagua spika,
I mean kama Mbatia tayari ni mbunge kabla ya kuapa atakuwa anafanya nini kwa mwezi mzima.

Kazi ya mbunge ni ubunge.

Mbatia hawezi kufanya shughuli zozote za kibunge mpaka aapishwe. Kitu pekee anachoweza kufanya kama mbunge ni kama kutakuwa na uchaguzi wa Spika anaweza kumchagua.

Tofautisha kuwa mbunge na kufanya shughuli za kibunge. Kuna watu wanasheria by profession, lakini hawafanyi kazi za uanasheria. Kutofanya kazi za uanasheria hakuwaondolei uanasheria wao.

Fact kwamba Mbatia hawezi kufanya shughuli za kibunge - zaidi ya kumchagua Spika- mpaka aapishwe kwanza, hazimuondolei ubunge wake kwa sasa hivi.

Point yako nini?
 
Mkuu, mbunge anaapishwa kabla ya kufanya "National Assembly" Bussiness.

Parliamentary bussiness is different from National Assembly. The later is just a part of the whole parliamentary bussiness, like Local govt issues for example.

What's the difference between the two?
 
Katiba ni a top law/document. Ina set a broad net. Kwa hiyo kufikiri kwamba katiba inaandikwa mahsusi kwa kiapo fulani ni makosa.

Kifungu kipo kwenye katiba kwa sababu katiba inataka viapo vyote vinavyohusiana na utendaji wa kazi yake viapwe kabla ya mtu kuanza kazi.

Kiapo cha uaminifu bungeni hakihusiani na kazi za waziri, kwa hiyo hakihusiani na uwaziri.

Kwenye red. Absolutely right kwamba hivi viapo viko independent. Tatizo linakuja ni mtu wa aina gani anatakiwa kula kiapo? Waziri anatokana na ubunge, na ili uwe mbunge unatakiwa ufanye nini? Kinachogomba hapa ni utarabu kwamba unaanza na number 1,2,3 ... au unaanza na no 3.2.1?
 
Unless kama kuna mfano huko nyuma ambapo Rais aliteua na kuapisha mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge tunaweza kusema anafuata precedence au kama aliwahi kuteua wabunge wakati ambapo kikao cha Bunge kilikuwa mbali kama kilivyo sasa na kuwafanya wachelewe kuapishwa Ubunge...

ndugu yangu ndugu yangu! rais hatakiwi kutekeleza majukumu yake kwa kufuata precedence au utaratibu uliozoeleka bali kwa MUJIBU WA KATIBA, unaweza ukaanzisha thread yenye maneno meeeengi sana lakini ikawa hakuna mantiki! cha muhimu ni kutueleza ni sehemu gani ya katiba imekiukwa, yaani ibara au kipengere gani cha katiba ndo ukiukwaji umefanyika! tuache maneno mengi tuangalie katiba inasemaje, AG amenukuu vipengere kujenga hoja yake, basi na wale wanaopinga waje na vipengere kuunga mkono hoja zao!
 
Kazi ya mbunge ni ubunge.

Mbatia hawezi kufanya shughuli zozote za kibunge mpaka aapishwe. Kitu pekee anachoweza kufanya kama mbunge ni kama kutakuwa na uchaguzi wa Spika anaweza kumchagua.

Tofautisha kuwa mbunge na kufanya shughuli za kibunge. Kuna watu wanasheria by profession, lakini hawafanyi kazi za uanasheria. Kutofanya kazi za uanasheria hakuwaondolei uanasheria wao.

Fact kwamba Mbatia hawezi kufanya shughuli za kibunge - zaidi ya kumchagua Spika- mpaka aapishwe kwanza, hazimuondolei ubunge wake kwa sasa hivi.

Point yako nini?
Hapa mkuu wangu umechapia.. Profession ya mtu ni elimu tofauti kabisa na Ubunge ambao unaweza kuvuliwa na ukawa batili hata kabla ya kuanza ubunge. Hutahesabika kama ulikuwa mbunge lakini huwezi kuondoa elimu ya mwanasheria kichwani. Hivyo kuchaguliwa au kuteuliwa sii hoja kabisa kesho Mbatia anaweza kuvuliwa Ubunge na JK hata kabla hajaingia bungeni na ikasomeka sii mbunge tena.

Kifupi unapoapishwa na Bunge unakuwa sehemu ya muhimili huo na ndio unaotoka mawaziri japokuwa ni makosa lakini you have to be part of the team na kwa sheria zake, kama tunavyowakilisha majina ya team ya Taifa Stars FIFA lazima wachezaji wetu wawe raia wa nchi husika kufuatana na kanuni za usajili wa uraia wa nchi hiyo. Hivyo kwetu sisi Bongo hatuna uraia wa nchi mbili (itatazamwa hivyo) lakini nchi nyinginezo wanaruhusu - Vipengele vyote hivi hutamwa kutokana na picha ya kwanza ya uraia wa mhusika..
 
Kwa Rais wenu mwenye kichwa cha Koroma yote yanawezekana. Hivi kwa nini huwa hapendi kujielimisha huyu panzi? Ingemgharimu nini kama angesoma katiba kwenye ibara zinazohusu Bunge na baraza la mawaziri kama hakuwa na uhakika? Huyu jamaa sijui ni kazi gani ilikuwa inamfaa! Urais hapana bwana uwezo wake mdogo sana! Waliosoma naye hebu watusaidie darasani alikuwaje huyu?!

