Erring on the Side of Caution: Kikwete usiwaapishe mawaziri wasioapishwa kuwa wabunge kwanza!

Nimeuliza swali hili mara mbili, hakuna aliyenijibu

Kuna sheria, kanuni na taratibu. Hata kama Rais hajakiuka sheria ni wazi amekiuka taratibu zilizopo miaka 50 iliyopita.
Tukikubali mkanganyiko huu ipo siku tutafanya uchaguzi jumapili matokeo jumatatu na jumatatu hiyo hiyo rais mteule ambaye ni 'Rais kamili' (hapaswi kula kiapo kwasababu ni formality)aliyetangazwa na tume ya uchaguzi akasimama magogoni mlangoni akiwa na mkuu wake wa majeshi, waziri mkuu mteule na baraza la mawaziri(ambao ni wabunge kamili wanasubiri tu kula kiapo ili washiriki shughuli za bunge).

Mbona watu washajibu hili la precedent.

Precedent ni Kikwete mwenyewe tumeambiwa.

Jakaya Kikwete - Wikipedia, the free encyclopedia

Kikwete throve in the military and grassroots party political organisation, mobilisation and administration until 1988 when he was appointed to join the Central Government. President Ally Hassan Mwinyi appointed him Member of Parliament and, simultaneously, Deputy Minister for Energy and Minerals on November 7, 1988
 
Nimesoma vizuri hoja za Kiranga na hoja za Werema; wote wawili nadhani wanagusia kwa mbali hoja yenyewe ya kuhalalisha hili. Nimerudi na kusoma vizuri tena Katiba na jawabu likko wazi sana kiasi kwamba nilivyoliona nimebakia kucheka kwamba ni rahisi kuliona lakini Werema hakulitoa hivyo; Kiranga ameligusia kwa mbali kidogo.

Ninaamini Rais anaweza kuwaapisha hawa kuwa mawaziri. Waliotetea na wale ambao tumepinga tumeangalia kitu kisicho sahihi!!! Kilikuwa mbele yetu lakini hatukukiweka sawasawa. Kiranga amekigusia in the negative ndio maana amepata shida kutushawishi lakini probaby ndiye aliyekuwa on the right track kuliko jibu la Werema (japo anakaribiana na Werema zaidi).
 
una maana hakuna haja ya kuwa na waziri kwa maana haandai bajeti sio.
huyo secretary hawajibiki kwa bunge, hali kadhalika mashirika.

Kwa nini unafikiri nina maana hakuna haja ya kuwa na waziri? Wapi nimesema waziri haandai bajeti?

nani kakwambia sekretari na mashirika hawawajibiki kwa bunge?

Ikiwa hata rais anawajibika kwa bunge, utasemaje sekretari wa wizara na muajiriwa wa shirika la umma hawajibiki kwa bunge? Au unaposema "hawajibiki" unamaanisha "hawajibiki moja kwa moja"? Kama ni hivyo tofauti kati ya kuwajibika na kuwajibika moja kwa moja -zaidi ya hops tu- ni nini?
 
Nimeshaandika kabla kwamba kufananisha uchaguzi wa rais na uchaguzi wa wabunge ni kile kinachoitwa "comparing apples to oranges".

Leo hii January Makamba na Mizengo Pinda wamekuwa wabunge biula kupigiwa kura na wananchi kwa sababu "wamepita bila kupingwa", hawakupata mpinzani. Inawezekana tukapata rais bila ya wananchi kumpigia kura kwa sababu hakuna mpinzani aliyejitokeza?

Nimeshaandika hapo juu kwamba ubunge unaanzia pale Tume ya Uchaguzi inapomtangaza mtu mshindi, au rais anapomcertify mtu fulani kwamba ni mbunge. Kwa hiyo hawa wateule wa rais ni wabunge tayari, ila itawabidi wale kiapo ili kuweza kufanya shughuli za kibunge (ukiondoa kumchagua Spika) kama katiba inavyosema.

Kwa hioyo kuwaapisha uwaziri hakuna makosa, kwa sababu ni wabunge tayari.

Si kweli kuwa kuwaapisha wabunge hao kuwa mawaziri hakuna makosa kwasababu ni wabunge tayari! Hao si wabunge bali ni "wabunge wateule" hadi watakapoapishwa kuwa wabunge kamili ndio inawapa uhalali wa kuendelea kuapishwa huo uwaziri.

Kumbuka pia wabunge wateule wanamchagua Spika kwanza mara tu wanapokutana Dodoma kabla ya shughuli nyingine yoyote ili nao waapishwe ndipo waanze kufanya kazi za kibunge. Kama Spika hajachaguliwa hakuna Bunge maana wabunge hawatakuwa na uhalali wa kufanya kazi za kibunge hadi wameapishwa.

