Erring on the Side of Caution: Kikwete usiwaapishe mawaziri wasioapishwa kuwa wabunge kwanza!

Suala limezua mjadala hivi bado linaonekana hakuna tatizo! Nani hasa humshauri mkuu wa kaya? Amshauri to move the court for clear interpretation, si kwa mwanasheria wa serikali! Nashauri tena hapa
 
Kama suala ni precedence ilikwisha tokea. Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mbunge na kisha akamteua kuwa Naibu waziri wa maji nishati na madini na akaanza kazi ya naibu waziri kabla hajaapa bungeni. Msingi hapa ni kwamba mbunge anakuwa mbunge Mara tu anapotangazwa na tume ya uchaguzi au kuteuliwa na malaka ya uteuzii yaani Rais
 
Kwani hii serikali ina uelewa kiasi gani wa katiba na mambo yanayowahusu watanzania? Naona kama inaenda hisia zaidi kuliko taratibu!
 
Hii nayo kali! Ni mawazo yako tu au kuna sehemu umedesa?

Hiyo ni wazi kabisa, unakuwa Mbunge kwa kuchaguliwa ama kuteuliwa, kinachofata ni kuapishwa, na kuapisha si lazima iwe kuna kikao cha bunge kinachoendelea au lazima ukaapishwe ukumbi wa bunge. Unaapishwa popote tu mradi, ni kweli umeteuliwa na inahakikishwa ni kweli ndiye wewe uliyeteuliwa.

Kiapo sio kazi, kazi ni uliyoteuliwa kuifanya, kiapo unaapishwa ukiwa wewe tayari upo kazini, huwezi kula kiapo kama bado hujateuliwa na haupo kazini.

Tusichanganye viapo na uteule.

Unakuwa waziri kwanza na kula kiapo baadae, unakuwa Mbunge kwanza na si kula kiapo. Huwezi kuapa kama wewe si waziri kama umeteuliwa kuwa Waziri na huwezi kuapa kama wewe si Mbunge kama umeteuliwa kuwa Mbunge.
 
Kama suala ni precedence ilikwisha tokea. Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mbunge na kisha akamteua kuwa Naibu waziri wa maji nishati na madini na akaanza kazi ya naibu waziri kabla hajaapa bungeni. Msingi hapa ni kwamba mbunge anakuwa mbunge Mara tu anapotangazwa na tume ya uchaguzi au kuteuliwa na malaka ya uteuzii yaani Rais

Well...inawezekana, lakini katiba inasemaje? au tunafumbia macho tu maana ni mambo yasiyotuhusu hayo?
 
Hiyo ni wai kabisa kwani unakuwa Mbunge kwa kuchaguliwa ama kuteuliwa, kinachofata ni kuapishwa, na kuapisha si lazima iwe kuna kikao cha bunge kinachoendelea au lazima ukaapishwe ukumbi wa bunge. Unaapishwa popote tu mradi, ni kweli umeteuliwa na inahakikishwa ni kweli ndiye wewe uliyeteuliwa.

Kiapo sio kazi, kazi ni ulyoteuliwa, kiapo unaapishwa ukiwa wewe tayari upo kazini, huwezi kula kiapo kama bado hujateuliwa na haupo kazini.

Tusichanganye viapo na uteule.

Unakuwa waziri kwanza na kula kiapo kwanza, unakuwa Mbunge kwanza na si kula kiapo.

Sheria na taratibu zinaruhusu kufanya hivyo?
 
Nakubaliana na MMKJJ -- ni lazima mkuu wan chi afuate sheria kanuni, desturi na hata mazoea ikibidi katika masuala ya namna hii. Na iwapo sheria/kanuni ina utata, au iko kimya basi ni vyema ku-act on the side of caution kama MMKJJ anayoshauri.

Lakini serikali yetu, hasa hii ya JK imekuwa ina act with impunity mara kadha – kwa kutegemea kwamba hakuna chochote kinachoweza kutokea, na kikitokea dola inaweza ku-crush tu, au kwamba wana-capitalize katika unyonge wetu.