HII HAIKUWA cabinet reshufle bali graduation ceremon ya corruption institute. Kumbuka graduation ya kwanza ilifanyika kwa wezi wa EPA, Richmond na Radda ambapo waliopigwa disco noi Basil mramba na Daniel Yona tuu.

Hii graduation ya corruption institute ya juzi ilikuwa na ma genious sana, hakuna hata mmoja aliyepelekwa mahakani ingawa loss walioipataia serikali ni sawa na bajeti ya mwaka mzima ya wizara ya maji ya ya kisiwa cha commoro.

Mpango ulikuwa ni kumchuuza James Mbatia, naye aliingia mtegoni akizania ataupta uwaziri wa fedha au madini lakini mwisho wa siku, kajikuta kapishana na mpira langoni. yupo wapi lamwai?.

wewe ngoja hawa walioteuliwa au kusajiliwa upya katika baraza la mawaziri watakavyokuwa mbogo kwa kuhujumu. tena muda huu watahakikisha CAG anapewa chake ili awalinde. ni bora mkoloni arude tuu labda tutapiga mbele hatua lakini hawa wazalendo wenzetu ni sawa na hakuna kabisaaaaa.

CCTV africa wametangazo hii corruption. Mabalozi wote wa nchi za nje wmeshuhudia kwa jinsi gani hawa mawaziri wametoka bila kukamtwa! sasa mpaka china wametuzalau kabisa na kujenga urafiki wa karibu na Kenya. kweli kabisaa hatuna nchi!
 
Watanzania hatuna kabisa concept ya streamlining. Tunapenda kung'ang'ania mambo magumu magumu na yanayochanganya bila hata sababu za msingi.
Kweli mkuu tume-complicate vifungu vya katiba hadi vinatuchanganya wenyewe.
Lakini hizi complications wanaziruhusu wao ili kina Werema wapatie loopholes kama hizi, ila siku hizi angalau watu wanahoji hata kama wanafunika lakini wanajua watu wameona siyo kama zamani hili lingepita hivihivi tu bila kuhojiwa.
 
By Nyani Ngabu Watanzania hatuna kabisa concept ya streamlining. Tunapenda kung'ang'ania mambo magumu magumu na yanayochanganya bila hata sababu za msingi.
Tafadhali sana, tungependa kufahamu ni namna gani au kivipi, tena in "detail" au kwa "kinaga ubaga", jinsi ambavyo hiyo dhana yako ya "streamlining" inegeweza kusaidia matatizo unayodhani kuwapo kutokana na mfumo au hali iliyopo hivi sasa?
 
Ndio sababu nilikuwambia hapo awali uvute pumzi na usome kwa makini. Yaani mtu anaweza kukumbua mvua inanyesha na mko wote pamoja lakini bado ukamuuliza - kweli mvua inanyesha?!

Nimeomba vifungu vya katiba, mie nime cite ibara ya 68.

Kwa nini kubishana kama mvua inanyesha nje wakati tunaweza kutoka na kuangalia?

Kwa nini kubishania maneno wakati katiba ipo online?
 
Kaka, taratibu! Tushazoea ego -trippin' zako kwa muda mrefu. Lakini, kwa taarifa yako, kuna Watanzania zaidi ya milioni 43, na pengine ni 0.01% tu kati yao wana access na mtandao wa JF. Usijifanye wewe ni mjuaji and so intellectually gifted as much as you would like to pretend to be so!

Mie nilishasema tangu zamani kwamba sio tu sijui, sijui hata kama sijui. Sasa ukisema kwamba najifanya mjuaji wewe ndiye utakuwa hunijui.

Halafu quote yako umeikata, hujataka kuiweka yote, kwa makusudi. Kwa sababu ungeweka quote yote kusudio lako la kutaka kumfanya Kiranga ana ego trip lisingekamilika.

Kiranga ameonyesha kabisa kwenye hiyo post bashasha la mzaha linaishia wapi na habari za umakini zinaanzia wapi.

Nukuu yako imekata hii context ili unipake matope unavyopenda.

Mie kama nataka ku ego trip kuna sehemu nitaenda ku ego trip face to face, ego tripping JF halafu iweje?

Wewe unayesema nina ego-trip mwenyewe jina lako linakusuta.
 
Kwenye red. Absolutely right kwamba hivi viapo viko independent. Tatizo linakuja ni mtu wa aina gani anatakiwa kula kiapo? Waziri anatokana na ubunge, na ili uwe mbunge unatakiwa ufanye nini? Kinachogomba hapa ni utarabu kwamba unaanza na number 1,2,3 ... au unaanza na no 3.2.1?

Ili uwe mbunge unatakiwa uwe certified ama na Tume ya Uchaguzi ama na rais.

Hawa wanaoenda kuapishwa uwaziri ambao ndio kwanza wameteuliwa ubunge washakuwa certified na rais kwa hiyo ni wabunge tayari.

Soma ibara ya 68, soma wanaomchagua Spika ni kina nani.

Wanaomchagua Spika ni wabunge, hawahitaji kuapishwa na Spika kuwa wabunge.

Ukishasema viapo vipo independent, halafu ukavifanya viwe vinategemeana kama nambari 1,2,3 unajichanganya wewe mwenyewe na kutuchanganya wasomaji wako.
 
Back
Top Bottom