Msichakachue Katiba! Kuapishwa uwaziri kabla ya kuapishwa ubunge ni ubakaji wa katiba. Hakuna yeyote anayewaapisha wabunge zaidi ya spika, waape kwanza nafasi za ubunge then waapishwe uwaziri.
 
Nimesoma vizuri hoja za Kiranga na hoja za Werema; wote wawili nadhani wanagusia kwa mbali hoja yenyewe ya kuhalalisha hili. Nimerudi na kusoma vizuri tena Katiba na jawabu likko wazi sana kiasi kwamba nilivyoliona nimebakia kucheka kwamba ni rahisi kuliona lakini Werema hakulitoa hivyo; Kiranga ameligusia kwa mbali kidogo.

Ninaamini Rais anaweza kuwaapisha hawa kuwa mawaziri. Waliotetea na wale ambao tumepinga tumeangalia kitu kisicho sahihi!!! Kilikuwa mbele yetu lakini hatukukiweka sawasawa. Kiranga amekigusia in the negative ndio maana amepata shida kutushawishi lakini probaby ndiye aliyekuwa on the right track kuliko jibu la Werema (japo anakaribiana na Werema zaidi).

Hahaha,

Kiranga for AG!

On a serious note, Kiranga labda anapata muda wa kwenda na watu toe to toe zaidi hapa wakati Werema katoa a top down communique.

Tupe maelezo zaidi, kitu gani kimekushawishi? ni kitu gani hicho nilichokigusia negative ambacho pengine ningeweza kukielezea vizuri zaidi positively?
 
Si kweli kuwa kuwaapisha wabunge hao kuwa mawaziri hakuna makosa kwasababu ni wabunge tayari! Hao si wabunge bali ni "wabunge wateule" hadi watakapoapishwa kuwa wabunge kamili ndio inawapa uhalali wa kuendelea kuapishwa huo uwaziri.

Kumbuka pia wabunge wateule wanamchagua Spika kwanza mara tu wanapokutana Dodoma kabla ya shughuli nyingine yoyote ili nao waapishwe ndipo waanze kufanya kazi za kibunge. Kama Spika hajachaguliwa hakuna Bunge maana wabunge hawatakuwa na uhalali wa kufanya kazi za kibunge hadi wameapishwa.

Msichakachue Katiba! Kuapishwa uwaziri kabla ya kuapishwa ubunge ni ubakaji wa katiba. Hakuna yeyote anayewaapisha wabunge zaidi ya spika, waape kwanza nafasi za ubunge then waapishwe uwaziri.

Hilo la "wabunge wateule" lipo katika kifungu gani cha katiba au sheria gani?

Ninayo katiba hapa, taja ibara.
 
Hahaha,

Kiranga for AG!

On a serious note, Kiranga labda anapata muda wa kwenda na watu toe to toe zaidi hapa wakati Werema katoa a top down communique.

Tupe maelezo zaidi, kitu gani kimekushawishi? ni kitu gani hicho nilichokigusia negative ambacho pengine ningeweza kukielezea vizuri zaidi positively?

Well.. clue iko kwenye 'kiapo cha uaminifu'.... naend akuangalia Avengers nikirudi nadhani nitaweka sawa. Jibu la Werema is pathetic for an AG to give! Angalau la kwako katika kuuliza uuliza maswali limefungua jawabu.
 
Nilijuwa tu utatoka kapa kwenye hiyo post ya MMJ!
 
Mbona unatoa majibu mepesi sana Kiranga? This is pure literal-traslation. Kama secretaries wanaweza kuandaa bajeti na wanafanya hivyo kwa nini bunge linawalipa wabunge kushiriki kuandaa bajeti? Kwa nini wasipumzike na kusubiri kila kitu kiletwe Dodoma?

Nimeeleza hapo juu kwamba bajeti inaandaliwa na sehemu tofauti, serikali, bunge mpaka mashirika ya umma. Kwa hiyo kusema kwamba kuandaa bajeti ni shughuli ya bunge, kwa maana ya kwamba mtu ambaye hana hadhi ya ubunge hatakiwi kuifanya (kama mnaosema waziri ambaye hajaapishwa ubunge hastahili kuandaa bajeti mnavyotaka tuamini) kutakuwa makosa, kwa sababu tushaona mpaka ma sekretari na wakurugenzi wa mashirika ya umma wanashiriki katika kuandaa bajeti.

Na hawa wote si wabunge na wala hawajaapishwa na Spika.

Sasa kama katibu mkuu wa wizara - mtu ambaye haapishwi na Spika kwa sababu si mbunge- anaweza kushiriki kuandaa bajeti kwa upande wa serikali, kwa nini waziri asiweze kufanya hivyo hivyo?
 
Nilijuwa tu utatoka kapa kwenye hiyo post ya MMJ!

mie si muaguzi, mtu kaeleza kwamba kaiona pointi yangu, lakini hajaeleza kaiona vipi, mie nitajuaje alichojua kabla mwenyewe hajanieleza?