Kuna mtu ametaja hapo nyuma kuhusu JK na EPA. Huyu mjamaa (JK) alikwenda Bungeni akawa Prosecutor na jaji na kutoa hukumu kwamba walioiba EPA warejeshe hela ama sivyo jela – au kitu namna hii kama wengi tulivyomuelewa.

Na ndivyo ikawa – waliorudisha (inasemekana) walipona, na waliogoma kurudisha (akina Farijala) wako jela.

Sijui JK alitumia kifungu gani cha Katiba, sheria ipi au kanuni gani.

Ni impunity alichikifanya na kwa lengo lakie maalum kama sote tunavyofahamu.

Ni sawasawa na Obama asimame katika Bunge la Congress na kuwahukumu watuhumiwa wa kikundi cha Mafia.

Na kabla ya uchaguzi wa mwaka juzi (2010) kulizuka suala (katika vikao vya CCM-NEC) kuhusu ugombea wa Dr Shein katika nafasi ya urais wa Zanzibar – kwamba hakuwa na sifa za kugombea chini ya Katiba/Sheria za huko kwa sababu hakuwa amejiandikisha kama mpiga kura katika daftari la kule.

Hilo suala likafunikwa ki-ujeuri jeuri tu bila shaka kutokana na ukweli kwamba chama kikuu cha upizani kule – CUF – tayari kilikuwa ne-utralised) katika makubaliano baina yake na CCM kwa hivyo hakukuwa na credible force ya kuweka pingamizi mahakamani.

Mimi naona wakati tunaelekea kwenye Katiba mpya, ni vyema tukaanza kuiheshimu hii ya sasa na iwapo kuna utata, yuwe tahadhari. Bila kuonyesha mfano huu, nina hofu kwamba hata Katiba tarajiwa itakuwa inakiukwa kiujeuri jeuri tu.

Kama suala ni precedence ilikwisha tokea. Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mbunge na kisha akamteua kuwa Naibu waziri wa maji nishati na madini na akaanza kazi ya naibu waziri kabla hajaapa bungeni. Msingi hapa ni kwamba mbunge anakuwa mbunge Mara tu anapotangazwa na tume ya uchaguzi au kuteuliwa na malaka ya uteuzii yaani Rais
Nini maana ya kiapo?Kiapo hakina uzito wowote?kama mbunge anakuwa mbunge pindi tu anapochaguliwa, je kwa suala la raisi inakuwaje?Marekani kama tujuavyo raisi anachaguliwa mwishoni mwa mwaka kabla ya raisi aliyepo madarakani kumaliza kipindi chake lakini raisi mteule anaapishwa katikati ya Januari.Hata jirani zetu Kenya nao katika katiba yao mpya wameweka utaratibu huo kuwa raisi anashika madaraka na kuwa na mamlaka baada ya kuapishwa tu(Hii ni kuweka tu mambo wazi kwa sababu ilikuwa inajulikana kuwa mamlaka ya raisi yanaanza baada ya kuapishwa ndio maana Kibaki aliapishwa usiku ili keshoye aanze kuwashughulikia 'wapinzani'),why can'twe apply the same reasoning and argumemt on MPs?Please convince me otherwise...
 
Are you trying to say that 'certification' or the swearing in of members of parliament is a mere formality,an insignificant event that can be easily overlooked?That the swearing in of MPs serves no purpose except in the election of the Speaker of the house of assembly?Then,why do MPs elected after a by-election when there is no need to elect a speaker also go through the 'mere formality' of being sworn in?
If the law is not clear then it is better to follow a routine that stirs away from controversy.

1. Please understand that certification and swearing in are two different things. certification is done by NEC when the winner is announced, the announcement actually carries a declaration declaring the winner to be the legal MP. This is why a person declared a winner by the NEC can elect the Speaker, and the constitution recognizes this person as an MP even before electiong the Speaker.

2. the oath cannot be overlooked because without the oath an MP cannot perform parliamentary duties other than electing the Speaker. That same oath is negligible in the context of one being sworn in as a minister because a minister need not perform parliamentary duties.
 
Mkuu Kiranga,

Sheria zetu nyingi tume ziadapt hata bila kujua zinamaanisha nini.

Kiapo is oarth to the office. Rais akishachaguliwa anakuwa president elect mpaka akisha kula kiapo. Presidential institution inamuingia kwa kiapo tuu. Vivyo hivyo kwa wabunge, ubunge sio baada ya kuchaguliwa bali baada ya kiapo.

Swali la msingi ni ubunge unaanzia wapi?, ni baada tuu ya kuchaguliwa au kuapishwa?. Kama ni baada ya kuchaguliwa, basi kuapishwa hakuna maana yoyote!.

Nimebahatika kuhudhuria mabunge 4 yakiapishwa pale Dodoma, wabunge nao huitwa wabunge wateule!.

kule kwa EMT nilijibu hivi, na hapa ninajibu vile vile.

Nimeshaandika kabla kwamba kufananisha uchaguzi wa rais na uchaguzi wa wabunge ni kile kinachoitwa "comparing apples to oranges".

Leo hii January Makamba na Mizengo Pinda wamekuwa wabunge biula kupigiwa kura na wananchi kwa sababu "wamepita bila kupingwa", hawakupata mpinzani. Inawezekana tukapata rais bila ya wananchi kumpigia kura kwa sababu hakuna mpinzani aliyejitokeza?

Nimeshaandika hapo juu kwamba ubunge unaanzia pale Tume ya Uchaguzi inapomtangaza mtu mshindi, au rais anapomcertify mtu fulani kwamba ni mbunge. Kwa hiyo hawa wateule wa rais ni wabunge tayari, ila itawabidi wale kiapo ili kuweza kufanya shughuli za kibunge (ukiondoa kumchagua Spika) kama katiba inavyosema.

Kwa hioyo kuwaapisha uwaziri hakuna makosa, kwa sababu ni wabunge tayari.
 
Mkuu Kiranga, you have raised an interesting point, you seem to imply that "taking an oath" is insignificant, out of topic within the same domain, can we say that "Someone becomes a president as soon as the electoral committee announces the winner, one need not be sworn in"

Nimeeleza hapo juu kufananisha uchaguzi wa rais na uchaguzi wa mbunge kuwa ni kufananisha visivyofananishika.

Huwezi kusema kati ya rangi ya bluu na utamu wa muwa kipi kimezidi kingine? unapofananisha rangi fananisha rangi, unapofananisha utamu fananisha utamu.

Urais na ubunge domains tofauti, process za uchaguzi tofauti, sheria tofauti, utavifananishaje vitu tofauti?

Mbunge anaweza kuteuliwa kuwa mbunge, rais je? Mtu anaweza kuwa mbunge bila hata ya kura moja kwa "kupita bila kupingwa", rais je?

Kiapo cha rais ni "oath of office", kiapo cha mbunge ni "oath of allegiance", tofauti, haviwezi kulinganishwa.
 
Kama suala ni precedence ilikwisha tokea. Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mbunge na kisha akamteua kuwa Naibu waziri wa maji nishati na madini na akaanza kazi ya naibu waziri kabla hajaapa bungeni. Msingi hapa ni kwamba mbunge anakuwa mbunge Mara tu anapotangazwa na tume ya uchaguzi au kuteuliwa na malaka ya uteuzii yaani Rais

Ahsante kwa kutoa precedent hii iliyotupa president.
 
Kosa kubwa ambablo binafsi naamini ni mahakama inastahili kuamua ni phrase ya "shughuli za kibunge". Watu wengi wanatafsiri kama "shughuli bungeni".Shughuli za kibunge na 'shughuli bungeni' ni vitu viwili tofauti. Shughuli za kidaktari na shughuli hsopitali si kitu kimoja.

Kwa mfano, mtu aliyesomea uwakili akapasi hadi mtihani anaweza kuwa na sifa zote za kufanya kazi za uwakili. Lakini ili aweze kujitambulisha kuwa ni wakili ni lazimaale kiapo cha kazi hiyo. Hata daktari ni hivyo hivyo, anaweza akawa amehitimu masomo yote na kufanya vizuri lakini ili aweze kuingia katika udaktari ni lazima aape kwanza. Sasa udaktari siyo kutibu tu au kugawa dawa tu; ni mjumuisho wa mambo mengi yanayohusiana nahilo.

Watuwengi na hata Werema mmojawapo wanapozungumzia shughuli za "kibunge" wanaifunga hii kumaanisha ni yale ambayo mbunge anayafanya bungeni tu na yanayohusiana na mambo ya bunge tu. Naamini tafsiri hii si sahihi. Tafsiri sahihi ina maana ya mambo yote abmayo yanaweza kufanywa na mbunge ikiwemo kuwa waziri!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Well...inawezekana, lakini katiba inasemaje? au tunafumbia macho tu maana ni mambo yasiyotuhusu hayo?

Ibara ya 68 inatuambia "wabunge" wanamchagua Spika.

Na kwa sababu wanaomchagua Spika wanakuwa hawajaapishwa na Spika bado (kwa sababu Spika hajachaguliwa) kwa hivyo basi, wabunge hawa wanaomchagua Spika wanakuwa wamepata ubunge wao kabla ya kumchagua Spika, na kwa hiyo, kabla hawajaapishwa.
 
Kama suala ni precedence ilikwisha tokea. Rais Ali Hassan Mwinyi alimteua Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mbunge na kisha akamteua kuwa Naibu waziri wa maji nishati na madini na akaanza kazi ya naibu waziri kabla hajaapa bungeni. Msingi hapa ni kwamba mbunge anakuwa mbunge Mara tu anapotangazwa na tume ya uchaguzi au kuteuliwa na malaka ya uteuzii yaani Rais

Ilikuwa lini hii? na Kikwete aliapishwa lini kuwa mbunge? maana kumbuka kuna vitu viliwezekana wakati wa chama kimoja na ambavyo havikuwezekana baada ya vyama vingi...
 
Nakubaliana na MMKJJ -- ni lazima mkuu wan chi afuate sheria kanuni, desturi na hata mazoea ikibidi katika masuala ya namna hii. Na iwapo sheria/kanuni ina utata, au iko kimya basi ni vyema ku-act on the side of caution kama MMKJJ anayoshauri.

Lakini serikali yetu, hasa hii ya JK imekuwa ina act with impunity mara kadha – kwa kutegemea kwamba hakuna chochote kinachoweza kutokea, na kikitokea dola inaweza ku-crush tu, au kwamba wana-capitalize katika unyonge wetu.

Kuna mtu ametaja hapo nyuma kuhusu JK na EPA. Huyu mjamaa (JK) alikwenda Bungeni akawa Prosecutor na jaji na kutoa hukumu kwamba walioiba EPA warejeshe hela ama sivyo jela – au kitu namna hii kama wengi tulivyomuelewa.

Na ndivyo ikawa – waliorudisha (inasemekana) walipona, na waliogoma kurudisha (akina Farijala) wako jela.

Sijui JK alitumia kifungu gani cha Katiba, sheria ipi au kanuni gani.

Ni impunity alichikifanya na kwa lengo lakie maalum kama sote tunavyofahamu.

Ni sawasawa na Obama asimame katika Bunge la Congress na kuwahukumu watuhumiwa wa kikundi cha Mafia.

Na kabla ya uchaguzi wa mwaka juzi (2010) kulizuka suala (katika vikao vya CCM-NEC) kuhusu ugombea wa Dr Shein katika nafasi ya urais wa Zanzibar – kwamba hakuwa na sifa za kugombea chini ya Katiba/Sheria za huko kwa sababu hakuwa amejiandikisha kama mpiga kura katika daftari la kule.

Hilo suala likafunikwa ki-ujeuri jeuri tu bila shaka kutokana na ukweli kwamba chama kikuu cha upizani kule – CUF – tayari kilikuwa ne-utralised) katika makubaliano baina yake na CCM kwa hivyo hakukuwa na credible force ya kuweka pingamizi mahakamani.

Mimi naona wakati tunaelekea kwenye Katiba mpya, ni vyema tukaanza kuiheshimu hii ya sasa na iwapo kuna utata, yuwe tahadhari. Bila kuonyesha mfano huu, nina hofu kwamba hata Katiba tarajiwa itakuwa inakiukwa kiujeuri jeuri tu.

Katiba, sheria, kanuni zote hazina utata kuhusu mtu kuapishwa uwaziri kabla ya ubunge.

Kikwete anajua hili si kosa kwa sababu ibara ya 68 ya katiba iko upande wake.

Isitoshe yeye mwenyewe ni mfano hai na "precedent" ya mtu aliyeteuliwa ubunge na kuapishwa uwaziri kabla ya ubunge.
 
Ibara ya 68 inatuambia "wabunge" wanamchagua Spika.

Na kwa sababu wanaomchagua Spika wanakuwa hawajaapishwa na Spika bado (kwa sababu Spika hajachaguliwa) kwa hivyo basi, wabunge hawa wanaomchagua Spika wanakuwa wamepata ubunge wao kabla ya kumchagua Spika, na kwa hiyo, kabla hawajaapishwa.

ndicho kitu pekee ambacho katiba inawaruhusu kufanya kabla hawajaapishwa.
 
Nini maana ya kiapo?Kiapo hakina uzito wowote?kama mbunge anakuwa mbunge pindi tu anapochaguliwa, je kwa suala la raisi inakuwaje?Marekani kama tujuavyo raisi anachaguliwa mwishoni mwa mwaka kabla ya raisi aliyepo madarakani kumaliza kipindi chake lakini raisi mteule anaapishwa katikati ya Januari.Hata jirani zetu Kenya nao katika katiba yao mpya wameweka utaratibu huo kuwa raisi anashika madaraka na kuwa na mamlaka baada ya kuapishwa tu(Hii ni kuweka tu mambo wazi kwa sababu ilikuwa inajulikana kuwa mamlaka ya raisi yanaanza baada ya kuapishwa ndio maana Kibaki aliapishwa usiku ili keshoye aanze kuwashughulikia 'wapinzani'),why can'twe apply the same reasoning and argumemt on MPs?Please convince me otherwise...

Kuna viapo tofauti vyenye maana tofauti, kuna "oath of office", "oath of allegiance" etc.

Kabla ya kuvirundika viapo vyote katika kapu moja inabidi ujue unaongelea kiapo gani.
 
ndicho kitu pekee ambacho katiba inawaruhusu kufanya kabla hawajaapishwa.

Sawa,

Hakuna anayesema hawa wabunge walioteuliwa na rais wanataka kufanya zaidi (mambo ya ubunge) kabla ya kuapishwa na Spika.

Swala hapa, wao ni wabunge kabla ya kuapishwa ama la?

Ibara ya 68 inatuambia ni wabunge.

Hivyo Kikwete anapowaapisha kuwa mawaziri washakuwa wabunge tayari. Kikwete mwenyewe aliapishwa hivyo hivyo kwa mujibu wa mdau mmoja hapa. Kitu ambacho kinasadikika kwa sababu Kikwete first time alivyoingia bungeni alikuwa mbunge wa kuteuliwa na rais na akaingia unaibu waziri moja kwa moja.
 
Hivi inakuwaje mwanasheria mkuu anashindwa kuona makosa ya waziwazi kama haya? Na kama haoni hili anawezaje kusimamia mikataba ya kibepari kama Barrick na Uranium guys toka Marekani? Kama hao mawaziri wataapishwa kesho ni wazi wakubwa watakuwa wamedharau katiba! Hilo halina ubishi. Na watu wataanza ku-question dhamira ya serikali kwa wananchi wake. Nchi haiwezi kuongozwa na watu ambao hawajala kiapo! Hilo halipo sehemu yoyote duniani. Hakuna!

Ni lazima watu waape kwa mujibu sheria na taratibu zilizoweka. Serikali inatakiwa sasa ielewe madhara ya tabia yake to the rest of the population. Wakishaonesha waziwazi kwamba hawaheshimu katiba ya nchi wanategemea wananchi waiheshimu kwa vipi?

Pili, kuna kitu kingine office ya mwanasheria mkuu ajiridhishe. Nacho ni uraia wa wabunge wote wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri. Narudia, office ya mwanasheria mkuu ihakiki na kujiridhisha uraia wa wabunge wote wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri.
 
Back
Top Bottom