Hata kama nafikiri nimemuelewa, kwa sababu mwenyewe yupo hapa, ninachofikiri mie kinaweza kuwa tofauti na alichoelewa yeye. Sipendi kufanya assumption kwa vitu ambavyo vinaweza kuwa verified kirahisi.

Wewe umeelewa alichoelewa kabla ya mwenyewe kutueleza hapa?

Una Extra Sensory Perception au telepathy?
 
Well.. clue iko kwenye 'kiapo cha uaminifu'.... naend akuangalia Avengers nikirudi nadhani nitaweka sawa. Jibu la Werema is pathetic for an AG to give! Angalau la kwako katika kuuliza uuliza maswali limefungua jawabu.

I have been hammering on this repeatedly.

What took you so long?
 
Hili nimeshali address kama mara nne hapo juu. Do not compare apples to oranges.

Mgombea ubunge akikosa mpinzani anapita bila kupigiwa kura kama alivyopita Mizengo Pinda au January Makamba, can you say the same for the presidency?

Unaona analogy yako inavyoanguka flat?

Hata hao akina Pinda na Januari pamoja na kupita bila kupingwa waliapishwa kwanza!
 
Hata hao akina Pinda na Januari pamoja na kupita bila kupingwa waliapishwa kwanza!

And your point is?

Mie nasema hawa hawakustahili kufika tatu kwa sababu hawakupata kuwa mbili, wewe unasema hata hao walishapita moja unusu!
 
Nachotaka kujua mimi kuna kiapogani kilichokusudiwa ktk ibara hii?..kama hakuna kwa nini kifungu hiki kipo kwenye katiba. Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Inawezekana hilo la JK ni kweli lakini labda kwa sababu hawakuwepo watu walioweza kuona hili tunaloliona sasa.. kwa sababu kama ni kweli kwanini Rais anasubiri wabunge waapishwe ndio ampate waziri mkuu na mawaziri wengine baada ya uchaguzi badala ya kuwatangaza kabla hawajaapishwa na wakati tayari ni wabunge wateule?

Kwamba ni wabunge ni wabunge kwa maana ya kwamba wamechaguliwa wawakilishi lakini si kwa maana ya kwamba wanafurahia haki na madaraka yao ya kibunge. Vinginevyo, kama tayari ni wabunge kamili kiapo cha nini basi? Kama kiapo hakiongezi lolote kwenye ubunge wao au kukamilisha process ya wao kuwa wabunge kwanini ni muhimu?
Mbunge anaweza kuhudhuria vikao vya halmashauri za LAGs kabla ya kuapishwa?
 
mie si muaguzi, mtu kaeleza kwamba kaiona pointi yangu, lakini hajaeleza kaiona vipi, mie nitajuaje alichojua kabla mwenyewe hajanieleza?

Hata kama nafikiri nimemuelewa, kwa sababu mwenyewe yupo hapa, ninachofikiri mie kinaweza kuwa tofauti na alichoelewa yeye. Sipendi kufanya assumption kwa vitu ambavyo vinaweza kuwa verified kirahisi.

Wewe umeelewa alichoelewa kabla ya mwenyewe kutueleza hapa?

Una Extra Sensory Perception au telepathy?

Ndio sababu nilikuwambia hapo awali uvute pumzi na usome kwa makini. Yaani mtu anaweza kukumbua mvua inanyesha na mko wote pamoja lakini bado ukamuuliza - kweli mvua inanyesha?!
 
Hahaha,

Kiranga for AG!

Kaka, taratibu! Tushazoea ego -trippin' zako kwa muda mrefu. Lakini, kwa taarifa yako, kuna Watanzania zaidi ya milioni 43, na pengine ni 0.01% tu kati yao wana access na mtandao wa JF. Usijifanye wewe ni mjuaji and so intellectually gifted as much as you would like to pretend to be so!
 
Mimi sioni ulazima wa mawaziri kuwa wabunge. Wabunge waachwe kuwa wabunge na mawaziri waachwe wawe watendaji wa serikali.

Haya mambo ya mawaziri kuwa lazima wawe wabunge ni upumbavu tu. Hivi kuna hata anayejua sababu ya ulazima huo ni nini?

Kwani mawaziri wasipokuwa wabunge watashindwa kufanya kazi zao?

Dawa hapa ni ndogo sana - ondoa ulazima wa mawaziri kuwa wabunge.

Kweli kabisa! Aisee mtafute Warioba na timu yake utoe hayo maoni maana ifike mahali tuwe kama Marekani na Ghana mawaziri wasitokane na wabunge. Wanasiasa wanatuvuruga sana kupewa kazi za wataalamu na watendaji serikalini. Ndio maana tupo hapa tulipo.
 
Kiranga

Kazi ya mbunge ni nini kabla ya kuapa ukiacha kuchagua spika,
I mean kama Mbatia tayari ni mbunge kabla ya kuapa atakuwa anafanya nini kwa mwezi mzima.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom